Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa ka Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Avelyne Mushi baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Bukoba, kuanza ziara a kikazi ya siku moja mkoani Kagera.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia Mwenyekiti wa Chama Cha Walemavu wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Simon Andrea, baada ya kufungua Baraza la Vijana wa CCM wilaya hiyo, jana, May 25, kwenye Uwanja wa Mashujaa, wilayani humo. Waliosimama ni baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM walioshiriki ufunguzi huo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akikata utepe kuingia kwenye kambi ya Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM, wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, kwa ajili ya kufungua baraza hilo la mwaka.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimkabidhi cheti Kamanda wa Vijana wa CCM mkoa wa Kagera, Dioniz Malinzi kwa kuwa mmoja wa waliowezesha kambi hiyo ya Baraza la Vijana kufanyika.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na viongozi katika Ofisi ya CCM mkoa wa Kagera.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitoa salam za Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwenye msiba wa mtumishi wa siku nyingi waserikali, Balozi, Dk. Vedasto Kyaruzi, mjini Bukoba, baada ya kwenda kwenye msiba huo wakati wa kuaga mwili wa marehemu tayari kwa mazishi yaliyofanyika jana mjini Bukoba.
Vijana wa CCM waliopiga kambi hiyo ya Baraza la Vijana, Missenyi, wakimsikiliza Nape alipowahutubia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Tuwe na mtazamo tofauti kuhusu walemavu. Baada ya kuona hali ilivyo huku ughaibuni, ambako walemavu kama huyu anayeonekana pichani wana vyombo vya kusafiria, inahuzunisha kuona wa kwetu wanatambaa chini, na jamii inaona ni sawa tu.

    Baada ya kuona huku ughaibuni hata majengo hujengwa yakiwa na namna ya kuwawezesha walemavu hao kuingia na kutoka kwa urahisi, inahuzunisha kuona hali ilivyo Tanzania.

    Tanzania ina utajiri mkubwa wa rasilimali. Ingewezekana kabisa kuwapa usafiri hao walemavu wanaotambaa. Lakini tuko radhi kuwaona waporaji mbali mbali wakitafuna utajiri huo wakati wenye mahitaji wanateseka.

    Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa hotuba kuhusu suala hili la walemavu na mahitaji yao. Nadhani ilikuwa mwaka 1972. Hapo kwenye picha wanaonekana watu wanaoitwa viongozi. Inakuwaje wasiwe na mtazamo wa kurekebisha hali ya huyu mlemavu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2012

    Jamani huyu Mzee ni mpigania uhuru, mmoja kati ya waasisi wa harakati za uhuru wa tanganyika kupitia chama cha taa na tanu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2012

    Sasa mwenyekiti wa walemavu hata baskeli ya walemavu mmeshindwa kumtafutia? Ina mana wakishasalimiana hapo ndo wamnyanyuwe au wamuwache tu ajiburure peke yake? Jamani zingatieni utu first, mengine ni ya kuja na kupita yakasahaulika.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 26, 2012

    ziara ya kikazi siku moja kula kula ccm siku zenu za mwisho zinakaribia tutawapandisha mahakamani mmoja mmoja hatutaki kuchezewa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...