Meli hiyo inavyoonekana kwa Nje
 Meli hiyo inavyoonekana kwa ndani.
Meli hiyo inavyoonekana kwa Ujumla
---- .
Azam yaamua kufanya kweli na hivi karibuni meli ya kisasa iko mbioni  kuzinduliwa ambayo ikawezesha watu kwenda na magari yao Zanzibar. Meli hiyo inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.
KAMPUNI ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa ya kisasa kwaajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja. Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa. 

 Mohamedi alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200 ambapo abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo.

Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe, Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2012

    Assalama Leko zako Muungwana Said S.Bakhressa na Azzam kwa ujumla!

    Haya ndiyo mambo Sheikh lililobaki ni kuukamilisha ule 'Ungo' Uwanja wa Timu ya Mpira kule Chamazi-Mbagala ili na sisi wana Mbagala tuweze kujitetea dhidi ya dharau za Wanamuziki wa Kizazi kipya juu yetu kuwa Mbagala kila nyumba ni jalala!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2012

    Hiyo ni ferry

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 20, 2012

    Tatizo ni moja tu ambalo kwetu wakaazi wa shangani imekuwa kero kwa muda mkubwa sasa. Tatizo lenyewe ni sehemu ya kupakia na kushushia magari na abiria wa meli hiyo.

    Kwa sasa meli zinazosafirishia magari kwenda dar na pemba hutumia ufukwe wa hapa shangani karibu na posta na benki kuu ya biashara. Kwa vile hakuna sehemu maalum ya kuegesha magari yanayongojea kusafirishwa, sehemu hiyo huwa daima imejaa magari na kusababisha msungomano wa magari na wapita njia katika sehemu hiyo.

    Ikiwa Azam nao watatumia sehemu hiyo basi naona patakuwa hapapitiki tena hata kwa miguu.

    Kinachochekesha hapa ni ule mtindo wa magari kuegeshwa hapa na kusubiri hadi maji ya kupwe ili meli iweze kusogea karibu na kupakia magari, au mara nyengine meli inasubiri maji yajae kiasi ili iweze kuelea na kuondoka. Hapatumiwi watu wa taaluma ya hali ya hewa na bahari kujua ni time gani kwa siku gani kutakuwa high au low tides.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 20, 2012

    Hongera Azam, wewe kweli ni mzalendo
    kwani unajenga nchi, sio hao mafisadi
    wanaiba na kupeleka ulaya.
    Mungu akuzidishie
    Amen
    Ras z

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 20, 2012

    ni nzuri sana afadhali.ila tunaomba kuona sehemu ya abiri au vyumbani.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 20, 2012

    si mchezo hongera sana said s bakhressa wewe ndio mbunifu wa hali ya juu

    hizo ndio meli zinazotakiwa kuwepo hapo nchini sio zile meli za mizigo zilizouwa raia wasiokuwa na hatia zaidi ya 2000

    mungu akuzidishie zaidi ya hapo ili tuzidi kufaidika na mafanikio yako

    sasa nitakuwa nikisafiri kuelekea zanzibar na suzuki yangu nikifika napiga misele mji wa amani nikimaliza narudi na suzuki yangu

    big up Azam Familly.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 20, 2012

    Ahsante sana AZAM, mimi naomba ikiwezekana tuulizie kabisa kwenye Idara zinazohusika, masharti ya kwenda na gari Zanzibar na au Dar yatakuwa yepi ili kuondoa usumbufu. Mkipata tubandikie hapahap kwenye blog yetu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 20, 2012

    Sasa niuthibitisho tosha namna gani tunavyoweza kuimarisha muungano wetu wasiyopenda wanywe sumu,Ahsante ndugu baresa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 20, 2012

    Lugha iliyotumika katika kichwa cha habar hii nadhani sio sahihi.Watu hawataenda zanzibar kwa magari yao bali wataenda zanzibar pamoja na mgari yao.Kichwa cha habar mm kilinifanya nidhani kumejengwa au kutajengwa daraja lakuunganisha dar na zenji.Hivyo kichwa cha habr kinatoa ujumbe tofauti.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 20, 2012

    Ongera Azam

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 20, 2012

    hizo notkomail no sawa km ngapi/hr. itachukua mda gani kwa safari 1?
    hongera sana!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 20, 2012

    notkomail 20 ni sawa na kutumia dakika ngapi toka Dar kwenda Zanzibar, habari haijakamilika kipande hiki cha speed hasa ukizingatia sie sio wataalamu wa vyombo vya majini ingekuwa kama ile ya gari ya KM/HR tungetumia general knowledge ya physics ya form two. WANAOJUA WATUJUZE

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 20, 2012

    Tanga na Mtwara je? Ili tukimbie Foleni na ajali za Barabarani. Pia muanzishe USAFIRI BASI MBEZI,MPAKA SLIPWAY MSASANI KUTOKA HAPO MPAKA FERRY AU NYENGINE INATOkEA KAWE AU MSASANI CINE CLUB, ILI TUKIMBIE FOLENI VITU VIDOGO TUNASHINDWA TUNAJUWA WENGINE TUKITAKA KUFANYA AZAM WANATUZUIA. PANDU

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 20, 2012

    USALAMA NAO UWEPO UOKOAJI NAO UWEPO WAWE MAKINI MSIWEKE TAMAA MBELE TU ALLAH ATUZIDISHIE NA KUTULINDA NA TUONGEZEE BIDII YA MAFANIKIO.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 20, 2012

    Kigamboni sasa hivi ni kero ngoma kama hii hali ingekuwa shwari kabisa hata kwa gharama ya juu kidogo

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 20, 2012

    Hii nzuri, ila nakushauri uvushie watu na magari kwenda kigamboni italipa, ukipeleka znz-dar inaweza isijae na ukaishia kupata hasara, vusha kigamboni hao TEMESA wamelala usingizi biashara ipo hapo.
    Hongera Bakhresa huu ndio uwekezaji!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 20, 2012

    Hii ni Boat nadhani, sio Meli. Tutofautishe Ziwa na Bahari, sio kila Ziwa ni Bahari.
    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 20, 2012

    20 nautical miles (Nm) ni sawa na 37 km/hr

    ReplyDelete
  19. Mwangwitwa ChrisJune 20, 2012

    huu ndio uwekezaji watanzania wanautaka kama huyu AZAM safi sana yeye analeta hapa nyumbani lakini hawa ndugu zetu mafisadi wao wanaiba wanawapelekea hao wazungu ambao wanatuletea misaada mpaka wanatushangaa hawa jamaa vipi?bajeti yao tunawasaidia bado wanaiba,kweli akili ni nywele kila mtu anazo,nichukue nafasi ya kukupongeza AZAM,sasa issue ni namna ya kupata ajira kwenye hiyo meli

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 20, 2012

    Mambo ya msingi ni kujenga sehemu ya kupakia/pakua magari katika kila bandari.
    Tuelezwe taratibu za kwenda na magari Zanzibar itakuwaje? je Zanzibar ni kama Moro tu kuwa naenda halafu hamna masharti mengine?
    Gharama zinakadiriwa kuwaje?
    Je kuna haja ya kufanyba 'booking' mapema au ni kama pale Kigamboni, wa kwanza kufika ndio wa kwanza kuhudumiwa (ukiondoa mafisadi wachache wanaoruka foleni)

    Shukrani sana kwa huduma hii

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 21, 2012

    Muungano unahitaji watu kama hawa:

    Watu muhimu katika Muungano ni wale wanaoona faida zake akiwemo Sheikh Said Seif Bakhressa!

    Ndiye anatuwakilisha nchini na mwana mapinduzi mzuri, Wapinga Muungano hatuna muda wa kuwatimizia mahitaji yao!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...