Habari iliyotufikia chumba cha habari cha Globu ya Jamii hivi punde,inaeleza kuwa watu watatu wamepoteza maisha papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya sana katika ajali iliyokutanisha magari mawili iliyotokea hivi sasa maeneo ya Tegeta Kibaoni njia panda ya kwenda Wazo Hii jijini Dar.

Chanzo cha ajali hiyo inasemekana ni Lori lililokuwa likitokea Wazo Hill ambalo lilikuwa kwenye mwendo kasi kufeli breki na kwenda kugonga gari la abiria likikokuwa limesimama hapo Kibaoni kupakia abiria.

Shughuli ya kuokoa majeruhi kwenye ajali hiyo inaendelea hivi sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2012

    Sehemu hiyo ajali za aina hiyo hiyo zinatokea kila wakati na kuua watu wengi, zikihusisha magari makubwa ya mchango, kifusi, mawe au ciment yakitokea wazo hill na kushindwa kukata kona kuingia barabara kuu ya bagamoyo. Kwa kuwa hivi sasa barabara hiyo inatengenezwa ni bora ufumbuzi wa kudumu ufanyike wakati huu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...