Anko Michuzi,
Naomba unipe nafasi ili nitoe dukuduku yangu kuhusiana na stendi za mabasi. Hivi karibuni nilikuwa na wageni kutoka nje wakiwa na watoto na walikuwa wanaitembelea Tanzania kwa usafiri wa basi. Walianzia DAR wakitaka kuelekea Moshi. 



Stendi ya Ubungo kulikuwa vurugu tupu, kila mtu kelele walisukumwa mpaka wakapoteza mizigo. Ilikuwa ni vurugu ya aibu. Kila muuza tiketi anatufuata huku akipiga kelele. Tuliokolewa na Dereva Taxi mmoja ambaye alitushusha njiani ili tupandie basi hapo, kwani kituoni haikuwezekana. Safari  haikuwa mbaya ila kufika moshi vurugu nyingine. Baada ya Moshi walielekea Tanga.


 Kwa kweli hata mimi nilishangazwa na tofauti kati ya makonda na wauza tiketi wa stendi ya Tanga na ile ya DAR, MOSHI na ARUSHA. Tulifika stendi ya mabasi Tanga na alitufuata kijana mmoja kutuuliza kama ni wasafiri. Alianza kwa salamu Je Waungwana hamjambo? Baada ya kumjibu akauliza mwasafiri leo? tukasema ndio. Wapi? Arusha au Dar? tukamjibu Dar.  Mnahitaji tiketi? Nikamwambia tunaulizia ofisi ya basi fulani ambalo ninalifahamu kuwa la uhakika kwa ruti hii. Akatuambia ofisi yake ile pale, ongea na Mzee yule mwenye kofia. Akamalizia Safari njema.


 Mimi nilishangazwa na ustaarabu huu, kwani wakati wote tunaongea nae hakuna muuzaji wa tiketi yeyote alikuja kutusumbua. Na yeye mwenyewe alikuwa ameshikilia kitabu cha tiketi basi nikamuuliza je basi lako linakwenda wapi? Akasema Dar.  Huko, huko tunakokwenda sisi.Nilifurahishwa sana na ustaarabu huu na umakini wake basi nikamkaribisha soda baada ya kununua tiketi zetu.


 Nikajiuliza ni kwanini ustaarabu huu wa Tanga hauigwi kwenye Stendi zingine? Hivi hizi purukushani kwenye stendi ya mabasi ndio njia halali ya kutafuta maisha? 


Ningependa sana kusikia toka kwa wafanyakazi wa Stendi ustaarabu ni bei gani?

Asante
Mdau  Waja Leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2012

    makondakta hawana ustaarabu kabisa. kuna mmoja wa kwenye basi la Shabiby sina hamu naye nilitamani nimrushie ngumi!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2012

    Kweli kabisa Mkuu! Ustaarabu huu unahitajika si kwa makonda peke yao bali hata abiria. Mfano abiria vituo vya daladala Dar es Salaam ni vurugu tupu. Mbona tusiwe na utaratibu wa kupanga foleni kama vile ilivyo nchi jirani? Kituo cha mwanzo/mwisho, yaani terminus, watu hupanga foleni na kila gari linapofika wanapakia kwa utaratibu huo. Hivi hata kibibi aliyefika mapema naye atatoka mapema na bouncer aliyechelewa kufika naye atatoka kwa muda wake.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2012

    ANO Stated:

    Nakubaliana sana na hilo jambo kuhusiana ustaarabu hapo kwenye kituo cha mabasi (TERMINAL) Ubungo. Binafsi nilipata a very bad experience wakati nilikuwa nasafiri kwenda Mbeya. Kama tujuavyo mabasi yaendayo Mbeya yanaondoka asubuhi sana. Nilipofika hapo terminal bado nipo kwenye TAXI watu walitokea pande zote na kuaanza kuizunguka TAXI hata hawakupi nafasi ya kutoka. Nilipofanikiwa kushuka mizigo yangu ilikuwa inagombaniwa na hao wabeba mizigo, eventually nilipopatana na mmoja wa hao wabeba mizigo wenye wheel barrows, mara alipoweka mizigo yangu kwenye wheel barrow lake, alianza kukimbia na mizigo yangu na mimi nikaanza kukimbia nyuma yake huku nikimpigia makele asimame lakini akaendelea kukimbia haraka sana mpaka akatoka nje ya gate hapo Ubungo. Cha kushangaza Polisi hapo Ubungo walikuwa wakipita na wakaona kinachoendelea but they could not be bothered. Toka siku hiyo anytime nikiwa nasafiri na nikifikiria kwenda hapo Ubungo Terminal Moyo wangu unaenda mbio sana. Wakati umefika watanzania inabidi tuwe waastarabu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2012

    Wachaga wanauhusiano gani na kukosekana kwa ustaarabu, tambua huu ni mfumo mbovu wa watendaji wetu na wamiliki wa mabasi. kama mabasi yote yatakuwa na ofisi za uhakika, kubadili mfumo wa kukata tiketi kwa kutumia huduma za electronic kadhia hii itakuwa haipo, ufike wakati wa sis watanzania kubadilika

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2012

    NATUMAI MHESHIMIWA MWAKYEMBE ANALIONA HILI NA ATALIFANYIA KAZI. STENDI ZA MABASI ZINAATHIRI SAFARI NA KUWANYIMA WAFANYABIASHARA WA UHAKIKA HAKI ZAO. MATAPELI WAMEJAA KILA KONA. MABASI NDIO USAFIRI WA WATANZANIA WENGI WAENDAO MIKOA MBALIMBALI. WAHUSIKA TUNAOMBA MLIFANYIE KAZI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...