I.          UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Kambi ya Upinzani, ninatoa maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Bajeti ya Nchi ya mwaka wa fedha 2012/2013 kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Kifungu cha 99(7) toleo la Mwaka 2007.

Mheshimiwa Spika, Natoa pongezi za dhati kabisa kwa Ndugu William Augustao Mgimwa, Mbunge wa Jimbo la Kalenga mkoani Iringa kwa kuteuliwa na Rais kuwa Waziri wa Fedha na Uchumi. Vile vile nawapongeza Ndugu Saada Mkuya na Ndugu Janeth Mbene kwa kuteuliwa kwao kuwa Wabunge na baadaye kuwa Manaibu Mawaziri katika Wizara hii nyeti sana.  Ninawapa pole pia maana Wizara ya Fedha sio Wizara lelemama. Kambi ya Upinzani itaendelea kuisimamia Wizara hii kwa ukaribu sana kama ilivyofanya katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Mtakapofanya vizuri tutawapongeza ili muongeze juhudi, mtakapoharibu tutawawajibisha.
 
Kusoma hotuba kamili ya Mh Zitto Kabwe BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2012

    Anonymous

    chomoeni bajeti ya serikali yenye ulaji mtupu ipitishwe ile ya Upinzani. Serikali na kuwa na watalaam bado inababaisha! Masikitiko matupu.

    Musa bin Musa

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2012

    Mhe. Zitto hivi madai ya wazungu ni ya kweli kuwa Tanzania kuna pesa nyingi lakini wabongo wanazikwepa kwa kukimbilia nje, kama vile Ugiriki, Italy, spain, Portugal, USA (Nchi ambozo chumi zake ni mbovu) nitaje nchi hizo kwa uchache? Lakini wabongo wa nje wakija kuanza kuwekeza nyumbani hawatakwamishwa? Tunaomba tuakikishiwe kama chadema na ccm mtatusaidia kwa hilo. Inasemekana Ushuru wa kuingiza matendea kazi bandarini bodo kigongo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2012

    Ni muhimu mawazo haya kufanyiwa kazi pia na siyo ya kupuuzwa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...