Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mradi wa kufyatua matofali yaliyotengenezwa kwa mashine ya Hydrafoam kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari ya Mboga,wilayani  Bagamoyo. Mashine  hiyo yenye thamani ya Shilingi Milioni Sabini 70m/- imetolewa na Rais Kikwete kama msaada kwa vijana waliounda ushirika ili kuboresha maisha yao kwa kufanya  miradi mbalimbali ya ujenzi na uzalishaji, Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu
 Matofali imara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2012

    Hongera sana JK. Umefanya la maana kuhakikisha elimu inadumishwa nyumbani kwako. Pia Chuo kikuu cha Dom ni jitihada zako japo hakikujengwa na CCM kama ccm wanavyotaka kuudanganya umma wa watanzania. Binafsi nitakukumbuka kwa kuweka mbele elimu.

    Mdau Alphonce.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2012

    HONGERA MHE,JK kwa kuwawezesha vijana kuendesha maisha yao.
    pia huo ufyatuaji wa hydroform unasidia kupunguza garama za ujenzi kwa asilimia fulani,asnte sana.

    kuhusu suaala la elimu unstahili pongezi hasa kwa mpango wa shule za sekondari za kata kwa kli watanzania wengi zaidi wanaweza kujipatia elimu.

    mdau hapo juu anasema kua UDOM haikujengwa na CCM huwenda ikawa kweli,kwasasababu CCM sio wahusikaji moja kwa moja na utendaji kama huo.ila kumbuka mafanikio yote yametokana na uongozi wa busara wa Rais JK NA ccm ndio chama kinachoiongoza serikali iliopo madarakani.

    nadhani sio vyema"BANIANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA"Tukubali tukatae CCM ina chachu ya mengi yenye mafanikio.

    nakumbuka mzee mwinyi A.H aliwahi kusema, mazuri yote ni ya kwetu sisi sote,mabaya yote nimefanya mimi peke yangu. MNYONGE MNYONGENI.................

    MDAU WASHINTON

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2012

    Mkuu hongera tunakukubali kwa kujishughulisha
    na kuweka urais chini mtazamo wa sidhani kama Tanzania atatokea tena Rais mwingine anaye weza kuwa karibu sana na jamii pia umeiweka tz katika uwazi mzuri sana hongera mzee. sd20k@yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...