Juni 26, 2007 Mhe. Amina Chifupa wa Mpakanjia alitutoka. Globu ya Jamii inaungana na wadau wote kuikumbuka siku hii adhimu ambayo kipendwa cha wengi alitangulia mbele ya haki. ULALE PEMA PEPONI AMINA CHIFUPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. "Inna Lillahi Wainna Ilayhi Rajiun"

    Kweli siku zimekwenda, miaka imekatika,
    Tutoka tusingependa, ila yote ya RABUKA,
    Tutazidi kukupenda, daima twakukumbuka,
    Mola akulaze pema, Dada AMINA CHIFUPA.

    Huko umetangulia, hilo juwa uhakika,
    Nasi sote ndio njia, katu hilo liepuka,
    Siku saa kiwadia, 'labeka' tutaitika,
    Mola akulaze pema, Dada AMINA CHIFUPA.

    Rabi yote kughufiri, kwa kila ulopituka,
    Akwepushe yake 'nari', adhabuze nusurika,
    Pema kulaze pazuri, Jannatu kupumzika,
    Mola akulaze pema, Dada AMINA CHIFUPA.

    Mola mlaze pema peponi marehem AMINA CHIFUPA - AMEN.

    ReplyDelete
  2. Rehema JettaJune 27, 2012

    Namuomba Mwenyezi Mungu ampumzishe mahali pema patulivu peponi, Yeye, Mumewe na Mama yake, pia ampe moyo wa subira na amuongoze katika njia iliyonyooka mwanae Abdulrahman, Amin.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 27, 2012

    Du miaka inakwenda. Five years already! RIP Amina and your husband.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 27, 2012

    Amina Mungu akulaze pema peponi AMEN.
    Nitamkubuka Amina siku zote, ni kwasababu yake ndio nilianza kusikiliza Radio Clouds. Amina alikuwa ni natural Talent ya presentation. She had confidence, she was funny and very articulate. Nakumbuka weekend moja nikiwa Dar nilikuwa nasikiliza kipindi chake cha watoto kwenye Clouds. Ilikuwa ni discussion kuhusu tatizo la madawati mashuleni. [Nadhani kulikuwa na uncle fulani na Mama Mdogo Amina] basi watoto na wazazi wao wanachangia nini kifanyike. Amina akasema hili tatizo la madawati sio la shule za msingi peke yake, lipo sekondari hata chuo kikuu. Akasema, aliwahi kwenda chuo akakuta wanafunzi wanajifunza wakiwa wamesimama nje ya lecture Theatre wanachungulia dirishani. Akajiuliza je hii ni level ya elimu ya juu kiasi kwamba umekuwa msomi hadi huhitaji dawati au ni shida ya madawati? Nakumbuka aliomba walioko chuo wapige simu kuchangia kwani yeye chuo alikwenda kutembea tu!! Nilicheka kweli siku hiyo, If you studied at the UDSM you know what that means. Amina alikuwa anafurahisha kwenye vipindi vingine pia. Anaaddress a serious issue in a very relaxed genuine way.
    Amina I will always remember you. . I wish all the best to Rahman your boy. By the way hivi inawezekana Clouds FM kutengeneza tapes za Amina's best programs ili wapenzi wake tujinunulie kama kumbukumbu? Ingewezekana hata pasenti fulani iwekwe benki kwa ajili ya Rahman's pocket money when he is 18? Tunaendelea kusikia sauti ya Marehemu Kanumba kwenye movie zake na Mheshimiwa je?
    Nawatakia kila la kheri ndugu na jamaa wa Kipenzi chetu Amina na walezi wa mtoto wake.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 27, 2012

    HK Nimependa unavyojibu mashairi kwa muda mfupi
    sesophy

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 27, 2012

    ina lilahi waina illahi rajiun umetutoka amina ulikuwa mpapanaji wa kweli tulio baki nao ni MAFISADI TU na mungu atakulipia kwa yeyote aliyekulia njama kwa sababu kwa mungu hakuna kubwa na haki yako daima hatopotea, rahman amkuze vema abdulrahman na ampe moyo kama wako Allah ma amin.

    miss you so much

    mdau u.s.a

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 27, 2012

    ULIPENDWA NA WENGI, LAKINI MUNGU KAKUPENDA ZAIDI. PUMZIKA KWA AMANI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...