MAREHEMU MWASHABAN A. LIGANJA
Mama Miaka mitano (5) sasa imetimia tangu ulipotutoka. Daima tunamshukuru Mungu kwa muda wote ambao ulikuwa nasi, si tu kuwa Mama mwenye upendo bali kwa kuwa ulikuwa mtu wa pekee miongoni mwetu.
Ulibarikiwa hekima, ucheshi, zaidi sana sauti iliyobeba matumaini siku zote na pia kufanya jambo kwa kusudi maalum.
Daima unakumbukwa sana na Mumeo George Mapango, wanao Mariam (Chuma), Eva (Hawa), Jackson (Kibabu), na Maria uliyependa kumuita IA, Rose, Richard na Patrick (Said). Wakwe zako Deogratius Sakawa, Ibrahim Lugandu, wajukuu zako Precious (P) na Pricilla, wadogo zako, ndugu, marafiki zako,majirani na wafanyakazi wenzako.
Ushauri wako na mema mengi uliyotufundisha tutaendelea kuyafuata. KISOMO TAREHE 10 JUNI, 2012 SAA 10.00 JIONI NYUMBANI KWAKE OCEAN ROAD (FLATS).
INNA LILAH WAINA LILAH RAJIUUN
I love you Mama. I miss you dearly.
ReplyDeleteDachu.