IIKIWA siku mmoja tu baada ya kuteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL), Kapteni Milton Lusajo Lazaro amesema shirika hilo linanafasi kubwa ya kupata mafanikio iwapo litaendelea kutekeleza mpango wake wamaendeleo wa miaka mitano.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana, Lusajo alisema atatumia uzoefu wake alioupata katika sekta ya usafiri wa anga kuleta mabadiriko katika shirika hilo na kuliwezesha kushindana sambamba na kampuni nyingine za ndani na nje ya nchi.

Kpt. Lusajo rubani anaeheshimika katika sekta ya usafiri wa anga si kwa Afrika Mashariki pekee ila Afrika kwa ujumla na anarekodi ya kuendesha ndege kwa masaa zaidi ya elfu kumi na mbili na pia amewahi kushika nyadhifa tofauti katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) pamoja na ATCL kabla ya kuteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL.

 “Napenda kutoa shukrani zangu kwa waziri Mwakyembe na viongozi wengine wa Wizara kwa kuwa na imani nami. Nimekubali uteuzi wake na nitafanya kazi alienipa kwa moyo mmoja.  Nina ahidi kuwa nitautumia uzoefu wangu wa zaidi ya miaka 35 katika sekta ya usafiri wa anga na kuipa ATCL uwezo kushindana kibiashara. Natoa wito kwa wafanyakazi wenzangu kutoa ushirikiano ilituweze kusonga mbele. ,” alisema.

Lazaro alisema kampuni yake itaendelea kutoa huduma kama kawaida na kuongeza kuwa safari zote za kampuni zitaendelea kama ilivyopangwa na ratiba licha ya mabadiliko ya uongozi.  “Hakuna sababu ya wananchi kuwa na wasi wasi. Kilichotokea ni mabadiliko ya uongozi tu lakini mipango na shughuli zote za kampuni zinaendelea kama ilivyopangwa,” alisema.

Lazaro aliongeza kuwa jukumu kubwa alionalombele yake ni kuongeza idadi ya ndege za shirika hilo aidha kwa kukodi au kuingia ubia na makampuni mengine katika jitihada za kuimarisha nafasi ya kampuni yake ili iweze kushindana kitaifa na kimataifa katika miaka michache ijayo.

 “ATCL haiwezi kupata mafanikio bila kuwa na ushirikiano mzuri na serikali pamoja na wananchi kwa ujumla. Nawaomba wananchi waendelee kuonyesha ushirikiano na uzalendo waliouonyesha katika wiki chache zilizopita baada ya kuanza kwa huduma za kampuni yetu.

“Nawahakikishia wateja wetu na wananchi kwa ujumla kuwa kampuni yangu itaendelea kutoa huduma na bidhaa bora zilizo katika bei za kiushindani ukilinganisha na makampuni mengine yanayotoa huduma hii katika soko,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2012

    Wadau wa sekta na watu wengine wanaokujua wanakusema mh captain kwamba ni mtu wa maringo na mwenye kujisikia sana.Kama ni kweli jitahidi hiyo hali usiilete mahali pa kazi kwani utaharibu sasa hivi.Otherwise ALL THE BEST

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2012

    Tupe basi angalau CV yake!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2012

    HAKUNA SABABU YA KUENDELEA KUKODI MADEGE!!!

    Kama Wananchi wanategemewa sana kuwa Wadau na Serikali kwa ujumla licha ya kukopa WB au IMF ili kupata ndege mpya ni bora kuwashirikisha Wananchi na vyanzo vya ndani vya waweekezaji ili kupata uwezo wa kununua ndege mpya badala ya kukodi:

    Mfano:

    1.Kutoa (IPO-Initial Public Offering) yaani Toleo la awali la hadharani la hisa ili Wananchi wawekeze na kuchangia ktk Shirika ili kupata ndege mpya.

    2.Licha ya kukopa Benki ya Dunia WB au Shirika la Fedha la Kimataifa IMF ambako hakuna kipaumbele kwa sisi kupata mkopo tunaweza kuwashirikisha Wadau wa ndani (Local sources of Investors) ili kuchangia uwezo wa kupata kununua ndege mpya.

    3.Pana umuhimu Serikali ikaelekeza fungu ili kupata ndege mpya na Ushirikiano na Wadau wa nje iwe ni ktk (Management and Operations)Usimamizi wa Shirika na Uendeshaji.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2012

    Huyu ameshaanza kazi vibaya, yaani dreams zake ni kukodi au kwenda kuingia ubia. Badala ya kufikiria kununua za kwetu wenyewe?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2012

    Watu wenye mitazamo hasi bwana! badala ya kupima kazi ya mtu unaanza na personality issues? Anony wa Thu Jun 07, 08:21:00 AM 2012 umenisikitisha...
    kwa mtazamo wangu Mhe. Mwakyembe amejua mtu wa kupewa kazi - kwa sababu anaweza kufanya 'kinadharia na vitendo'
    ...All the good wishes Captain - make us proud... Raise our Flag high. TANZANIA TUNAWEZA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...