Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. 
Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. 
Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.
 MAPATO
SHILINGI MILIONI
AMapato ya ndani
 
11,889,078
 i)mapato ya kodi (TRA)
10,232,539
 
 ii)Mapato yasiyo ya kodi
1,163,533
 
BMapato ya Halmashauri
493,006
 
 Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. 
Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.
Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.
Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Waziri wa Fedha na Uchumi Kivuli
19.06.2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...