Mahakama kuu ya Tanzania Kitengo cha kazi leo kimetoa onyo kwa Chama cha Madaktari Nchini (MAT) kuzingatia amri ya Mahakama hiyo iliyotolewa siku ya Ijumaa tarehe 22 Juni 2012 ya kusitisha na kutoshiriki katika mgomo na kumtaka Rais wa Chama cha Madaktari kutangaza kutii amri hiyo kupitia vyombo vya habari.
Home
Unlabelled
mahakama yatoa onyo kwa madaktari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



KWANINI HIZI HATI ZA KI SERIKARI ZINAKUWA ZINAANDIKWA KINGEREZA, KWANINI ISIWE KISWAHILI NDIO LUGHA YETU YA TAIFA. BADILISHENI BASI TUJUE KINGEREZA NDIO LUGHA YA TAIFA NA DOLA NDIO FEDHA YA TAIFA.
ReplyDeleteWakoloni wa karne zile walitumia lugha kama njia ya kujihami ili wajikweze,ili kuwe na tabaka la wanaojuwa na wasiojuwa. Tanzania lugha yetu ya Tifa ni Kiswahili, alafu ni lugha nzuri kuliko kiingereza.
ReplyDeleteMdau wa kwanza, Tanzania ina lugha mbili za kiofisi, Kiswahili na Kiingereza (hakuna sehemu inayobainisha lugha moja kuwa mbele ya nyingine katika taratibu za kiofisi bali zote ziko sawa). Hivyo ukiona lugha mojawapo inatumika muandishi anakuwa hajafanya kosa lolote kabisa. Ni kwamba asiyeelewa atafute mkalimani ama mtoa taarifa, endapo atapenda, atoe taarifa kwa lugha zote mbili. Ila mahakama iko sahihi, na walengwa wanaifahamu hii lugha iliyotumika.
ReplyDeleteLugha iliyotumika ni ya kiubabe saana,hakuna majadiliano hapo. Inanikumbusha "Kibanga ampiga mkoloni".Wakoloni walitumia lugha kama hii kutukandamiza.
ReplyDeleteDr Gangwe Bitozi
Mdau wa Tatu uko sahihi kabisa sina ubishi na hoja yako, Lakini mimi natamani tuzungumzie swaala lenyewe, huu ndo utaratibu, kwamba mtu unapodai haki utishiwe ili usiidai haki hiyo? mimi siyo Dactari na wala katika familia yetu hayupo Daktari labda baadae,Hata hivyo ninauchungu sana na namna watu hawa(viongozi wa nchi) wanavyoshindwa "ku-handle" mgogoro huu, ambao mimi kwangu kama ningekuwa Rais nauona kuwa ni rahisi sana kuutatua, kwasababu mamlaka yote ni yangu na naweza kuamua vyovyote vile "kuwa-favor" Madactari hawa na nikakubalika, hakuna ambaye angenipinga, kwanza nchi hiyo sasa hivi watu wanalipa sana kodi, kwahiyo nisingetegemea serikali yangu ishindwe kutatua tatizo dogo kama hili, I know the Government is scared to open the flood gate for some reasons,may be they say, ok if we do this to Doctors, then Teachers will come up too, and other as well, NO! you can open the Flood gate in style in such a way that, nobody alse will follow the route.
ReplyDeleteHaya ndiyo maoni yangu.
Lugha iliyotumika ni ya kisheria na kuna utaratibu wa namna ya kutoa order. Tatizo langu ni moja kwamba experte interim injunction order ilitolewa ijumaa jioni (hata judge kaandika "late yesterday")hiyo ina maana upande wa madaktari haukusikilizwa na wakapewa amri kutekeleza haraka, ikizingatiwa kwamba kesho yake week end inaanza tutegemee nini kwa amri kama hii? Bila shaka madaktari watakwenda kazini ila kwa mgomo baridi na hapo serikali itajiona kama imeshinda ila kwa utendaji imeshindwa. Kazi hii ni tofauti na kazi nyingine, hawa wanaamua hatima ya maisha ya watu tukiwalazimisha kama serikali ilivyofanya kupitia mahakama, matokeo tutayaona. Serikali imeshindwa kuwa na busara.
ReplyDeleteMadaktari wanatibu watu,hawaandiki wakaratasi kama wengine, kuna kazi huwezi kumlazimisha mtu kuifanya eti kwa hamri. unamshikia mtu bunduki unasema mtubu huyu, unategemea matokeo yaweje. Wahusika tumia njia za kidemkrasia malizeni haya kasomi. Watanzania wanakufa kwa ajali, njaa basi hata jambo ambalo linawezekana. ONENI HURUMA
ReplyDeleteLugha ya kisheria iliyorithiwa toka kwa mkoloni, let us emancipate ourselves from mental slavery......
ReplyDeleteDr Gangwe Bitozi.