| KATIBU MKUU WA RT, SULEIMAN NYAMBUI NA TABASAMU LA USHINDI |
Pongezi kwa washindi meza kuu
Kanali Mstaafu Juma Ikangaa ( wa kwanza kulia) akifuatilia matangazo ya matokeao ya uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania ( RT) uliofanyika Mei 20, mwaka huu mjini Morogoro, Ikangaa aligombea nafasi ya Rais wa RT na kushindwa dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Antony Mtaka .
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akiongea na mmoja wa viongozi wa RT na kulia ni Rais wa RT , DC Mtaka ilikuwa kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika
Rais mpya wa Shirikishio la Riadha Tanzania ( RT), Antony Mtaka ambaye ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro ( aliyeshika ua)akipongezwa na baadhi ya wajumbe waliochaguliwa wa Shirikisho hilo juzi ( Mei 20) wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Mjini Morogoro ( aliyekaa kulia) ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa ( BMT) Dioniz Malinzi.
Rais mpya wa Shirikishio la Riadha Tanzania ( RT), Antony Mtaka ambaye ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro ( aliyesimama ) akitoa hotuba yake ya shukrani kwa wajumbe wa Shirikishi hilo, Viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi ( wapili kutoka kushoto) kwa kumchangua kwa kura za kishindo pamoja na safu yake ya uongozi mpya baada ya kushinda mpinzani wake Kanali Mstaafu Juma Ikangaa , uchaguzi huo ulifanyika juzi Mjini Morogoro. Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii


Ikangaa kashindwa kupata Urais wa RT! Ikangaa pamoja na experience yote kama mwanariadha, uongozi wa michezo jeshini na hata BMT kashindwa!? Kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!
ReplyDeleteMkuu wa Mkoa wa Morogoro alikuwa Naibu Waziri wa Michezo. Naibu Waziri wa Michezo ni Mbunge wa Mvomero. Aliyechaguliwa kuwa Rais RT ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero! What a coincidence!?
ReplyDeleteNilipata kukutana na kundi la Tanzania kwenye Mashindano ya Riadha ya Dunia likiongozwa na mtu binafsi "mfanyabiashara" . Hilo kundi halikuwa na kiongozi yoyote toka RT wala wizarani wala serikalini. Kwa bahati, mmoja wa wanariadha wa Tanzania alishinda medali kwenye mashindano ya marathon! Lakini hapakuwepo hata mtu wa kumpa bendera ya kukimbia nayo uwanjani baada ya kushinda. Sijui kama alipata cheque yake ya ushindi kwa sababu alikuwa hata hajui kama atalipwa na yule kiongozi wa msafara alikuwa kaivalia njuga ile cheque na mshindi wetu walikuwa wamemlewesha chapa chapa wakati wa kwenda kuchukua cheque!
Katika mashindano hayo hayo kundi la Kenya liliambatana na mawaziri wawili, makocha, madaktari, wasaidizi wa wanariadha, PR Personnel na maafisa kadhaa wa utalii.
Katibu Mkuu. Sasa ndiyo ngoma imefika kwa kenge. Pumu imepata mkohozi. Lawama Ltd.
ReplyDeleteNASASAMBUA KILA KITU:
ReplyDeleteMjaribu kujiuliza na kufuatilia kwa nini huyo Juma Ikangaa pamoja na Umahiri wake na Uzoefu hakupata?
JIBU NI KUWA JUMA IKANGAA na kundi lake walikuwa wanaitumia Tasnia ya Riadha kwa maslahi binafrsi!
Na ndio hao wameihujumu Riadha Tanzania kufikia hapa tulipo na aibu ulizotoa Mdau wa Pili hapo juu.
Pana mtoto mmoja ni Mwanariadha mzuri sana anafanya kazi ya kuosha magari (Car wash) pale Tancot House ,Luther House nyuma ya Swiss Air dogo alitakiwa atoe Tshs. 500,000/= (Laki tano) kama 'rushwa' na kundi la akina Juma Ikangaa ili awekwe kwenye timu ya kwenda kwenye mashindano nje.
HAPA NDIO MTATHIBITISHA NI KWA NINI JUMA IKANGAA HAFAI !
TUSILAUMU MATOKEO YA KURA KTK RT !
Je wandugu Mwosha magari anaweza kuwa na Rushwa ya Tshs. LAKI TANO?