Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,Mh. Jerry Slaa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mchakato wa uanzishwaji wa huduma za matibabu kwa wananchi kupitia mpango mpya wa Tiba kwa Kadi (TIKA) kwa madiwani wa Manispaa hiyo yanayotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambao ni msimamizi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inayoendelea hivi sasa kwenye ukumbi wa Arnautoglo,Ilala jijini Dar es Salaam.Kushoto Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Khamis Mdee na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Ellioth Mwasambite.
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Khamis Mdee akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya mchakato wa uanzishwaji wa huduma za matibabu kwa wananchi kupitia mpango mpya wa Tiba kwa Kadi (TIKA) kwa madiwani wa Manispaa ya Ilala,Jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Ellioth Mwasambite akiwatambulisha baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Ilala waliofika kwenye Mafunzo hayo leo.
Baadhi ya Madiwani wa Ilala waliofika kwenye Mafunzo hayo leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...