Na Mohammed Mhina na Pardon Mbwate, wa Jeshi la Polisi

Mwanafunzi mmoja wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kigadye wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Abeid Manase(8), amefariki dunia hapo hapo na wengine wanne kujeruhiwa vibaya baada ya kulipukiwa na bomu la kutupwa kwa mkono walilokuwa wakilichezea.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ACP Fraisser Kashai, amewataja watoto waliojeruhiwa na bomu hilo kuwa ni wanafunzi wawili wa darasa la kwanza Tuju Seluke(7) aliyejeruhiwa tumboni na Sarah Manase(6) aliyejeruhiwa kwenye paja na mguu kulia. wote wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Kigadye wilayani Kasulu.

Kamanda huyo amewata wengine waliojeruhiwa kuwa ni watoto wadogo wenye umri wa miaka minne kila mmoja ambao walikuwa wakichezea bomu hilo kwa pamoja ambao ni Enjord Seluke aliyejeruhiwa kwenye sikio la upande wa kushoto na Isaka Yohana aliyejeruhiwa kwenye jicho la upande wa kushoto.

Kamanda Kashai amesema majeruhi hao wote wamelazwa katika hospitali ya Misheni iliyopo katika kijiji cha Shunge wilauani Kasulu kwa matibabu zaidi na hali zao zimeelezwa kuwa zinaendelea vizuri.

Kamanda Kashai amesema jana majira ya saa 11.00 jioni, huko katika kijiji cha Kigadye, watoto hao walikuwa wakilichezea bomu hilo la kutupa kwa mkono na ndipo lilipowalipukia na kumuua mwenzao na wengine hao wane wakajeruhiwa.

Bomu hilo lilikuwa limefichwa katika moja ya bustani nyumbani kwa Bw. Ayoub James Luvahovi mkazi wa kijiji cha Kidae na likimbia mara baada ya tukio hilo na Polisi wanamsaka.

Katika tukio linguine Kamanda Kashai amesema huko Kasulu, watu wenye silaha wamemjeruhi kwa kumpiga risasi tumboni mfanyabiashara mmoja Bi. Deothera Malusha(23) na baadaye kumpora shilingi 150,000 pamoja na simu yake ya mkononi aina ya Nokia yenye thamani ya shilingi 55,000.

Amesema baada ya uporaji huwo, majambazi hayo yalikimbia na kutokomea katika msituni na majeruhi amelazwa kwenye Hospitali ya wilaya ya kasulu mkoni Kigoma na hali yake bado sio nzuri.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia watuhamiaji haramu 52 kwa makosa ya kuingia na kuishi nchini bila ya kibali.

Kamanda Kashai amesema kuwa wayuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo mbalimbali walipokuwa wakifanya shughuli za uvuvi mkoani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2012

    Hii imekaaje hadi watoto wanachezea bomu kama toys? inaonekana hayo ni maeneo hatari kabisa kwa maisha ya watu, na je mtu wa kawaida kama Bw. Luvahovi ambae ni mtuhumiwa namba moja ametoa wapi silaha kama hii? ah! kazi sana nchi hii!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2012

    Inasikitisha sana kuona watoto wadogo wanaachwa katika mazingira ya hatari bila ya uangalizi wowote, poleni sana kwa msiba na ajali

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2012

    hiyo ndio kigoma, mwisho wa reli. Serikali inatiakiwa iangalie jinsi ya kusafisha mkoa huu, mchanganyiko na wahamiaji haramu umezidi, ni kama wenye wajibu huo wamesahau kazi yao, na zile kambi za wakimbizi bado zipo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...