Mhe. Naibu Spika, Job Ndugai,Mb akizungumza na Watanzania waishio Korea Kusini katika Chuo Kikuu cha Dongkukk wakati alipoalikwa kutoa mada MCHANGO NA NAFASI YA WATANZANIA WAISHIO NJE YA NCHI KATIKA BUNGE. Kushoto katika meza kuu ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Korea Kusini, Nd. Emmanuel Lupilya na kushoto ni Katibu wa Jumuiya hiyo Nd. Msofu.
Baadhi ya watanzani waishio Korea Kusini wakimsikiliza Mhe. Naibu Spika Ndugai,Mb alipokutana nao katika Chuo Kikuu cha Dongkukk jijini Seoul. Watanzania hao walimuomba Mhe. Naibu Spika kuwasilisha maombi yao kwa Serikali juu ya umuhimu wa kufungua Ubalozi nchini Korea Kusini kama zilivyofanya hivi karibuni nchi za Ethiopia na Kenya na hivyo kunufaika kwa kiasi kikubwa na fursa mbali mbali zinazotokana na mahusiano ya kidiplomasia ya karibu baina ya nchi hizo mbili.
Picha ya pamoja ya Watanzania waishio nchini Korea Kusini na Naibu Spika, Mhe. Job Ndugai,Mb ambae aliambatana na Balozi Johan aliewahi kuwa Balozi wa Korea nchini Tanzania 2001-2004, ambae pia husaidia shughuli za visa na huduma nyinginezo kwa Wakorea wanaohitaji kwenda Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2012

    Duh, jamani mpaka Korea kumbe watanzania tumechanja mbuga kote duniani ??? hii ni faida kuubwa sana kwa Taifa letu, hawa watu wapewe duo citizen,hawa ni rasilimali ya Taifa letu,maana waliyojifunza huko na kwingineko kote, watatuletea sisi huku nyumbani na tutajifunza uchapaji kazi kutoka kwao-kule kote dunia zingine hakuna UFISADI kuna kubeba mabox tu na kula kwa jasho la halali, siyo huku bongo ,mtu anamaliza chuo kikuu anapata kazi TRA au Tannesco baada ya miezi 6 ananunua gari ( Prado) na tayari kiwanja Sinza na anajenga, Kikwete atafukuza wangapi ??? siyo Mkulo peke yake ,sisi sote tumeoza. ni mimi msema kweli Zebedayo wa Badugu Nasa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2012

    Timu hii imejaa wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali. Kweli ni muhimu kwa Tanzania kutumia resource hizi katika maendeleo ya nchi kama mdau hapo juu alivyosema. Korea imeendelea sana na hata kozi wanazofundisha watanzania na mataifa mengine zinalenga kuzibadili nchi zinazoendelea.
    Tujifunze na kutumia exposure zetu vizuri kwa maendeleo ya Taifa letu lililojaa ufisadi na udhalimu.
    Mungu Ibariki Tanzania.
    Mdau
    Iringa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...