Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Group ya Saudi Arabia, Dkt. Sulaiman Al Fahim wakati walipokutana leo, Jumamosi, Juni 2, 2012, Ikulu Dar es Salaam. Dkt. Al Fahim ambaye ni mwenyekiti wa zamani na mmilikimwenza wa Klabu ya soka ya Portsmouth ya Uingereza yuko nchini kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika uchumi wa Tanzania. Dkt. Al Fahim pia ndiye aliyeongoza mazungumzo na kununuliwa kwa klabu bingwa ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Manchester City na Kampuni ya Arabuni. (Picha na fredy Maro).
Home
Unlabelled
Rais Kikwete akutana na Mmiliki wa klabu ya Portsmouth Dkt. Sulaiman Al Fahim Ikulu jijini Dar es Salaam leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuweni makini na watu wanaokuja na majoho toka arabuni kwa madai ya uwekezaji,ni aibu mtu anapokuja na kupata kukutana na raisi ndani ya ikulu.Huyu jamaa japo ndio alihusika katika mazungumzo ya kununua man.city na ndio gia aliyoitumia kununua portsmouth lakini hana kitu kwani timu imefilisika na inashindwa hata kulipa mishahara na imenyang'anywa pointi kumi ikasababisha kushuka daraja la tatu.kama angekua na pesa si angeokoa timu yake? Ameshindwa hata kuwalipa mishahara wachezaji Tal Ben Haim na Kanu. Waandishi wetu wa bongo jaribuni kufanya research kidogo ili mtoe habari ya pande nyingi sio kuchukua tu story na kui publish kama mlivopewa na watu wa PR
ReplyDeleteKJ...mwambie huyo amwambie kocha wake aje aangalie vipaji vya soka Tanzania.
ReplyDeleteDavid V
anon wa kwanza:
ReplyDeletekwa hiyo akija na suti ni poa hata kama alifilisika.
anon wa kwanza:
ReplyDeletekuwa muwazi kuwa hutaki mwarabu au isilamu, mdini mkubwa we.
sasa avae nini wewe mshamba hapo juu AVAE SUTI au awe MZUNGU? ndio wa maana??? mijitu mingine ZEROOOO
ReplyDeleteHuyo jamaa hapo juu ni mshamba sana, na anaabudu wazungu wakati wazungu wanamuona nyani tu, pole sana kaka kwa ujinga wako mkubwa....
ReplyDeleteUsije kusema kuwa hujui wamiliki wakiingia nchini.
ReplyDelete