Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh.Dkt. Fenella Mukangara (pichani) amepata ajali mbaya mchana huu maeneo ya Nzega Mkoani Tabora wakati akiwa njiani kuelekea Jijini Mwanza kwenye Ufungunguzi wa Mashindano ya Taifa ya Mchezo Vishale (Darts) yanazinduliwa leo Jijini humo.
Globu ya Jamii imefanya mawasiliano na Mh. Mukangara na kuthibitisha kupata ajali hiyo ambapo anasema chanzo chake ni kuchomekewa na basi moja la abiria (ambalo hakulitaja jina lake).
"Ni kweli tumepata ajali hapa maeneo ya Nzega Mkoani Tabora wakati tukiwa njiani kuelekea jijini Mwanza ambako leo kunafanyika ufunguzi wa Mashindano ya Taifa ya Mchezo wa Darts,tunashukuru Mungu wote tumetoka salama japo tumepata majeraka katika sehemu mbali mbali za mwili."Alisema Mh. Mukangara.
Tunaendelea kuwasiliana na Mh. Mukangara na tutaendelea kupeana taarifa zaidi.


Pole mheshimiwa na wote waliohusika kwenye ajali hii.Haya sasa tuone serikali itafanyanini juu ya swala la madereva wanaoendesha magari kwa kutofuata taratibu za udereva.kwaniwananchi tumepiga sana kelele na kupoteza ndugu zetu juu ya uzembe wa madereva. WAKATI UMEFIKA WA KUBADILIKA NA SERIKALI KUFUATILIA UZEMBE WA MADEREVA.
ReplyDeleteatatibiwa na nani wakati madaktari wamegoma?.au ataenda india na nchi nyingne wanakothaminiwa wataalamu badala ya kuabudu siasa kama hapa kwetu?, au ana daktari wake anayemlipa vizuri!
ReplyDeletePole sana. Tatizo madereva wengi Bongo hawafuati sheria za barabarani au hawazijui kabisa! Bongo road law.
ReplyDelete