Nyumba ambayo imepatwa na janga la kuwaka moto usiku wa kuamkia leo ikiendelea kuteketea kwa moto huo katika maeneo ya kashai,Wilayani Bukoba Mkoani Kagera,Chanzo cha moto huo inasemekana ni mshumaa uliokua ukiwaka katika moja vyumba vililivyo ndani ya nyumba hiyo na kusababisa kuwaka kwa moto huo.hakuna mtu aliepoteza maisha katika ajali hiyo.
Kikosi cha Zima moto Mkoani Mara kikiendelea na jukumu lake la kuuzima moto huo.
Sehemu ya Mabaki ya mali za watu waliokuwa wakiinshi kwenye nyumba hiyo.
Baadhi ya wakazi wa Kata hiyo ya Kashai wakiwa katika eneo la tukuo kushuhudia.
mmoja kati ya wapangaji kwenye nyumba hio akiongea na Mdau wa Globu ya Jamii alietuletea taarifa hii wakati akisema chanzo cha moto huo na kuthibitisha kuwa ni Mshumaa uliokuwa unawaka.
Hii ni mara ya kwanza nasikia mshumaa ndio chanzo cha kuteketea nyumba. Mara nyingi utasikia ni hitilafu ya umeme, hata kama nyumba iliyoungua haikuwa na umeme. Hii 'hitilafu ya umeme' hutumika kuficha uzembe unaosababisha moto.
ReplyDeleteHuu ndiyo moyo/spirit watanzania tuliokuwa nao wa kupiga kazi tuliyoichagua kufanya. Hongora sana kikosi cha zima moto Bukoba. Viongozi wetu wangekuwa na moyo huu nchi yetu ingekuwa mahali bora pa kuishi kuliko sehemu nyingine yeyote duniani. Endelezeni moyo huu watoto wetu wafuate.
ReplyDeleteKazi kwlei kweli moto Kagera unazimwa na kikosi cha zima moto kutoka Mara. Ama kweli wahaya bila watani zao wakurya ni apache alolo!
ReplyDeleteHONGERA KIKOSI CHA ZIMAMOTO, JUHUDI ZENU TUMEZIONA JAPOKUWA MMEKUTA MAJIVU HIVYO HAMKUFANYA AJIZI MKAYAZIMA.
ReplyDeleteKuna mwaka moto uliwaka Tanga na fire ilitoka Dar
ReplyDeleteni kawaida, imagine wilaya ambazo hazina zima moto na makao makuu ya mkoa yako mbali na wilaya hizo, lazima sehemu yoyote zima moto ilipo karibu isaidie. cha muhimu isije ikatoka zimamoto mkoa mmoja hadi mwingine na ukakuta ina hitilafu, du!
ReplyDelete