Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza kusitisha Serikali kutoa tamko lake kuhusu mgomo wa madaktari, ambao ulitakiwa kutolewa leo kama alivyoahidi jana Bungeni.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Waziri Mkuu, Pinda, alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua Serikali ina mipango gani ya dharula ya kuumaliza mgomo huo.
Alisema kwa hivi sasa, Serikali imechukua dharura, kwa kuwaita madaktari wastaafu kwenda kwenye baadhi ya Hospitali za Serikali kushika nafasi maeneo ambayo madaktari waliogoma.
Vilevile Serikali imewataka wananchi waende kuhudumiwa kwenye hospitali za Jeshi, ikiwemo Lugalo.
Kuhusu Dkt Stephen Ulimboka, Mhe. Pinda ameseama kuwa hata yeye alipopokea taarifa kuwa Dkt. Ulimboka ametekwa na kupigwa na kwamba alisikitika sana, na anamuombea apone haraka ili waendelee na suluhisho la mgomo huo wa madakatari.
Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya ndani kuunda jopo la wataalamu kuchunguza kwa haraka kuhusu tukio hilo.
Tulitangaziwa "Liwalo na liwe" sasa kusikitika kunatoka wapi?
ReplyDeleteMungu hakutaka Dr.Ulimboka afe, na atapona kwa uwezo wake.
ReplyDeleteDUA: "Mungu nakuomba kila aliyeshiriki hata kwa kiasi kidogo kama sisimizi kufanikisha unyama aliofanyiwa dokta ulimboka umdhalilishe hapa duniani hadi siku ya mwisho"Amina
Mmh mi cna upande, ukiangalia huo unyama unasikitisha ila kwa upande mwingine hivi Hawa wasio na kipato na wanategemea gvt hospital wafanyaje? Manake bora ya wngn tuna health insurance. Jamani madoctor kuweni na japo na huruma kidogo, watu wanaisha na taifa litabaki na nani? Naomba pia kuuliza mbona mi nakumbuka 90% yenu mmesomeshwa na fedha walizokua wanakatwa wazazi wetu? Just be fair, mbona walimu wanalipwa hela ndogo na ndio wanawafundisha kusoma na kuandika.tutafute njia mbadala na sio kuua wasio na hatia. Plz we have to be decent, so that we don't kill innocent people.
ReplyDeleteMIMI NI MWALIMU LAKINI NAKUBALI KUWA KAZI YA UDAKTARI YATAKA MOYO KWAHYO HATA KAMA NALIPWA KIDOGO SAWA HAITOSHI LAKINI SIWEZI HATA SIKU MOJA KUWA SAWA NA MTU ANAYEPASUA MATUMBO ANAYEOSHA VIDONDA VIMESHANUKA, ANAYESHONA MWILI ULIOPASUKA, KAZI YAKE NI YA HATARI KWANI ANAWEZA AMBUKIZWA MAGONJWA KWA KUSHIKA DAMU NK. WATANZANIA TUSIWE TUNAPINGA KILA KITU AMBACHO KIKO WAZI JAMANI UKWELI KAZI YA UDAKTARI NI NGUMU SANA HATA WALIPWE MILIONI TATU SAWA KWANI HAO WANAOIBA MAMILIONI SI WANATUUA IMPLIEDLY? TATIZO TUMEFINYWA UWEZO WA KUFIKIRI KWAHYO UKIPINDISHWA KIDOGO UNAAMINI KUWA MADAKTARI WANASABABISHA VIFO MAKUSUDI SI KWELII JAMANI WANATAKA HATA NASI TUWE NA HUDUMA NZURI MIMI NILIENDA KUJIFUNGUA NIKAAMBIWA KUSHEA KITANDA IMAGINE KITANDA KIDUCHUU UNA MTOTO NA MWENZIO ANA MTOTO SASA HAPO AFYA IKO WAPI? TUAMKE TUWEKE MAMBO YA SIASA PEMBENI TUANGALIE HALI HALISI
ReplyDelete