ANKAL,
MAMBO VIPI, KUNA MTU ANAITWA MWAMGONGO alitunga shairi katika Globu ya jamii juzi juu ya Sensa na kuwekerwa na Kipengele cha dini na Serikali kugoma. Nami nimetoa Jibu.
SHAIRI: ENYI WATU WA TAKWIMU! (JIBU)
Salamu nyote wadau, wa habari za bloguni
Rubani na wapiga dau, hata mlio maskani,
Sensa haita wasahau, namlio gerezani,
Kutambua wenye dini, si kazi ya serikali.
Si kazi ya serikali, kutambua wenye dini,
Msaada wa serikali, hauendi kwa wenyedini,
Huwafikia wa suruali, na wavaao magauni,
Kutambua wenye dini, si kazi ya serikali.
Katika nyumba za ibada, humo wanajuana,
Wakwetu anaitwa Sada, wenzetu wanae Anna,
Daima hakuna shida, na bado tuna zaana,
Kutambua wenye dini, si kazi ya serikali.
Hakika limekupa shida, Mwagongo kutoka Tanga,
Tujione ni wakawaida, dini wasipo ipanga,
Wala tusiwape shida, wakianza kujipanga,
Kutambua wenye dini, si kazi ya serikali.
Serikali haina dini, hakuna asofahamu,
Haishabikii udini, bali amani idumu,
Tuishi kama zamani, wala tusishutumu,
Kutambua wenye dini, si kazi ya serikali.
Mbona tupo wapagani, tunaishi masikani,
Tumejaa majumbani , hatupajui makanisani,
Hata huko msikitini, napo pako shakani,
Kutambua wenye dini, si kazi ya serikali.
Umeongelea hesabu, za watu pia makazi,
Dini isiwe ni sababu, tukageuka wakambizi!
Watu wawe mabubu,kisa dini hakuwekwa wazi?
Kutambua wenye dini, si kazi ya serikali.
Watu tunahamasisha, kuhesabiwa majumbani,
Dini zinawakumbusha, kutokimbilia mashambani,,
Lipi lina chekesha, tusipende ‘uhayawani’,
Kutambua wenye dini, si kazi ya serikali.
‘Una iga za dipatimenti’, ya watu wa Marekani,
Kuanda tovuti, dini zote kuweka ndani,
Ushoga hamuutaki, sisi unataka Umarekani?
Kutambua wenye dini, si kazi ya serikali.
Dini haina tofauti, kwa mzungu na msukuma,
Haina mvaa suti, wala Mchaga asie soma,
Ni haki kupiga shuti, katika Takwimu daima,
Kutambua wenye dini, si kazi ya serikali.
Mapadri makanisani, hata nanyi maasikofu,
Hamasisheni waumini, wahesabiwe bila hofu,
Wabakie majumbani, watoto hata vipofu,
Kutambua wenye dini, si kazi ya serikali.
Kalamu naweka chini, sore nilipokosea
Jalalu ibariki nchi, Amani sije potea,
Zoezi bado bichi, Sensa wasije kosea.
Kutambua wenye dini, si kazi ya serikali.
Mroki Mroki ‘Father Kidevu’
www.mrokim.blogspot.com
Kinyenze, Morogoro
hongera shairi nzuri sana, waambie hao kujua dini siyo kazi ya serikali. Big up!!!!!!!!!!!
ReplyDeletesafi sana ,kila dini ihesabu watu wake na kuwatambua, ukianza kuandika maswala ya dini mwishowe mtasema na koo ziandikwe. Wapagani tutakwenda wapi?
ReplyDeleteHongera kwa tenzi yako ilojaa maoni yako."Kutambua wenye dini si kazi ya serikali".
ReplyDeleteKama ni hivyo, serikali katika fomu zao kipengele cha udini kiondoshwe kwakuwa sio kazi yake kutambua dini ya mtu.
Naifike wakati kipengele cha ukabila nacho kiondolewe kwani kinaleta ubaguzi fulani.
Hana maana kwamba nabdi kuga kla walcho nacho wamarekani ila yale mazuri s ushoga.
ReplyDeleteKama hawataki kuweka kpengele cha Dini basi kina TBC waache kutoa takwimu.
Kipengele cha dini lazima kiwepo, kama takwimu zipo na ni za uongo ni lazima zirekebishwe, na kazi ya kuhesabu watu ni ya serikali si ya viongozi wa dini. Lakini kwa vile vyombo vya serikali vinatoa takwimu ambazo kwanza si sahihi, pili bila yakutuambia zimetoka wapi inabidi sasa utaratibu utolewe ilikipengele cha dini kiwepo ilitupate takwimu sahihi.
ReplyDeleteNa kama si muhimu kwa nini zinaogwapwa? Kama waislam wanataka kuhesabiwa kwa nini inakataliwa. Basi nakama si muhimu hatuta hesabiwa, mkae na hesabu zenu mnazozitaka.............kwani kutaharibika nini?