Mkuu wa Wilaya ya Hai,Mhe Novatus Makunga akitoa matone ya vitamin A na dawa ya minyoo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mtoto barani Afrika yaliyoadhimishwa mwishoni mwa wiki.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika mkoani Kilimanjaro mhe Novatus Makunga ambaye ni mkuu wa wilaya ya Hai aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Kilimanjaro akipokea maandamano ya watoto wakiingia katika viwanja vya maadhimisho hayo yaliyofanyika wilayani Siha.
Bendi maalumu ya watoto walemavu wa shule ya msingi ya faraja iliyoko wilayani Siha ikitoa burudani na baadaye kupiga wimbo wa taifa.
Wanafunzi wakiingia kwa maandamano katika maadhimisho hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...