MWANAFUNZI wa Chuo Kukuu cha North Texas cha Marekani, Sitti Mtemvu (kushoto), akitoa msaada wa sh. 500,000 kwa msichana Happines Kaaya (22), aliyezaliwa akiwa mlemavu,leo huko Machimbo, Temeke, jijini Dar es Salaam. Mama yake Sitti, Mariam Mtemvu, ambaye ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akimpa pole Happiness.
Mmoja wa wapangaji wa nyumba anayoishi Happiness na mamake Khadija Msuya akielezea jinsi wanavyomsaidia msichana huyo mlemavu Sitti akitoa msaada mwingine wa sh. 200,000 kwa mtu mwenye ulemavu, Nassoro Tayari mkazi wa Buza jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kununulia vipuri vya kutengenezea baiskeli yake.
MWANAFUNZI wa Chuo Kukuu cha North Texas, Marekani, Sitti Mtemvu, ametoa msaada wa sh. 500,000 kwa msichana Happines Kaaya (22), aliyezaliwa akiwa mlemavu.
Msaada huo alikabidhi kwa mama mzazi wa Happiness, Khadija Msuya wakati alipotembelea kwenye chumba wanachoishi eneo la Machimbo, Temeke, Dar es Salaam.
Siti ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mtemvu Foundation, alisema kuwa ameamua kutoa msaada huo baada ya kuguswa na taarifa za msichana huyo alizozisoma kwenye mafaili ya mfuko huo, uliopo Temeke, Dar es Salaam.
"Taarifa za msichana huyu, zilinigusa mno kuliko wengine, kiasi cha kuamua kuanza kutoa msaada kwa Happiness aliyezaliwa akiwa mlemavu na analelewa mamake kwa shida,"alisema Siti.
Siti ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu, alisema kuwa fedha alizizitoa ni sehemu ya mapato yanayotokana na bajaji zake tatu zinazofanya biashara ya kubeba abiria jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa Bajaji hizo alizinunua kutoka na na fedha alizolipwa baada ya kushiriki kwenye filamu moja nchini Marekani anakosoma.
"Sitoishia kutoa msaada kwa msichana huyo, bali nina imani Mungu akinijalia nitaendelea kutoa msaada kwa yatima na watu wengine wanaoishi kwenye mazingira magumu"alisema Siti.
Mama mzazi wa Happiness, Khadija, alishukuru kupata msaada huo kutoka kwa Sitti, ambao alidai utamsaidia sana kupunguza baadhi ya matatizo yanayomkabili.
Alisema kuwa mtoto huyo ambaye alimzaa akiwa na ulemavu, hana uwezo wa kutembea ambapo hata kula chakula ni vigumu inabidi alishwe na kumsaidia wakati wa kujisaidia.
Alidai kuwa Baba mzazi wa Happiness, Joel Kaaya alimtelekeza yeye na mwanawe ambapo mpaka sasa haijulikani aliko.
Msuya alitoa wito kwa watanzania wengine kujitokeza kusaidia hata ikiwezekana kumnunulia happiness kiti cha magurudumu kitakachorahisisha kumpeleka Hospitali na hata kutoka nje kucheza na wasichana wenzie.

Na Richard Mwaikenda

Pia siku hiyo, Siti alitoa msaada mwingine wa sh. 200,000 kwa mtu mwenye ulemavu,Nassoro Tayari mkazi wa Buza jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kununu vipuri vya kutengenezea baiskeli yake
Be blessed.
ReplyDeleteNapenda watu wanapotoa misaada hasa kwa makundi ya watu wasojiweza ILA hii biashara ya kutangaza kuwa umesaidia kwa kweli si njema sana. Anyway hao ni tabaka la siasa labda ni njia ya kujitangaza hiyo
ReplyDeleteKWANZA NAPENDA KUTOA PONGEZI ZANGU KWA BI SITTI MTEMVU KWA MOYO WAKE WA DHATI WA KUTOA MISAADA KAMA HII INAYOHITAJIKA SANA KATIKA JAMII YETU.
ReplyDeletePIA NINGEPENDA KUTOA UFAMAMISHO MDOGO KUHUSU KUTOA MISAADA KWANI KUNA MSTARI MWEMBAMBA SANA KATI YA KUTOA KWA MOYO MKUNJUFU NA KUTOA ILI KUWEKA SURA KWENYE KIOO,NIMEONGELEA KUHUSU MSTARI MWEMBAMBA SANA KWA SABABU BILA KUTUJULISHA KATIKA VYOMBO VYA HABARI TUTAJUAJE WAPI MSAADA UNAHITAJIKA?
PIA KUWASAIDIA WALEMAVU WA AINA YOYOTE ILE NA KUWAWEKA KATIKA MAGAZETI WAKIPOKEA MISAADA MIMI BINAFSI HUFURAHIA KUWA WAMESIKILIZWA VILIO VYAO NA MTOA MSAADA LAKINI PIA HUWA NA PATWA NA HISIA ZA KUONA KAMA KUNA UDHALILISHWAJI FULANI KWANI HUJIULIZA KAMA MPOKEA MSAADA AKIKATAA KUPIGWA PUCHA HUKU ANAPOKEA PESA MTOAJI ATATOA AU ATAGOMA?
DINI MOJA KUBWA INASEMA UKITOA KWA MKONO WA KULIA BASI HAKIKISHA MKONO WA KUSHOTO HAUJUI KINACHOENDELEA.
MARA NYINGI NIKIWA JIJINI DARES SALAAM KWA MAPUMZIKO HASA MTAA WA SAMORA ZAMANI INDEPENCE AVENUE HUTOA MSAADA KWA WALE WANAOHITAJI KANDO KANDO MWA BARA BARA LAKINI HUJITAHIDI KUANGALIA HAMNA WATU WENGI WANAONIANGALIA HALAFU HUZUKA GHAFLA NA KUMUWEKEA YULE NILIYEMLENGA KUMPATIA HELA KATIKA CHOMBO ALICHOKAMATA NA KUYEYUKA HATA NAFASI YA KUPOA ASANTE HUWA HAIPO NIKIFIKA MBELE KIDOGO HUGEUKA NYUMA NA KUWA NA "EYE CONTACT" NA NILIYEMPATIA PESA HUKU NILI"SMILE" NA MUHUSIKA HUONYESHA ISHARA YA KUSHUKURU NA KU "SMILE BACK" HASA KWA KUWA KIWANGO NILICHOWEKA KWA SIKU ILE ANAWEZA KUFUNGA DUKA,HUYEYUKA KAMA NILIVYOZUKA.
NAFIKIRI KUTOA NI MOYO SIO UTAJIRI KAMA TUNAVYOJUA NA NAWASHUKURU WOTE WANAOISAIDIA JAMII YETU HASA SISI TULIOKO NJE ISIPOKUWA NINGEOMBA TUWATAKE RIDHAA ZAO HAWA WAHUSIKA KWANZA KABLA HATUJAWAWEKA MAGAZETINI PIA MTOAJI PIA AJIULIZE KUNA UMUHIMU WA KUWEKA FEDHA KATIKA BAHASHA AU KUZIONYESHA JAPOKUWA KIWANGO KIMESHANADIWA?KUNA UMUHIMU WA KUTUMIA HUNDI? HAYA BAADHI YA MASUALA YA KUJIULIZA ILI KULINDA HESHIMA YA HAWA WENZETU TUNAOWASIDIA KWANI KUWA MASIKINI ISIWE NDIO CHETI CHA KUONDOA UTU WAO.
HII NI CHANGA MOTO TU NATOA ILI TUIFANYIE KAZI KWA MANUFAA YA WATANZANIA WENZETU AMBAO TUNAWALENGA KWA MISAADA NA KUHAKIKISHA THAMANI YA UTU WAO INABAKI 'INTACT'
MDAU.
COLORADO,USA.
Ubarikiwe sana Binti Mtemvu, hakika Mwenyezi Mungu ndiye atakayekurudishia wema huo. Big up girl...
ReplyDeleteNi Vizuri sana kuwasaidia wanaohitaji misaada yetu lakini hili la kutangaza kwenye vyombo vya habari au kujitangaza kuwa umetoa msaada kwa mapicha na habari kemkem kwenye vyombo tofauti nafikiri tuliangalie tena na kujiangalia wenyewe nini dhamira yetu hasa pale tunapotoa misaada
ReplyDeleteNaungana na ndugu yangu wa Colorado USA umesema yaliyo sawa kabisa
Mdau kutoka Colorado USA naungana nawe kwa mikono na miguu yote. Hata mimi sipendi watu wanaotoa msaada then wanapangwa kurasa nzima ya habari kuwa wamempa mtu hela sjui nini hii itakuwa back door mtu anaandaliwa kushika madaraka flani so akija waseme alikuwa anasaidia. Kiukweli ukiwa unasaidia watu hata usipojitangaza utashangaa wao wenyewe watakavokutangaza. Tuwe na utu jamani ni sawa na baadhi ya watu dar enzi hizo sisi wa mikoani ukifikia kwake wakati wa likizo basi upate kikazi anakutangaza ulivokuwa unakaa kwake kama si yeye usingekuwa hapo ulipo jamani hayo yote ya nini? kama mtu umemtunza lazima atatangaza tu mema yako. Tunashukuru wewe Sitti umesaidia ila si lazima kupblish namna hii.
ReplyDeleteMdau UK
naungana na mdau mmoja aliyetoa maelezo yake lakn baadae akamalizia kwa kusema..'anyway hawa ni tabaka la siasa hivyo pengine yupo kwenye maandalizi ya kisiasa ndio maana akaweka hadharani msaada wake...si unajua bongo mtoto wa mwanasiasa ni mwanasiasa baada ya baba au mama yake?.
ReplyDeletekazi kwenu watanzania wenzangu.
Hongera Sitti Mtemvu,
ReplyDeleteLicha ya uchambuzi uliofanywa hapo juu kuhusu mtindo na taswira ya utoaji,,,pamoja na mapungufu yaliyotajwa ukweli ni kuwa hiki kitendo cha kutoa kinawapa mwamko walio wengi kujitahidi na kuwakumbusha ya kuwa ni muhimu kuwafikiria wenzetu walio ktk hali tete, pia kutoa hakuhitaji uwe na Utajiri wa kupindukia kile unachoona ni kidogo kwako ni kikubwa kwa muhitaji aliye katika shida!
Kutangaza ktk vyombo vya habari siyo vibaya ila pia kiusalama haipendezi.Ndio mwanzo wa kuwaandaa vibaka kuvizia hata kukata nyavu za madirisha kwani wanajua kuwa pesa iko ndani,hata wenye shida wengine kama ndugu na marafiki wanaweza kufanya usumbufu kwa kwenda kukopa kwani wameshatangaziwa kupewa hela.
ReplyDeleteMDAU BONGO DSM
Nyinyi mnaosema watoa misaada wasijitangaze ni wanafiki wakubwa! Mbona slaa alipotoa msaada kwa walemavu Mwanza alijitangaza katika Tanzania Daima, Mwana Halisi, ITV na jamii forum! acheni unafiki wenu wa kichadema...
ReplyDeleteIwe alitoa msaada Slaa, Siti au hata awe nani.
ReplyDeleteKutoa tunaambiwa ukitoa mkono wa kulia wa kushoto USIJUE. Huko ndio kutoa.
Huku kutoa kwa mapicha na shughuli sawa umetoa lakini ni kwenye macho ya ulimwengu, kwa mwenyeezi mungu kutoa huku hakukubaliki.
Kuna mtoa mada kachangia amesema ''labda anaandaliwa kanafasi'' akirudi tushtukie kalamba nyadhifa.
TAFUTA KAMUSI NDUGU ULIOTOLEA MFANO WA 'SLAA' HAPO JUU UKISHAJUA MAANA YA 'UNAFIKI' ANGALIA VEMA MAELEZO YA WACHANGIAJI KUHUSU KUTOA MISAADA NA KUHESHIMU UTU WA WA WALENGWA PAMOJA NA USALAMA WAO.
ReplyDeleteHUKUULIZWA NANI NA NANI WAMEJITANGAZA NA KATIKA MAGAZETI GANI?USIAMKE NA KUROPOKA OVYO ANGALIA WATU WANAONGELEA NINI?
WEWE UNAONGELEA MAMBO AMBAYO SISI WACHANGIAJI HATUNA AJENDA NAYO,SASA HUONI KAMA MNAFIKI UNAWEZA KUWA WEWE USIEJUA UNACHOONGELEA KUWA HAKIHUSU MADA INAYOZUNGUMZIWA?
NIMEJARIBU KUELEZA WAZI UMUHIMU WA KUTOA NA UWEZEKANO AU UMUHIMU WA KUTUJULISHA NA SISI ILI TUJUE WAPI MSAADA UNAHITAJI BILA KUDHALILISHA AU KUHATARISHA USALAMA WA WALENGWA KAMA ALIVYOCHANGIA MWENZANGU KATIKA SUALA HILO SASA WEWE UMEKUJA NA HOJA YA MIFANO YA KINA SLAA NA MAGAZETI HAMSINI NANI KAKUULIZA UTOE MIFANO SOMA UPYA UONE KAMA KUNA MCHANGIAJI YOYOTE ALIYEGUSIA KUWA HAMNA ALIYEWAHI KUJITANGAZA?
USHAURI WA BURE SOMA MADA JIBU IKIWA IKO HAJA NA USITOKE NJE YA MADA KAMA UNAO UWEZO HUO KIAKILI VINGINEVYO UNATUJUULISHA WENGI KUWA KUNA TATIZO KATIKA UBONGO AU MADARASA.
MDAU.
COLORADO,USA.
NI kawaida kutoa msaada na kujitangaza ili ninyi wengine mjue kuwa nilitoa msaada ukitoa kimyakimya sasa nani atajua?hapo akirudi huko Marekani aombe msaada mwingine wamkubalie kumpa tena,si kweli ni pesa ya bajaji kama alivyojielza ni kawaida watanzania kujidanganya,any way tunamshukuru kwa msaada aliotoa
ReplyDelete