Mkurugenzi wa Asasi zisizo za kiserikali Bw.John Ulanga akiongea wakati wa semina ya kujadili bajeti ya nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka 2012/13 wakifatilia semina hiyo iliyoandaliwa na Taasisi inayojishughulisha na mambo ya uchumi ya Deloitte,katikati ni Mwenyekiti wa shirikisho la viwanda Tanzania Felix Mosha na Mkurugenzi mtendaji wa Samaria Groups Jayesh Shah.
Mtaalam wa Maswala ya Kodi na nishati ya umeme wa kampuni ya Deloitte Bill Page akichangia mada kuhusiana na bajeti ya nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka 2012/13 wakifatilia semina hiyo iliyoandaliwa na Taasisi inayojishughulisha na mambo ya uchumi ya Deloitte.
Asanteni wadau kwa kuchangia mada za kiuchumi nchini kwetu. Ijumaa iliyopita nilikuwa Hapo hapo na kina Ernst & Young, pia PwC walikuwa na wadau wengine Hilton na KPMG pia. Jitahidini na njie mfanye shughuli hii mapema ijumaa wakati mambo bado moto. alexbura dar
ReplyDeleteMnachanga kwa ari endapo:
ReplyDelete1.Limetokea suala nyeti
2.Mna lengo la maendeleo
3.Mna lengo la kujiimarisha kihali
Lakini ile puuu 'kapu' limejaa watu wanakaa mafungu mafungu tayari tayari kwa mkao wa kula!
Ghafla kapu linakuwa limetoboka chini hakuna hata ndururu moja ndani!
Pana Mzee mmoja hapo analalamikiwa sana na watu katika masuala ya uwekezaji wa Mitaji!
Deloite ni Taasisi mnaheshimika!,
ReplyDeleteMjadala wa wenu umehusisha waliomo hapo kutajwa ktk Ufisadi zaidi kuliko maendeleo ya Uchumi.
Sasa Semina yenu hapo ilihusu maendeleo ya Ufisadi au maendeleo ya Uchumi?
Ni muhimu masuala ya watu kutajirika kupitia Wizi,Rushwa na Ufisadi wahukumiwe Kibiashara!
ReplyDeleteHaiwezekani masuala yanayohusu Thamani kuamuliwa Kisiasa au Kijinai pekee,
Mfano Mhalifu anavuna fedha kwa njia chafu anatajirika, kinachotakiwa apigiwe mahesabu ijulikane mali yake halali ni ipi na haramu ni ipi halafu ile isiyo yake ni ya Mamlaka anafilisiwa anabakishiwa kiasi kilicho cha kwake au zaidi anapewa Mgawo wa Hisa kidogo.
Mahakama za masuala haya zitumike za Kibiashara zaidi huku Wadau kama SFO, mamlaka ya Kodi TRA ,Interpol,ICC na Transparecny International n.k.
Ni wazi tutaendelea tukiwa Kibiashara badala ya kuendesha mambo Kisiasa !