Mwenyekiti wa Wasanii wa Bongo Movie,Jacob Steven "JB" akikabidhi msaada wa vyandarua kwa Muuguzi Msaididi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga,pia Mwalishi wa Hospitali hiyo,Bi. Halima Msengi (kushoto) wakati wasanii hao walipotembelea hospitali hiyo na kujioneea hali halisi ya uhaba wa vyandarua katika baadhi ya wodi.Msaada huo umekabidhiwwa hospitalini hapo mapema leo asubuhi kwa hishani ya kampuni ya Bia Tanzania Kupitia kinywaji Chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Muuguzi Msaididi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga,pia Mwalishi wa Hospitali hiyo,Bi. Halima Msengi (kushoto) akipokea Vyandarua kutoka kwa baadhi ya wasanii wa Bongo Movie waliofika Hospitalini hapo leo.
Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na Mwenyekiti wao Jacob Steven "JB" wakiwa kwenye picha ya pamoja na Muuguzi Msaididi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga.Wasanii hawa wametembelea Hospitali ya Bombo mapela leo asubuhi kwa ajili ya kukabidhi msaada wa Vyandarua katika hospitali hiyo,ikiwa ni sehemu ya kupiga vita ugonjwa wa Malaria unaopoteza maisha ya watanzania wengi katika maeneo mbali mbali ya nchini.Msaada huo umekabidhiwwa hospitalini hapo kwa hishani ya kampuni ya Bia Tanzania Kupitia kinywaji Chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Wasanii wa Bongo Movie wakiwa wamezunguka kitanda cha Mmoja wa Mama aliejifungua watoto Mapacha katika Wodi ya Wazazi wa Hospitali ya Bombo Jijini Tanga mapema leo asubuhi wakati walipofika kutoa Msaada wa Vyandarua kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Kinywaji chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Mama Consolata Adam akimjualia hali Mmoja wa kina Mama waliojifungua leo kwenye wodi ya Wazazi,Ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Bombo,Jijini Tanga.
Michu, wasalam alekhom. Asante sana mkubwa kwa juhudi zako za ujasiliamali,maana umetuunganisha katika pande zote za dunia. Sasa basi dukuduku langu leo ni hii picha katika hosibitali hii ya Tanga, ndugu zangu, hivi vitanda ni imara sana ila tu angalieni rangi yua vyuma vyake ilivyochakaa,ni aibuuuu. Kipi kigumu hapo, je kikopo kimoja cha rangi ya blue ni bei gani ?????. kwanza hongera sana ,maana sisi wabongo hatuna noma za kulialia na kulalamika hovyo,angalieni hapo,kila mgonjwa kaja na shuka zake au kama hana shuka basi ana khanga katandika,hapo tayari ameipunguzia makali serikali yetu tukufu,sasa hata rangi !!!! Zebedayo msema kweli.
ReplyDeleteKaka,
ReplyDeleteHuyo Meneja wa kinywaji cha Grand Malt huyo mwambieni apunguze kidogo kunywa hizo grand malt jamani.
Khaah!
jamani hivyo vitanda havina shuka hata za koreja? Hospitala kuu ya mkoa vitanda kama hivyo? Kutu si kutu rangi si rangi ilimradi kimeitwa kitanda.Serikali ya mkoa hebu ondoeni hiyo aibu.
ReplyDelete