Bwana Erick Morro akisubiri wageni ili kutoa maelezo juu ya Tanzania na NGO yake ya TALENT SEARCH AND EMPOWERMENT(TSE).

Kuanzia tarehe 14 mpaka 17 Juni 2012 Watanzania tuishio katika mji wetu wa Nürnberg katika jimbo la Bayern tulishiriki kwa kikamirifu katika tamasha la mara ya tatu(3) la Afrika Festival hapa Nürnberg.

Katika ushiriki wetu tuliweza kuitangaza nchi yetu ya Tanzania, lugha yetu ya Kiswahili pamoja na kutoa ushirikiano mkubwa wa kutafuta misaada kwa shirika(NGO) inayoitwa TALENT SEARCH AND EMPOWERMENT(TSE) iliyopo Ubungo Kibangu, Dar es Salaam.- www.tsempowerment.org-

Shukrani za dhati tunaomba ziwaendee Mr. Albert Machoke, Mr. Ramadhani Barungi, Mr. Erick Mome Morro pamoja na mkewe Tamara Morro na mtoto wao Pamela Morro, Mr. na Mrs. Mukada, Dj Maxwell , Watanzania na Wajerumani wengine waliofika kulitembelea banda letu la Tanzania katika Festival hiyo.
Bibi Tamara Morro akitoa maelezo kwa mgeni aliyefika katika banda la Tanzania.
Mkaazi wa Nürnberg akipata kikombe cha Gahawa murua kutoka Tanzania.
Bwana Ramadhani Barungi akitoa maelezo kwa mgeni aliyefika kutembelea banda letu.
Baadhi ya Watanzania wakitoa maelezo juu ya Tanzania kwa Wajerumani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2012

    Big up watanzania wa Nürnberg.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2012

    safi sanaaaaaaaa nimefurahi. na nimemuona franz kwenye picha. na nimezipenda zote kwa ujumla na nililipenda sana banda la maonyesho lilitokelezeaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...