Waziri Mkuu wa Uholanzi,Mh. Mark Mutte akirejea nyumbani kwake toka mzigoni kwa kutumia usafiri wa injini kiuno (baiskeli) huku akiwa hana noma wala nini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2012

    why dont we copy and paste this?
    lakini inabidi labda ofisi zihame dar zihamie mbali kabisa labda Lushoto.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2012

    Hii kwa Tanzania hata iwe vp hawawezi kufanya viongozi wetu bila vingo'ra tutawatambuaje

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2012

    safi kabisa hiyo wao wanabana matumizi sisi tunatanua na mashangingi halafu baadaye tunapeleka kibakuli kuomba

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2012

    mazingira yana ruhusu. Bongo utahiendeshea wapi! LOL
    mdau paris

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2012

    Ukiwa kiongozi safi hata kutembea au kupanda daladala unafanya tu. Wenzangu na mimi wakijaribu wanatwangwa mawe na wananchi hadi kieleweke, maana ni maadui zaidi ya mengineyo. Inabidi wajifiche fiche au wapite kwa kasi sana, japo wananchi wengine wana shabaha tu bado.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2012

    yes ni kweli kabisa huyo ni waziri mkuu wa hapa uholanzi

    viongozi wa hapa kuanzia mawaziri na wengineo wote huwa tunapishana njiani na baskeli amani ya nchi hii ulinzi upo juu sana

    waziri mkuu anatumia baskeli na usifikiri labda maisha ni magumu hawa watu wa mihela vibaya sana

    baskeli ni moja ya mazoezi sio kujilemaza na magari masaa yote

    ni mfano mzuri wa kuigwa huko nyumbani mpaka mwenyekiti wa serikali za mitaa basi utamuona na gari

    mwendo pengine wa dakika 5 kwa miguu kiongozi wa kibongo ni lazima afike na gari ili kuonyesha ufisadi wake nje nje

    hapo ukiangalia viongozi wetu matumbo yamevimba vitambi mafuta tupu bp na sheli havichezi mbali

    big up viongozi wa uholanzi kwa kudumisha mazoezi kwani afya ni muhimu.

    Mdau uholanzi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 06, 2012

    Mnaona wanasiasa wa bongo?
    Wenzenu wanajinyima hawana makuu, wakati ninyi mnatumia mabilioni kwa mashangingi nk. Alafu mtu eti ni waziri wa kawaida tu bongo, wengine wana wapambe nk. Hizi pesa za wakulima mnazichezea hivyo hamjui kuwa ni laana?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 06, 2012

    Mwambie waziri wa bongo aendesha ata piki piki tu kama atakubali. Wao ni magari yanayokunywa mafuta kama wako yanakotoka, na gari lake mwenyewe anataka na dreva wa kumwendesha.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 06, 2012

    Sishauri viongozi wa bongo kufanya hivi mazingira ya bongo hayaruhusu kabisa. Huko ni netherlands rami kila sehemu, ulinzi wa kutosha ila bongo sio hivyo. Sio kila kitu ch kuiga jamani hata kama ni chema.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 06, 2012

    namjengea picha mizengo pinda na picha yenyewe haiji,yani ni imposiboooooooooooooo....

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 06, 2012

    Jamani wenzetu wako mbali sana...magari,mavazi sijui mbwembwe gani havina nafasi kwao.Sisi ushamba na umaskini unatusumbua..he na ubinafsi pia!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 06, 2012

    We anon wa tatu umesema exactly nilichotaka kusema... Mawaziri wa Bongo wakisafiri wanaenda 1st class tena saa nyingine na waziri wa nchi tajiri wanatanuaa.. wakishuka tu nchi tajiri vibakuli juu.. help help help. Inatia hasira kweli

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 07, 2012

    Mimi ni Mtanzania wa dutch wanasema geboren en getogen ila ninaishi uholanzi kwa zadi ya miaka 25 sasa na nimefanya kazi katika taasis mbali mbali za kijamii na za kiserikali hapa uholanzi.
    Baadhi yawatoa mada hawaelewi hali ya Uhalanzi ilivyokwa hivyo hawa wezi kulinganisha na Tanzania. Kwa usafiri wa baiskeli uholanzi ni kitu cha kawaida kabisa, ni kwamba kama wewe huna baiskeli ni kitu cha ajabu kabisa, ukiwa muhamiaji kituchakwanza unafundishwa kuendesha basikeli na lugha, pili ukizingatia nchi hii ni tambarare, pili usalama lakini pamoja ya yote hiyo nyumba ya waziri mkuu iko uwani tu wa ofisi yake...........pamoja na usalama wote uliokuwepi nchi hasubuti kuingia mjini na baisikeli, hata Malkia anaendesha baiskeli, lakini uwani kwake na maeneo ya karibu ambayo yote ni hifadhi ya kifalme. Na wote mpaka mawaziri wanamagari ya kifahari na wanaendeshwa vile vile, wao na watoto wao, kwa hiyo msipotoshe.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 07, 2012

    Anonymous said.
    Joto letu la Tanzania nalo linachangia maana anaweza kuloa jasho mwili mzima. Maana offisi nyingi zipo Dar ambapo joto nikali sana huwezi kulinganiasha na hao wenzetu hali inaruhusu kufanya hivyo. Muhimu ni kuangalia namna ya kupunguza matumizi tu kwa aina ya magari wanayotumia viongozi wetu.

    Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 07, 2012

    Tanzania! Tanzania! Tanzania!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 07, 2012

    ati kwatu hawawezi hakuan barabara kwani wenzetu walijengewa na kina nani? uongozi bora ndo unafanya nchi zza wenzetu zinapaa huku kwetu umimi ndo umechangia kuwa maskini wa kutupa, aah bora tubanane nao huku kwao manake huko home ndo utumwa wakubwa ndiyo walaji hadi tumetimkia mbali.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 07, 2012

    Ohoooo

    Hawa Mawaziri wetu wamezoea Ufalme nchi yetu masikini sana lakini wao wanatumia VX-V8 !!!

    Kama wataambiwa na Raisi watumie baiskeli walahi ni wazi wanaweza kujiuzulu Uwaziri!!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 07, 2012

    Itakuwa ni Kiama na mwisho wa Dunia kama hali hii itatokea Tanzania na hasa kwa Viongozi wa Afrika!!!

    Jamaa zetu huku ni Nusu Miungu kwa aina ya usafiri wanaotumia!!!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 07, 2012

    Mawaziri wa Tanzania waendeshe Baiskeli waote 'vingimbi' vya miguu,kuwa vifua 'tongwa' na kuwa Vijeba?

    Asalaleee nani atakubali?

    Labda Marehemu Baba Nyerere angekuwa hai ndio angekubali!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 07, 2012

    wewe unaejifanya umeishi uholanzi miaka zaidi ya 25 wacha ushamba wako na ulimbukeni

    wacha kujifanya unajuwa sana maisha ya uholanzi pengine wewe ni mpishi tu tena muosha vyombo ukafanye kazi kwenye serikali ya nani uholanzi?

    usidanganye watu eti baskeli wanaendeshea uwani tu

    sisi wote tunaishi hapa uholanzi na tunawaona viongozi sana tu na baskeli zao mpaka mitaani

    kama unakumbuka hata yule mtengeneza sienema ambae ni tajiri alieuliwa pale amsterdam na Mohamed B, alikuwa akiendesha baskeli

    wacha kutetea mafisadi wa tanzania kazi yao kutumia mali za umma vibaya mpaka mjumbe wa nyumba kumi ana shangingi.

    mdau uholanzi.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 07, 2012

    Acheni masihara ninyi! Wanafunzi wenyewe tumeshindwa kuwapatia usafiri sasa mnataka eti wanasiasa wetu waendeshe baiskeli.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 07, 2012

    mimi huwa naendesha baskeli to work every now and then kwenda jobu hapa dar ila ningumu. Yaani barabara zilizo na lami zote zimejaa mchanga pembeni, ukisogea pembeni unaweza angushwa na mchanga na ukisogea katikati ya barabara unaweza gongwa. Zile pedestrian pavements nazo zikichimbwa hazirudishiwi kama zilivyokuwa kwa kuwa magari hayapiti so no one cares. Halafu akili mbovu nazo zinachangia, Selander kuna kuna njia ya baiskeli saafi lakini ukifika kwenye njia panda inabidi ushuke maana hamna slope to allow a smooth transition

    Che

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 07, 2012

    Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wotee. Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana. Nilalapo nakuota wewe. Niamkapo ni heri mama weee...Tanzania Tanzaniaaa

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 07, 2012

    Tusiangalie tu kwa Viongozi wetu. Je, vijana wa chuo nao wanashindwa nini kufanya hivi? Kama wanashindwa wakati wakiwa Vijana, wakija kuwa mawaziri wataweza? Au hata wafanyakazi tu wa kawaida, tusiwaseme viongozi sana wakati hata sisi katika familia zetu baiskeli ni alama ya Umasikini.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 07, 2012

    Anonimous wa Thu Jun 07, 12:24:00 AM 2012. Huyo malkia Holland mbona mzee sana kuweza kuendesha baskeli?
    Takwimu zinaonesha kazaliwa 31 januari 1938. Halafu mbona hakuna hata taswira moja inayoonesha anaendesha baskeli'uwani' kwake au maeneo ya kifalme?
    Mark Rutte hakai uwani kwa 'ofisi' yake. Google utaona maisha yake ikiwa ni pamoja na kuwa single nk.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 07, 2012

    Nyie mnaesema kuwa hiyo kiyu bongo haiwezekani kwa sababu ya amani, mnaishi wapi? Kila siku Raisi na serikali yake wanasema Tanzania kuna amani, sasa nini cha kuogopa. Wapite tu----Kuna amani yeti misafara yao ina magari zaidi ya 30--wanapita kama wanafukuzwa na simba. Raisi juzi ameonyeshwa nafanya mazoezi ya kutembea---lakini kazungukwa na watu so chini ya kumi, wanaogopa nini??????? Mtu analala njaa, unasema anaamani??????????wapite tu na baiskeli.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 07, 2012

    Sio hawa Miungu Watu wetu wa sasa!

    Kiongozi wa kuendesha baiskeli nchini Tanzania alikuwa ni mmoja alikwisha fariki tarehe 14 Oktoba 1999 na mmoja aliwahi kufungwa miaka 27 Gerezani yupo hai huko Afrika ya Kusini!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 07, 2012

    Enheee !

    Wenye Uchumi wao imara na Fedha zao haooo Viongozi wao wanatumia baiskeli, tena hii hata kwa nchi zingine za Ulaya labda UK (Uingereza-Mtawala wetu wa Ukoloni, maana sisi tumerithi Umwinyi kwao) , Hii hata Uingereza thubutuu huwezi kuona hivi!

    Kama ingekuwa sisi tuna hali ya tahfifu na uwezo kama Uholanzi, asalaleeeee Mawaziri wangeagiza Ndege kila mmoja!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 07, 2012

    Jamani angelieni mmeona wanaojua kubana matumizi?

    Tena hawa jamaa Uholanzi wanatupatia Misaada kibao tu,

    Ndio hali ilivyo hata ktk maisha familia zetu mmoja unaweza kujibana kimaisha halafu mwingine ktk familia anapiga 'kiberiti' tena bila wasiwasi kile ulicho jibana kukitafuta!!!

    Hela yao nyingi wanajibana wao Uholanzi lakini zikifika kwetu zinaliwa na Mafisadi!!!

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 07, 2012

    Huyo Mwandishi wa Habari Mpiga atakuwa Mwingereza!

    Kwa kupenda 'ujiko' na Umwinyi Mwingereza yupo juu pia, si mnaona Mastaa wao wa Mpira na Ukoo wao wa Ki Falme?

    Maana Mwingereza na sisi (Tanzania) sawa sawa kwa madoido, anasa na kupenda Ubwana Mkubwa.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 07, 2012

    Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni!

    Huyo Mwana Habari anayechukua Picha atakuwa kama sio Mwingereza, atakuwa Mmarekani ,Muitaliana au Mspaniola!

    Hao ndio wapenda ujiko na Ufahari Duniani, Mwandishi wa kutokea nchi hizo za anasa anashuhudia MAAJABU YA MUSSA YA KIONGOZI WA NCHI UHOLANZI anaamua kuchukua picha kwa Libeneke!

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 07, 2012

    Haya basi viongozi wetu wanadai joto baiskeli hawaiwezi, je gari aina ya suzuki maruti pia mna hoja kwa nini msitumie badala ya VX,BMW,shangingi n.k
    Mdau
    Kigamboni Feri

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 07, 2012

    Wabongo tu kila kitu mna complicate

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 08, 2012

    misupu katika kusoma comment kuna mdau kanifanya niulize please nakuomba mdaau mwenzangu wa 12:37 tuweke wazi japo kwa kututajia jina la hawa watu, aliyefungwa miaka 27 gerezani na aliye fariki 1999 please ni soma zuri sana la historia hili please mdau mwenzangu nielimishe please

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 08, 2012

    Mdau wa 34 hapo juu Anonymous wa Fri Jun 08, 02:04:00 PM 2012

    Ni kuwa aliyefariki tarehe 14 oktoba 1999 ni JULIUS KAMBARAGE NYERERE ambaye ktk Tanzania yetu ndiye kiongozi angekubali kutumia usafiri wa baiskeli!

    Na pia aliyefungwa miaka 27 Gerezani ni Mzee Nelson Mandela angali yu hai aliyepo Afrika Kusini yeye ndio aliyebaki Duniani anayeweza kutumia aina hii ya usafiri wa baiskeli!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...