Karani wa Uandikishaji wa Wananchi katika zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu wa Tanzania(jina lake halikupatikana mara moja),akifanya kazi hiyo mchana huu katika Kata ya Mikocheni A jijini Dar es salaam, huku akiwa amezungukwa na Wakazi wa eneo hilo waliojitokeza kwa wingi ili waweze kusajiliwa.
Wakazi wa eneo hilo la Mikocheni A Kata ya Darajani wameulalamikia utaratibu wa Usajili wa namna hii,huku wengine wakisema umekuwa na usumbufu mkubwa,kutokana na Makarani hao kuifanya kazi hiyo katika hali ya taratibu mnoo. Mmoja wa wakazi wa eneo hilo alibainisha kuwa karani mmoja anawaandikisha watu zaidi ya mia, kwa hali hiyo tayari ni kero kwa namna moja ama nyingine, kwa sababu baadhi yao imewalazimu kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu huku wengine wakikata tamaa na kuondoka bila ya kuandikishwa.

utaratibu wausajili unakuwaje kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi?
ReplyDelete