Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi (kulia) akitia saini makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Jimbo la Gujarat, India, Bw.Girish Chandra Murmu katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaa wiki iliyopita.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara wa Jimbo la Gujarat India, Bw. Bharat Mody katika mkutano wa wafanyabiashara wa watanzania na wenzao kutoka jimbo hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesaini makubaliano ya kibiashara na Jimbo la Gujarat la nchini India ambapo wafanyabiashara wa pande hizo mbili wanatarajia kunufaika na ushirikiano huo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Bw.Raymond Mbilinyi alitia saini makubaliano hayo kwa niaba ya TIC wakati Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Jimbo la Gujarat Bw.Girish Chandra Murmu aliwakilisha upande mwingine mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lilishuhudiwa na wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao kutoka kampuni 10 za Jimbo la Gujarat India.

“Makubaliano ambayo tumesaini yatawezesha wafanyabiashara wa pande hizi mbili kuwa na ushirikiano wa kibiashara ambapo watanzania wataweza kuwekeza Gujarat na wao kuja kuwekeza nchini,” alisema Bw. Mbilinyi.

Alisema jimbo hilo lililopo Magharibi mwa India limeendelea kiuchumi katika nyanja za uzalishaji nishati ya umeme, kilimo, viwanda, uchimbaji mafuta na gesi hivyo kuja kwao nchini kutasaidia kupata ujuzi na teknolojia katika maeneo hayo.

Alisema nchi ya India ina mahusiano ya muda mrefu ya kibiashara na Tanzania kwani India ni nchi ya pili kwa wawekezaji waliowekeza hapa nchini hivyo makubaliano hayo yataongeza kasi ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Katika mkutano huo, wafanya biashara wa nchi hiyo waliweza kukutana na wafanyabiashara wa hapa nchini na kujadili maswala ya kibiashara na kujionea fursa mbalimbali zilizopo.

Kwa upande wake, Bw. Murmu alisema wako tayari kushirikiana na wenzao wa Tanzania kwa faida ya pande zote mbili.

“Tumekuja kuangalia fursa zilizopo na tuko tayari kushirikiana kwa faida ya pande zote mbili,” alisema Bw. Murmu.

Alisema mahusino haya pia yanatoa fursa kwa kampuni za hapa Tanzania kwenda kwao kujionea fursa zilizopo na kuwekeza au kupeleka bidhaa mbalimbali ambazo wanazalisha katika Jimbo la Gujarat.

Mjumbe wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI), Dkt.Samuel Nyantahe alisisitiza kuwa Tanzania inahitaji kuzalisha na kuyaongezea mazao yake thamani ili kuyatumia masoko ya nje likiwemo soko la jimbo la Gujarat.

“Wenzetu hawa wamekuja kujionea fursa zilizopo na kuzungumza na wafanyabiashara ,laikini kikubwa wenye viwanda tunasisitiza tuzalishe na kuyaongezea mazo yetu thamani ili tushiriki vizuri katika mahusiano kama haya,”alisema Bw.Nyantahe.

Alisema ni lazima nchi ijiepushe na uuzaji wa mali ghafi nje ya nchi na hatua hiyo ikifikiwa uchumi wa nchi utaimarika vya kutosha na kuboresha maisha ya wananchi.

Mkutano huo wa siku moja uliandaliwa na Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kwa kushirikiana na CTI na Chama cha Wenye Viwanda, Biashara na kilimo nchini (TCCIA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2012

    Hapa sasa ni sawa kabisa, kwa kushirikiana na wahindi yaani ni fresh kabisa SIYO wachina wenye vifaa vya kulipua, wao wameweka mbele sana pesa ubora hakuna. Ila ninachoomba tu ni kwamba , wasichana wa Kihindi nao wakubali kuolewa na waswahili !!! Mbona wazungu tunawaoa ??? Nyie wahindi vipi ?? mbona wagumu ??? Mimi Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...