Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliemaliza muda wake,Dr. Asha-Rose Migiro akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere,leo mchana. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe na kulia ni Mume wa Dk. Asha-Rose,Profesa Cleophas Migiro.
Dr. Asha Rose Migiro (katikati) akiteta jambo Waziri Membe sambamba na Viongozi mbalimbali wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakiongozwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberi Kacou (kushoto) waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Mwl. J.K Nyerere.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 10, 2012

    Hongera Dr. Asha Rose Migiro kwa kutuwakilisha vizuri UN katika nafasi ya pili kutoka juu kwenye Umoja wa Mataifa.

    Pili naunga mkono uamuzi wako wa kuamua kurudi Chuo Kikuu kufundisha, Hii itaweka bayana msingi kwa Watanzania na Waafrika kuwa unaweza kustaafu siasa na kurejea kwenye fani yako ya asili kama unavyotarajia kufanya wewe.

    Naamini Makamu wa Rais wa Marekani wakati wa Bill Clinton, Dr. Al Gore naye baada ya kutoka White House alirejea kufundisha.

    Hongera sana na karibu Nyumbani.

    ReplyDelete
  2. Karibu nyumbani mama Asha Rose Migiro!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 10, 2012

    Karibu sana bado tunahitaji mchango wako

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 10, 2012

    ..................Naamini Makamu wa Rais wa Marekani wakati wa Bill Clinton, Dr. Al Gore naye baada ya kutoka White House alirejea kufundisha."

    SO WHAT!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...