Baba yangu Mzazi Mzee Charles Omari na mama yangu Mzazi Agnes Omari katika Kanisa la Mtakatifu Lorenzo – Kibamba – Dar es Salaam kumeremeta upya baada ya miaka 50 ya ndoa takatifu
Mzee Charles Omari na mama yangu Mzazi Agnes Omari tayari kwa mnuso
Mama akijiandaa kumvisha upya baba pete ya ndoa
Baba akimvisha upya mama pete ya ndoa
Maharusi na wapambe wao mnusoni
Peter Omari na mai waifu wangu tukitoa neno la shukurani kwa wazazi wetu
Asalaam aleikhum kaka Muhidin Issa Michuzi!
Hongera kwa kazi nzuri unayoifanya kwa watanzania na raia wote wa Sayari hii ya Dunia tunao wasiliana nao kupitia chombo chako hiki cha kisasa cha mawasilaiano.
Mapema Mwezi huu Baba yangu Mzazi Mzee Charles Omari na mama yangu Mzazi Agnes Omari walisherehekea miaka 50 ya ndoa. Walirudia kiapo cha ndoa yao kwenye Kanisa la Mtakatifu Lorenzo – Kibamba – Dar es Salaam na baadaye kwenye mnuso wa kukata na mundu nyumbani kwao Hondogo – Kibamba – Dar es
Salaam.
Kwa ruhusa yako naomba kushirikiana picha hizi na wana ndoa wenzangu na wale ambao wanatarajia kuingia kwenye ndoa ikiwa ni kama ushuhuda kuwa kumbe inawezekana kuishi kwenye ndoa kwa muda mrefu.
Kwa wasio mfahamu Mstaafu Mzee Charles Omari alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu wakati wa utawala wa Mzee Ali Hassan Mwinyi kati ya mwaka 1985 na mwaka 1988 na alistaafu utumishi wa umma mwaka 1990 akiwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (Kulikuwa na Wizara inaitwa Wizara ya Ustawishaji Makao Makuu – Ministry of Capital Development (MCD) na Waziri wake wakati huo alikuwa Mheshimiwa mama Anna Abdalah.)
Mzee Charles Omari alifundisha Tabora Boys kati ya mwaka 1959 na mwaka 1963 na miongoni mwa wanafunzi aliowafundisha ni pamoja na jaji Joseph Sinde Warioba, Jaji Augustino Ramadhani na Joseph Mungai.
Alikuwa Mwafrika wa kwanza kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ifunda kati ya mwaka 1965 na mwaka 1969 na pia Mkuu wa Chuo wa kwanza wa Chuo cha Uongozi wa Maendeleo IDM - Mzumbe, na Kamishna wa Elimu ya Taifa kati ya mwaka 1983 na mwaka 1985 wakati wa utawala wa Rais wa Kwanza wa Tanzania.
Mimi Peter Omari ni mtoto wa saba wa Mzee Charles Omari na Mama Agnes Omari nikiendelea kutumika hapa Makao Makuu ya Sahara Media Group Ltd Mwanza nikiwa Meneja wa Vipindi wa Kiss FM lakini pia mtayarishaji wa Vipindi vya Kilimo Bora na Uchambuzi wa Hotuba Star TV. Pia ninaendesha kipindi cha Revival Times kila Jumapili asubuhi kupitia Kiss FM.
Watoto wengine wa Mzee Charles Omari na Mama Agnes Omari ni Mrs. Julieth Mgani, Mrs. Jane Mwanri, Arthur Mngoma Omari, Lilian Omari, pacha wangu Paul Omari na mziwanda Mary Mantissa Omari.
Kaka Michuzi nakushukuru kwa kunipa nafasi kuwang’arisha wazee wangu hawa kwenye libeneke hili kuu na linalo heshimika Duniani, na tuombeane dua njema nasi ndoa zetu zidumu na watoto wetu pia wapate maisha marefu nao pamoja nasi tuweze kuwa mashuhuda wa siku kama hii.
Ramadhan njema!
Peter Omari,
Programs Manager,
Kiss Fm Tanzania Ltd,
P.O. Box 1732, Mwanza, Tanzania.
Tel: +255 757/787 222 246.
Inapendeza sana
ReplyDeletePeter Omary, hongera na ziwafikie wazazi wetu hawa. Sasa ni haya yafuatayo, ndoto zako za kwamba na sisi tutakuwa na ndoa kama za hawa wazazi !!! ni ndoto za mchana ,hasa kwa kipindi hiki tulichonacho cha kizazi kipya. dada zetu wa kizazi hiki wamekuwa macho juu juu kama ya kinyonga,na ni limbukeni wa kutupwa ,siyo wasikivu kama mama yetu Agnes Omary ,tena wacha kabisa, huwezi kulinganisha. Hili ni janga linalozidi kukua tena kwa kasi, we have to address it daily, la sivyo ndoa kama hiyo ya wazazi wako na yenye watoto 9 !! haitaonekana tena katika dunia hii. Ni mimi Zebedayo msema kweli
ReplyDeletenawaombea kwa mungu kwa kutuonyesha mfano mzuri sana kwa jamii. mungu awape maisha marefu ya baraka tele na afya njema
ReplyDeleteameen
May God continue to bless you to celebrate 100 years of your marriage life. Peace and Love.
ReplyDeleteUmeandika vizuri Omari, well done. Hongera sana kwa kuwaheshimu wazazi. Mungu azidi kuwapatia wazazi wetu maisha marefu na yenye furaha. Kama bado wako hai, wafaidi. Ninawamisi sana wa kwangu, ambao wamekwisha tangulia kwa Mwenye Haki.
ReplyDeleteHongera wazazi wa Omari.
ReplyDeletePia Hongera Omari.
Nilichokipenda kingine kikubwa ni Uwezo wako wa kumpenda Baba yako na kuweza kuwa na historia yake ya kutumikia Taifa letu.
Tujifunze hili tusipoweza kuandika wenyewew historia za wazee wetu hakuna wa kutuandikia wanastaafu wanasahaulika kama hawakutumikia wala hawakumika na Taifa hili.
Kaka unayeema dada zetu hawashikiki ni wapi kina kaka wanashikika au ni watulivu kama Mzee Omari.
Usipende kuangalia upande mmoja tu au wanaume ndiyo wanahaki ya kuwa viruka njia.
unapoona ya kina dada na kina kaka ni hivyo hivyo pia ni kumuomba Mungu juu ya jamii yetu ambayo inaangamia kwa kukosa Maarifa ya Muumba wao.
Nyakati hizi ni za mwisho Ombea Taifa lako juu ya kila kitu.
Zebedayo wala hujasema kweli. Tunapenda sana kuwalaumu dada zetu kwamba ni macho juu,sie wanaume wa leo je,tumetulia? Tunatongoza mpaka kwenye facebook! Tuangalie mambo kwa mapana yake,tusitafute majibu ya mkato. Hata sasa inawezekana kabisa ndoa kufikisha miaka hamsini. Unadhani kipindi cha hawa wazee hakukuwa na vishawishi na makwazo? Kinachodumisha ndoa ni upendo wa kweli na uvumilivu. Hata sasa wapo kina kaka na kina dada wenye upendo wa kwweli. Hivyo kila mmoja kwa nafasi yake ajitahidi kudumisha na kuienzi ndoa yake,tutafika. Tuache kukimbilia visingizio dhaifu.
ReplyDeleteRamadhan Kareem kwa wale mnaofunga. Makobe karibuni staftahi!
Hongera sana kwa wazazi wetu hawa na pia sifa kwa Mwenyezi Mungu aliyewawezesha kuyashinda yote kwa miaka hiyo na pia kuifikia siku hii wakiwa pamoja.
ReplyDeleteNilisoma na Lilian na marehemu Salome pia.
Kwahiyo najisikia kama sehemu japo kwa mbaaali ya wazee hawa.
Mungu awabariki.
Kipapli
Hongereni sana, Mungu awabariki na kuwalinda wazazi na azidi kuwapa afya njema. Sisi wengine rafiki zao kina July walitulea sana wakati yupo mlimani.
ReplyDeletehayo maneno ya Zebedayo naomba nimuombe atuombe radhi wanawake kwani kwa kawaida kila kunapotokea jamb owanawake ni wa kulaumiwa ila kwa kuangalai statistics za researches zilizofanyika wanaume ndo wanaonekana wakorofi na kutokuwa waaminifu....hzo ni data ambazo zipo na zinajulikana. cha muhimu ulichotakwia ksuema ni pande zote mbili yaani mwanamke na mwanaume kuwe na umaninifu na kuvumiliana.
ReplyDelete"M'mungu awape wepesi katika siku za maisha yao" Kaka umesahau kitu kimoja tu umesahau kuweka picha zao za ndoa wakati Uleeeeeeeeeeee (kama zipo)zingeleta hamasa zaidi. Mshukuru Mungu kuzaliwa na lulelewa ndani ya ndoa kwani ni TUNU katika maisha.
ReplyDeleteHongera. Mungu awabariki. Nanyi watoto(?) kuwakumbuka/kuwajali wazazi wao. Wengine tunajifunza nini kwa familia hii. Wengi hata hawajali wazazi wao wanahali gani sasa. Kama unao piga simu sasa wajulie hali na uwaoneshe unawajali.GBUA (God Bless Yuo All)
ReplyDeletewewe unayesema eti wadada wa sku hizi macho juujuu kwani nyie wakaka wa siku hizi macho chinichini? kama kuoza wote tumeoza tu hakuna kulaumiana tatizo mnafikiri mume akiwa kiruka njia basi ni sifa ila mdada ndo muhuni kubalini matokeo. Hata zamani pia ndoa si zote zilizodumu kwa sasa mnajua coz of maendeleo na mawasiliano kila litokalo unajua ila kaa na wazee wa zamani wakusimulie utajua kuwa wanamshukuru Mungu those days hakukuwa na ukimwi. Alijiimbia masanja kuwa hakuna jipya chini ya jua yote yalikuwepo usifikiri ni uongo ukiona vimini vya sasa angalia picha za nduguzo za zamani. walikuwa wahuni wa kutupa ila walichotuzidi walikuwa na siri wamama wangapi wamekuwa wamezaa nje ila mume anakalishwa chini na kuambiwa amezee tu hiyo siri? wababa wangapi walikuwa na wake zaidi ya watano? tusihukumiane tu MAMBO YOOOOOOOTE UNAYOYAONA LEO KATIKA JAMII YALISHATOKEA NAWEWE SIKU UKIZEEKA UTASEMA VIJANA WA LEO WAMECHANGANYIKIWA THATS HOW LIFE IS. MAJARIBU YAPO NA YEYOTE AWEZA JARIBIWA SI MKE AU MUME LA MSINGI NI KUHESHIMIANA TU NA KUENDELEA HATA MUNGU ALIJUA WE WONT PLAY IT PERFECTLY NDO MAANA AKATUSISITIZA KUTUBU KILA SIKU MAANA HATA KAMA HUJAKMBWA BASI SHUKURU NI NEEMA YA MUNGU LAKINI WAWEZA ANGUKA TU SIKU MOJA. WAPO WALIOANGUKA UCHUMBANI, NDOANI NA WENGINE HAWAKUANGUKA.NI NEEMA TU YA MUNGU
ReplyDeleteNdugu Omary hongereni kuwa na wazazi mfano, ila mshikaji utafika pale? Mijia aka hiyoo 50? Mi ya kwangu inamiaka 20 na naona mambo fulani hivi!
ReplyDeleteebwana dada yako nafanya naye kazi pamoja, moja ya jina la baba yangu ni Omary, hivyo hujiita wote omary na zaidi jina langu linaanza na L. na dada yako linaanza na L.
Alinielekeza huwa nakuja pale mwanza kwenye kilekijiwe cha jioni pale na kushtu yananiii baridiiii.
hongereni sana wazazi, nakukumbuka sana peter tukiwa wote kibaha sec na st Gabriel kbh.
ReplyDeleteMungu awaongezee miaka mingi zaidi.
mgina frank
Hongereni sana wazee, tunawasifiyeni kwa kuwa ninyi ni mifano iliyo hai ya ndoa zilizodumu kwa nusu karne. Mungu awape afya na maisha marefu muzidi kupendana na kwa kuwa mzee ni mwalimu atunge japo kijarida kidogo cha maisha yake ya ndoa na misukosuko aliyoipitia tangu enzi za kuruka majoka bila shaka alikamatwa barabara na mama Omari mpaka wanazeeka wote. Hongereni watoto waliyozaliwa na wazee hawa bila shaka kuna miongoni mwenu atafuata nyayo za mzee na bibi.
ReplyDeleteHogereni Bw na Bi Omari Charles, mmeonyesha dira kufikisha miaka 50 ya ndoa yenu, kazi kwako seudende iga mfano wa wazazi
ReplyDeleteEng Kichonge, Baraka - Nelson Mandela African Institute of Science and Technology
SESE
Hongereni Sana wazee wetu na Mungu awazidishie zaidi Saba mara sabini
ReplyDeleteSeudende SESE
Hongereni sana wazee wetu Mungu awabariki sana na mtuombee na sisi wanenu tuishi nasi katika ndo zetu kiasi hicho
ReplyDeleteMngoma
Hongereni sana sana Mr na Mrs C. Omari. Mungu awabariki katika Ndoa yenu mfikie miaka 50 mingine.
ReplyDeleteNamoyo family.