habari kaka issa.,
Mimi mdau kutoka UK nina maoni yangu kuhusu wasanii wanaojiita kioo cha jamii naomba upublish kwenye blog yako ni jambo la aibu kwa msanii mkubwa awe wa music au maigizo ambao wanajiita bongo movie,kupeleka misaada kwenye kituo cha yatima juice,mchele.maharage,viroba vya sembe ambavyo thamani yake hata laki haifiki kwa hela ya madafu.

Wanatafuta na waandishi wa habari na kuwapiga picha watoto na kuwadhalilisha wakati kuna matatizo yanawakabili watoto makubwa zaidi hizo juice wanazowapa kama kweli wangekuwa na nia ya kuwasaidia wangewatengenezea mahali pazuri pa kulala kwanza na hivyo vyoo vilivyo katika hali mbaya kabisa sio kukaa kujinadi kwa kuwapiga picha watoto na kujitangaza kwenye mitandao ni aibu kwa taifa letu na hata mungu hapendi misaada ya namna hiyo ni kuwadhalilisha na sio kuwasaidia au nia yao kujinufaisha kwa kupitia yatima hao?

Kituo hicho cha yatima hao kinajulikana wapi kilipo lakini wao wanasema ukitaka kuwasaidia watoto hao uwasiliane kupitia wao walitakiwa watoe maelezo na adress ya wahusika moja kwa moja jinc ya kupeleka misaada sio kwa kupitia kwao tena wabadilike...

Wadau wenzangu ni ushauri tu maana ina niuma sana kuwaona wanavyo jishow off hao vioo vya jamii...
MDAU UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2012

    we mdau wa uk wewe.hao walao wamepeleka hata kidogo.eti hata laki haifiki.ungejua dhana nzima ya kudonate usingesema.utadhani hukai uk. utakuta hapa mtu anatoa hata one p ilimradi mwisho wa siku inaungana na ya mwenzake.hebu anza wewe utoe kila ulicho nacho tukuone.wabongo kwa kuosha.kuna watu bongo wanajilimbikizia mali hata sadaka hawatoi sembuse hao wanaotoa jasho lao. hebu kale pesa ya box ulalale siku ukishiba NENDA KATOE YOTE THEN UMFUATE YEYE ALIYEKUPA VYOTE.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2012

    we mbeba box kwanza rudi nyumbani usiwe mtumwa kwenye nchi ya watu, kutoa ni moyo bwege wee na kidogo walichotoa mungu anawaona kuliko wewe ambaye haujatoa hata kidogo, wangapi tunawaona wamegoma kurudi makwao mpaka mpigwe bomba, toa basi na wewe japo pound moja poooooor uuuuuu
    charles

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 05, 2012

    Jamani mko wapi, huyu mdau wa UK alitakiwa apewe vipande zaidi ya 20 na akome kabisa kuwa jeuri namna hii, eti yuko UK so what, ulishaambiwa kutoa ni moyo . Dola moja ukimpa mtu ambaye hana ,ni sawa na millioni moja kwake,au hujui hilo ?? hiyo laki moja unayoisema ni karibia ya dola 50 ni nyingi mno tena mno, ukijumlisha na muda wao walioutumia kwa jambo hili pia ni pesa tupu,mafuta waliyochoma kupeleka hivyo viloba ,ni pesa tupu, hiyo nia njema yao ya kutenda hicho kitendo cha kutoa ,ni pesa tupu. WEWE nenda bar kanywe hiyo dola 50 yako. Na wewe uliyesema kwamba ( anakuwa kama hakai UK !! shame on you, what you think,wanaokaa UK ni wajanja sana ?? au wajinga sana,you have seen the example. Zebedayo-msema kweli.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 05, 2012

    wewe jamaa wa UK una wivu wa kike, sasa wewe unataka wafanye nini , hata wakitoa kilo moja ya chumvi ni bora kuliko kukosa kabisaa, nyinyi wabeba box wengi kazi yetu ni kulaumu tu , kukosoa na kulaumu nyinyi ni mabingwa,

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 05, 2012

    Hata mimi nakubaliana na mbeba box, ulaya watu hawatoi zawadi kwa yatima na kujionyesha!! siku moja kati ya hao watoto mmoja anaweza kuwa BILL GATE, ni nani anataka kutangazwa umasikini wake eti kwasababu anapewa misaada!!!! Nilishaenda kwenye harambee ulaya na sikujua nani kanitoa nini na mtu alilipiwa hospital bills bila kujua ni msamalia mwema gani katoa. Tuache kujionyesha.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 05, 2012

    Mdau umesema kweli mana inatia aibu kweli kuona watu wanatafuta umaarufu kwa kupitia yatima misaada wala haitangazwi na kupigwa mapicha na hiyo misaada km hii MUNGU haipendi kabisa misaada ya kujionyesha wasaidieni ila msijionyeshe. Afu cc wala vumbi wa bongo choka mbaya tukae tukijua kwamba si wote walio ughaibuni wanapiga box wengine wana hela ya kulisha Tanzania yoote wanafanya kazi professional wengine wafanya biashara zao na wakisaidia hawatoi maneno.UUNGWANA NI VITENDO C KUJIONYESHA.

    MDAU MKEREKETWA

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 05, 2012

    Toeni misaada ila msijitangaze, ni dhambi. Mna-take advantage ya walio na shida, na bila ridhaa yao ya dhati wanalazimika kuwasindikiza katika njama zenu za kupata umaarufu ama kupaa katika umaarufu. Nendeni mkasaidie, ni jambo jema sana, lakini imeandikwa kuwa mkono wa kushoto usijue mkono wa kulia umetoa sadaka gani ama kiasi gani.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 05, 2012

    Sikubaliani kwamba kutoa kidogo kwa wasanii wetu ni tatizo. Kawaida unarudisha kwa jamii kidogo katika kile ulichopata kutoka kwa hiyo jamii. Wasanii wetu wanapata kidogo kutoka kwa jamii hivyo tutegemee watakachotoa kitakuwa relatively kodogo kwani sehemu kubwa ya haki zao tunaziiba. Tukiwawezesha watatoa kingi.

    Tatizo ni ile kujitangaza wakati unatoa msaada. Hiyo Mwenyezimungu hapendi kwani unakuwa kama haufanyi kwa ajili ya sadaka ila kutaka kuonekana (Riya)

    Kwa upande mwingine kujitangaza inasaisaidia kuhamasisha wengine kutoa kama walikuwa hawajaona. So kama unatoa kwa ajili ya Mwenyezimungu si vizuri kujitangaza ila kama unataka kuhamasisha uchangiaji mimi sina tatizo na kuonesha kwenye media

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 05, 2012

    Hiyo ya kupekuliwa kabla ya kuingia kanisani si Nigeria tu hata hapa Kenya hali ndo ilivyo!!!! Nionavyo mimi Al Shabaab is giving excuses for people not going to churches!!!! I hope hii hali haitafika Tanzania lakini the way things are going hatuko salama hata kidogo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 05, 2012

    na wengine walienda kununuliwa mayeboyebo karioakoo, jamani charity nyingi huku zinaanzaishwa lanikini misaada iktoka wanatumia wenyewe kwa manufaa yao, kama kuna dada mmoja kajidai kuomba watu pesa toka pande zote za dunia ili awajengee darasa mayatima, yaani pesa alizopata ni soda an mayeboyebo tu zingine kaendea holidays

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 05, 2012

    WANDUGU WOTE UK NA HAPA BONGO:

    Ni muhimu tuelewe ya kuwa,

    1.Msaada ni kile chochote utakachotoa hata iwe SENTI MOJA ni ndogo lakini pia ni kubwa inapomfikia Muhitaji au yule aliyekosa!

    Wanasema LAKI SI PESA lakini ukweli unabaki pale pale ya kuwa hata SENTI MOJA NI PESA!

    2.Ni muhimu pia TUTOE KWA IMANI, KAMA SEHEMU YA IBADA IKIWEZEKANA KWA SIRI na sio kwa kutafuta MASLAHI YA KIDUNIA!

    DAIMA MUNGU NDIYE MLIPAJI !!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 05, 2012

    Mdau wa UK,

    Ewe mwana Diaspora 'mchovu' wa Majuu,

    Wewe mbeba mabox wa Majuu ni POUND ngapi umeshawekeza kwenye Jamii huku nyumbani Tanzania?

    Wacha upumbavu wako kabisa hapa, achilia mbali ya kudai kuwa wamejionyesha!

    Ninyi muwepo huko hamtoi msaada wowote huku nyumbani Tanzania!, Labda kuondoa wale jamaa (TANZ-UK na WAZEE WA KAZI UK walichangia Waathirika wa mafuriko mwaka jana mwishoni 2011 na mchango wao wa msaada tuliuona, wewe je ulitoa?)

    Ndio ninyi mnatumia muda mwingi na fedha zenu kwa anasa mnatumia ma POUNDS yenu kulewa tu huko UK.

    Hata kama mkija Bongo asalaleeeee,,,, watu wanakoma mnachukua wake za watu mnavunja ndoa za watu kwa POUNDS zenu za kubeba maBox huko UK, mkija hapa TZ mnajirusha muda wote ktk Klabu za Usiku za starehe hata familia na ndugu zenu wengi mnawatelekeza mnawakimbia mkija hapa Bongo.

    Hebu tueleze wewe menyewe acha kudai msaada wao hauzidi Laki wewe hata ELFU HAMSINI hujawahi kutoa !

    Uongo???

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 05, 2012

    Wewe Bwege wa UK mbeba mabox unadai pyeeee,,,Msaada wanaotoa hauzidi Laki, wewe hata Elfu Hamsini (Tsh. 50,000/=) huna moyo wala huwezi kuthubutu kutoa!

    Afadhali watu wanaotoka Marekani wanatoa ninyi wa UK kwanza mabahili sana!!!

    Zaidi hela hiyo ELFU 50 ukiwa hapa Bongo unawaza kulewa Baa !!!

    Kwenda zako kule!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 05, 2012

    Mie naona, nanyi mkapake rangi,mjenge choo,bila kusahau kuweka mapazia na mkishaondoka watuambie kunawaliokuja kimya! Maneno mengi hamna la heri kwenu! Sie tushatoa na mitandao ya jamii ipo bwerere ungejuwaje wapo Hananasif!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 05, 2012

    Hata kama wametoa kidogo, ndio walichoona watoe kuliko, na huwezi kucompare na ambaye hajatoa kitu. Swali langu ni kwa nini unatoa ambayo haijakamilika?, ulitakiwa uoneshe the specific blog. Kwa watu ambao hawatembelei blog nyingi hawawezi kujua, na cha msingi ungewaambia wahusika direct. Kumsema mtu pembeni ni unafiki.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 05, 2012

    Hata kama wametoa kidogo, ndio walichoona watoe kuliko, na huwezi kucompare na ambaye hajatoa kitu. Swali langu ni kwa nini unatoa ambayo haijakamilika?, ulitakiwa uoneshe the specific blog. Kwa watu ambao hawatembelei blog nyingi hawawezi kujua, na cha msingi ungewaambia wahusika direct. Kumsema mtu pembeni ni unafiki.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 05, 2012

    Mimi nipo ughaibuni natafuta riziki inshallah, pia nina toa mchango(tumekikusanya waulaya na waafrika) kila mwezi kwa ajili ya Hospitali fulani pamoja na vyuo vyake vitatu hapo bongo.Nikiwa likizo bongo huwa natembelea hospitali hiyo kuona miradi tunayoidhamini inaendeleaje, kwa sasa tunaipanua nyumba ya kulala kinamama wajawazito wanaotoka mbali vijijini wakae kabla hawajajifungua, tumenunua gari la Hospitali, tumeagiza jenereta kwani ya sasa imechoka, tumenunua vitabu kwa ajili ya maktaba zaidi ya paundi elfu kumi na moja, na miradi mingine mingi tu.Hata siku moja sijawakarabisha waandishi wa habari au kujianika, kwani tunachotoa ni ridhaa yetu, na mwenyezi Mungu atajalia tuendelee kuwasaidia ndugu zetu. Kazi yangu haiitaji kujitangaza hadharani, lakini kama mtu anatoa na anataka publicity that is fine by me, kibaya ni kama mtu anazo halafu ni bahili kusaidia wale ambao hawakujaliwa.
    Dr Gangwe Bitozi.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 05, 2012

    wewe uliyesama mtoa maada ana uvivu wa kike umezaliwa na Babako? acheni kuwazalilisha wanawake. Mama ako angekuwa mvivu ungekosa hewa ungekufa tangu uchangani. try to be gender Sensitive.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 05, 2012

    Namsupport sana mdau wa UK, wamezidi sana cheap popularity, hao watoto wanahitaji zaidi ya sembe na juice sasa media attention yote ya nini na msaada wenyewe una last kwa siku moja?

    Bravo mdau wa UK, wanaosema mambo ya mabox ni wakuhurumia, sijui wao wanabeba nini huku? jamii ya ajabu sana hii

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 05, 2012

    WAOSHA vinywa wengine wanavamia tu hata hawasomi vizuri hapo juu nalaumiwa kwa kusema mdau kama hakai UK.kwa kumsaidia nilimaanisha kwamba hapa uk watu hata kama ana mahela kibao utamaduni wao wengi ni kidogo ila at the end of the day ndo hayo ma Oxfarm mnayoyaona so haina haja kudharau misaada hata kama ni kidogo namna gani kwani utawafanya wengine wakate tamaa ya kusaidia.Utamaduni wetu ni kuchangia maarusi tuuuuuu ila kama hapa UK kila sehemu kuna kikopo cha misaada na contributions zao ni kidogodogo saana

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 05, 2012

    Kamera za nini tunapotoa misaada?

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 05, 2012

    Mbeba Ma Box wa UK

    Unapokuja Tanzania huwezi kufikiri kutembelea angalau Mabwe Pande kwa Wahanga wa Mafuriko na kutoa hata msaada wa Tshs. 10,000/= !

    Unapokuja hapa Tanzania kazi yako ni kwenda Bureau De Change unabadili tena POUND 50 , 50 (Pound Hamsini Hamsini),angalia ulivyokuwa bahili , halafu unaelekea Baa kutwa kulewa!.

    Muda mwingi ni kuwatambia watu hapo Bar na kupora wanawake wa watu na kuvuruga ndoa za watu kwa hela yako ndogo ya kubeba Mabox UK.

    Zikiisha unarudi Bureau De Change hadi Pochi likiwa jeupe unaenda Ofisi ya ndege unarudi UK!

    Ukiwa UK huna uwezo wa kutumua chochote Tanzania kwa msaada wacha kwa Jamii kwa ndugu zako tu ni mgogoro!

    Kwanza ukiwa hapa Bongo unawakimbia ndugu zako unawakwepa!

    Wewe unasema Mastaa wa Bongo wanasaidia Tshs. 100,000/= , wewe huna Ujasiri wala uwezo wa kusaidia Tsh. 30,000/= (Elfu Thelathini)!!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 05, 2012

    Nina wasiwasi hao wanaomtukana mtoa mada ndio haohao wanaotafuta cheap publicity kwa kutoa misaada ambayo hailingani na hadhi yao katika jamii. Utakuta mtu anapeleka miche miwili ya sabuni hospitalini na picha zake zinamwagwa magazetini na kwenye mablog. Huku ni kuwa-exploit watu wenye shida. Kama kutoa misaada, basi tutoe misaada itakayobadilisha maisha ya wale tunaowasaidia, siyo kutafuta publicity kupitia matatizo yao.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 05, 2012

    Mdau wa UK wewe Mbeba Mabox Bwege!

    Ukiwa UK huna uwezo wa kutuma Bongo hata Pound 1 kuwasaidia ndugu zako, achilia mbali Jamii na watu baki wengine!

    Ukija Bongo huna ujasiri wa kutoa hata Pound 1 msaada kwa Jamii!, kutwa unashinda Baa unawakimbia hata nduguzo unalewa na wanawake za watu na washikaji!

    Leo ndio wewe unashangaa Msaada wa Shs. 100,000/- wa Msanii wa Bongo ?

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 05, 2012

    Ni kweli kabisa nakubaliana na mdau wa UK. watu wanawatumia hao yatima kujionyesha tu hakuna lolote. Mapicha kibao kujionyesha tu. Kwani ukitoa msaada mpaka ujitangaze? kutoa msaada ni kama kutoa sadaka, hata biblia inasema unapotoa sadaka kwa mkono wako wa kuume hata mkono wako wa kushoto usijue.Hivyo watu tuache hiyo tabia inakera sana.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 05, 2012

    Wachangia mada WATATU wa mwanzo.

    Kama nimemuelewa vizuri alieanzisha thread, hapa suala sio unga, maharage na juisi, yaani chakula cha kila siku, ni kweli hawa watoto wanahitaji kula ya kila siku. Point ya huyu menzetu wa UK ni kuwa kuna mambo muhimu zaidi hawa watoto wanahitaji mfano, sehemu ya kulala. Nina hakika tukioneshwa mahali wanapolala sote tutasikitika, jingine ni mabafuni na vyooni,ni mazingira duni. Wanastahili sehemu inayopendeza pia, hivyo basi, kama nimemuelewa vizuri mdau wa UK. Hawa watoto waboreshewe mazingira wanamoishi yaani malazi, makazi, elimu na kadhalika, sio ugali na maharage, mchele na juisi tuu.

    Pia kuna suala la elimu yao, afya, na marupurupu ya wanaowaangalia, yote haya inabidi kuyaangalia.

    Jingine alilolisema ni kuhusu kutokutoa anuani za haya makazi ya hawa watoto, inabidi ''kupitia wao''. Anuani zitolewe hadharani ili na sie wengine pia tuende kwa muda wetu tukatoe michango yetu, sio lazima tupitie kwao.

    Kubeba box sio kosa jamani, ili mradi mtu anafanya kitu mwenyewe anaona ni sawa, halali na kinampatia ajira na ujira.

    Kuna wahangaikaji wengi tu wapo nje ya nchi zao wanahangaika na maisha ugenini. Sio kosa mtu ''kubeba box'' whatever that means.

    Tuache kejeli na jazba, tuangalie kwa undani zaidi wengine wanasema nini, na pia tuheshimu maoni ya kila mtu sio kutoa kauli zenye mitizamo ya dharau na kejeli

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 05, 2012

    ahsante mdau wa UK kwa kweli hata mimi huwa nawaza kwa nini hawa viyoo vya jamii wasiwe na umoja wao kila baada ya muda flan wakatoa kitu cha maana kwa watoto badala ya juiv=ce na biscut za kuwaozesha meno???
    hata Mungu alisema toa kwa mkono wa kulia na wakushoto usijue. mi sidhani km wako sawa kuwaita waandishi wa habari coz of juice na cheap products. acheni show off bwn kidogo ulichonacho toa ila si kwa show off km za hawa wapendwa
    mdau 2--uk

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 06, 2012

    MDAU WA UK TUNAKUUNGA MKONO KABISA,MIMI NILISHANGAA SANA STAR KAMA HUYO ANABEBANA VIROBA VYA MCHELE NA SODA,UMEAMUA KUTOA MSAADA NA UNAUEWEZO,WASAIDIE YATIMA SEHEMU NZURI YA KUISHI AU KWENDA SHULE TUACHANE NA MASIFA YA WATU WAONE UMEJITOLEA KUMBE WAPI?AU BASI UNGEENDA KINYEMELE SIO KUKERA WATU HAPA.VIROBA VYA MCHELE AIBU SANA TUMIA TU WEWE NA FAMILIA YAKO.MDAU UK.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 06, 2012

    Si bora ya hao angalau wameweza kaonyesha moyo wa kutowa, kama wanajionyesha au vyovyote vile ulivyoweza kuwajaji wewe, basi MOLA pekee ndie ajuwae katika nafsi zao wametowa kwa dhamira gani, isitoshe na fungu lao kesho watakwenda kulikuta huko mbele twendako. Je wewe wa unaejiita MDAU UK mwenye machungu nao, UMEWAHI JAPO KUTHUBUTU?

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 06, 2012

    Baadhi yenu mliotoa maoni hamfikirii kwa kina!! Wewe mdau wa UK ulietoa hii maada pengine ni kwa vile uko UK ndo maana unaona laki si kitu. Kwani mara yako ya mwisho kutembelea bongo ilikua lini??? Kipato cha wasanii wetu nyumani ni kidogo sana kulinganisha na huko UK, kama alishakwisha kusema mdau hapo juu.. wanasanii wanarudisha kidogo wanachokipata kutoka kwa jamii.... Na misaada kama hiyo wanayoitoa ni muhimu sana(basic needs) kwa hao watoto yatima. Swala la kujionyesha pia nizuri kwa mtizamo wangu, maana inatuhamasisha na sisi, wanapata umaarufu vilevile watoto nao wananufaika, tatizo likowapi??. Kwa mfano usingeona usingekuja na hii maada... na sasa kwa maana moja ama nyinginge watu wanjifunza kitu hapa(great!!). Wewe kaa chini kua mbunifu/fikiria nijinsi gani kuhamasisha watu kutoa misaada badala ya kulaumu wanaojitolea na kuwavunja moyo. Kuwa UK kusikufanye ujione umewin maisha au kila utakacho kisema watu watakusikiliza, tunajua huko baadhi yenu mnatumika kama watumwa tu(slaves). mdau mtoa Facts apa!!

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 06, 2012

    Mithupu, wewe unasema huwa hubagui wala huchagui..., lakini ujumbe wangu umeutia kapuni.
    Dr Gangwe Bitozi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...