Ankal, hebu watupie wadau taswira hii ya waumini wa kanisa moja huko Nigeria wakipekuliwa kabla ya kuingia kanisani. Jamani amani tamu jamani. anayeleta chokochoko ya aina yoyote ili katika jamii hapa kwetu asionewe haya wala huruma.
La sivyo na sie yatatukuta haya tuanze kulia na kusaga meno...
Mdau Lagos
Mdau Lagos, asante sana kwa hii kali, ila hujatufahamisha ni nini hasa wanachokagua na wakikukutanacho adhabu yake ni nini ?? maana kwenye mabegi humu huwa kuna mambo mengi, sigara, bangi, kondomu.Au ndiyo yale ya enzi zile za Mutallabu na bomu lake kwenye chupi ?? maana Naigeria ni janja kweli kweli siyo hii ya kwetu janja dogo ya Arusha,hawa ni ngangali. Zebedayo msema kweli.
ReplyDeleteHiyo kali kwa mungu hakuna hayo, ila kwa mwanadamu na uovu wake inabidi iwe hivyo daa inasikitisha sana mahali tulipo fikia kwa sasa.
ReplyDeleteKwa nini wanapekuliwa?
ReplyDeleteMpekuaji inaonekana kama inamchukua muda mrefu kwa hao mabinti?
ReplyDeleteHii inakuja tu huku kwetu, nilimsikia kiongozi wetu akisema bora vita ili kurejesha heshima na hakuna aliyekemea. Ina maana tunakubaliana nae
ReplyDeleteAhsante sana mdau uliyetuletea habari hii.Hizi ndizo hasa habari za watu kuzielewa na siyo kila siku kusikiliza na kusoma habari za kipuuzi zisizo na maana wala fundisho lolote.(fulani kavaa nguo gani kapigana na nani ..nk)
ReplyDeleteUkweli habari hii ya Nigeria inatupa fundisho kuu tuelewe umuhimu wa amani na upendo katika jamii yetu ya Tanzania.Tujitahidi kujiepusha na hizi chuki zinazoanza kupikwa na wajanja wachache wenye maslahi yao wakizitumia dini ili watu tuwe maadui.Mimi nakumbuka nilipokuwa mdogo hatukuwa na hizi chuki za kipuuzi zinazopikwa hivi sasa.AGAIN THANK YOU VERY MUCH MDAU ULIYETUWEKEA HABARI HII
uzuri wa vita ni Jicho kwa jicho, jino kwa jino.Kila upande unaumia. Lakini haya ya kwetu, upande mmoja unatolewa meno bila majibu. Amani oyee!!!!
ReplyDeleteWatanzania kama kuku wakufugwa vile, tumezubaa zubaa tu, maneno mengiii,vitendo hakuna, waoga kama fisi vile(kasoro Jeshi letu ni kabambe).Mdau katoa picha inayojieleza, kama mtu unafuatilia habari za kidunia utaelewa kwanini hawa waumini wanapekuliwa,na nia hasa nikuzuia nini, tujibadili tuwe wajanja kaka kuku wa kienyeji!
ReplyDeleteJamani muwakumbushe wanasiasa wanaotaka kuingia ikulu kwa damu yetu wakihamasisha wafuasi wao kudai haki yao kwa nguvu.Ni wanasiasa haohao wanafanya vikao vya kuwahamasisha madakitari kuendelea na mgomo wakati siye twafa! Mheshimiwa kabisa
ReplyDeletekwa kweli dunia imefikia mwisho na pabaya sasa atamaliza saa ngapi ili misa ianze? kazi kweli kweli.
ReplyDeleteMbona hizo ni chuki za kidini wala sio siasa? Na humu Tz chuki za kidini zipo zinasubiri kulipuka tu. Haingii akilini useme kula kiti moto ni dhambi lakini kuua binadamu asiye na hatia eti kwa vile unatetea dini si dhambi. After all hakuna mtu aliyekatazwa kuabudu mungu kupitia dini yake, sasa chuki kwa wasio wa dini yako ni ya nini? Mungu atawalaani wote wenye imani za aina hii.
ReplyDelete