Hasheem Thabeet, Mtanzania anayecheza mpira wa kikapu Marekani amesaini mkataba wa miaka 2 na timu ya Oklahoma City Thunder..!!!
Watanzania ni wakati sasa wa kujivunia mafanikio ya baadhi ya watanzania wanaofanya vizuri katika viwango vya kidunia, katika historia ya michezo tangu tupate uhuru ni Hasheem Thabeet pekee ndio ameweza kufanikiwa na kucheza ligi ya juu kabisa duniani katika michezo.
Wako watanzania wengi wamefanikiwa katika michezo mbali mbali na kufanikiwa kucheza katika ligi za michezo mbali mbali na katika nchi mbali mbali ila kila mchezo una ligi zake ambazo ni za kiwango cha juu juu kabisa ni yeye pekee ndio amweza kufanya hivyo kwa kufanikiwa kucheza mfululizo.
Hasheem amecheza timu za Memphis na baadae kucheza Houston Rockets na mwshoni mwa msimu uliopita alicheza Portland Trail Blazers. Katika timu ya Blazers alicheza michezo yote 16 liyokuwa imebaki kabla ya msimu kumalizika.
Hasheem kwa sasa ndio mwafrika mwenye kiwango cha juu kabisa miongoni mwa waafrika wanaocheza kikapu Marekani na ni mchezaji pekee anayecheza huko toka ukanda wa Afrika , Mashariki, Kati na Kusini. Hasheem ni mchezaji wa Afrika ambaye ameingia NBA akiwa na kiwango cha juu kabisa katika historia ya mchezo huo, yaani No. 2 NBA Draft ya 2009.
Kwa Hasheem kuchukuliwa na timu kama Oklahoma City ambao ni mabingwa wa kanda ya magharibi ya NBA na mwaka huu walicheza fainali ya ubingwa wa NBA na kushindwa na Miami Heat, inaonyesha jinsi ambavyo bado mchezaji huyo anathaminiwa na bado uwezo mkubwa wa kuisaidia timu kubwa kama OKC ili iweze kufikia malengo yake.
Hivyo basi kwetu sisi Tanzania tunampongeza na kujivunia mafanikio hayo. Hasheem pia amekuwa ni mchezaji pekee wa kiwango cha juu ambaye amekuwa akirudisha fadhila nyumbani na kila anapopata mapumziko huwa anarudi nyumbani kuja kushirikiana na watanzania wenzake ili kuwainua na kuibua vipaji.
Kwa niaba ya shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania, natoa pongezi nyingi kwa Hasheem na tunamtakia kila heri na tumuombee kwa Mungu ili afanikiwe zaidi katika kikapu.
Mungu Mbariki Hasheem, Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
Phares Magesa
Makamu wa Rais
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF)
Tunakupongeza sana mkuu, lakini tunaomba ongeza bidii mluu, tunaojua hili gemu na kulifuatilia kwa makini, hataunapocheza dalili inaonyesha unakazi kubwa sana huko uendako, maana hata mshahara watakao kupa unaonyesha thamani yako kwa sana, ila kama unajali pesa hizo tu kwa sasa poa, lakini kwa malengo ya muda mrefu jifue mkuu unaweza kufanya mambo makubwa kuni ulifanya kabla ya kuingia NBA, Kila la kheri ni hayo tu!
ReplyDeleteBig Up Haseem .Tuwekeze kwenye ligi ya kikapu, si mpira wa miguu tu ,kunamichezo mingi .
ReplyDeleteSemeni na huyu anabeba boksi
ReplyDeleteArudi afanye mazoezi na wenzake safari za kujirusha bongo apunguze
ReplyDeleteIt's all good for him and we are proud as always, but it does not hurt to be frank with him at times. Hasheem work harder and prove people wrong! We will always be proud but individually you are capable of much more.
ReplyDeleteWazee wa hapo juu i support all your contributions towards our brother Hasheem.Man i tell you this, i am a fun of basketball and soccer and i go to watch communities practice here in columbus for streets games. Man they work hard, unfortunately that does not apply to our brother. As one contributor state above "if you satisfied with what you have, then you are good now" but if you want to have your own legacy look up on Mutombo, Ewing now Ibaka and move to soccer such as Drogba and others.
ReplyDeleteThey are many who saw money as you had now and they were quickly satisfied and quickly disappeared such as Samaki Walker and others.
I would like to see you doing big not only in NBA but also back home so you can be a sign for the future generation in sports.
Thanks
Columbus-Ohio
Thunder wakachukua ubingwa msimu ujao hivyo kuna dalili hasheem akapata ring
ReplyDeleteNi muhimu sana kumpa support kijana wetu. Ushauri kwake ni kuongeza mazoezi kwa nguvu. Naunga mkono mbiu hii ila Phares usipotoshe umma kwa kusema Hasheem ndie mchezaji pekee mwafrika aliyebaki! Wapo kina Ibaka (Senegal) na Sefoloza (South Africa) wa OKC, na wako very proactive!
ReplyDeleteNi kweli Hasheem anatuwakilisha sana ukizingatia michezo mingine tumeshindwa kung'ara kimataifa lakin Magesa hapo juu ameipamba mno taarifa hiyo. Hashim kwa sasa mshahara umeshuka sana toka kiasi cha dola millioni kwa msimu hadi laki 8 na ushee katika mkataba huu mpya. Nafurahi kuwa amepata mkataba manake ilikuwa inatia wasiwasi lakini thamani yake ndo hiyo! Mchezo wake umeonekana kupanda akiwa Portland lakin bado hajafanya vitu vya kumfanya aongezewe dakika za kucheza.Nadhani Oklahoma kutamfaa kwa kuwa ni vijana wajitumao na Serge Ibaka kama mwafrika mwenzake watapeana msukumo.
ReplyDeleteIbaka anatoka Congo Brazaville na ndiya mkali ktk waafrika kwa sasa!
Hivyo Hasheem bado ana kazi kubwa na watanzania tumuombee aibuke na apewe nafasi ya kuonyesha uwezo.
Mdau wa kikapu,HT
Sahihisho:Hapo juu mkataba wa mwanzo ni dola miliioni nne!
ReplyDeleteMdau HT
Sahihisho:Hapo juu mkataba wa mwanzo ni dola miliioni nne!
ReplyDeleteMdau HT
Hongera saaana Mwanandugu Kaka Hasheem Thabit!
ReplyDeleteMenyezi Mungu akufungulie zaidi.
Tuwakilishe!