SEKOUTOURE KHALIFA MNDEME
(24th Julai, 1965 -- 10 July, 2011)
Kaka kipenzi SEKOUTOURE KHALIFA MNDEME (Baba Khalifa); leo hii, tarehe 10 Julai, 2012, ni mwaka mmoja tangu ututoke.
Ni ukweli kuwa umetutoka kimwili, lakini ndani ya mioyo yetu bado ungali nasi. Kumbukumbu ya upendo na mwongozo wako unaendelea kuwa dira kwa siye ambayo umetuacha, tukisubiri siku ya kukutana nawe mbinguni kwa Allah.
Unakumbukwa na daima utaendelea kukumbukwa na mkeo kipenzi Bi. HALIMA HEMED MWAMTEMI, wanao wapenzi KHALIFA, HEMED na HAFSA ‘Dokta’; wanafamilia wote wa Omari na Sultani MUYANZA pamoja na ya MWAMTEMI.
Mungu na aendelee kuiweka roho yako, mpenzi Sekoutoure, mahali pema peponi – Ameen
allah akujaalie akulaze mahali pema peponi amin
ReplyDeleteakusamehe makosa yako na awape nguvu na subra wafiwa wote katika mtihani huu mzito kwao
innalillah wajna rajuun
Namwombea apumzike kwa amani milele.By shemeji yako Limbimbi.
ReplyDeleteTunamwomba Mwenyezi Mungu (SWT) amlaze ndugu yetu Sekou Toure mahali pema peponi. Amin. Poleni tena wafiwa. Ahmed Msuya.
ReplyDeleteNinakuombea Mwenyezimungu akuepushe na adhabu ya kaburi na atukutanishe kesho akhera inshallah.
ReplyDeleteNilishtuka sana nilivyopata habari ya kifo cha huyu Bw. Ilikuwa JUNI 2011 nilifika kazini kwake CRDB VIJANA BRANCH kwa nia ya kuomba maelekezo yake ya kupeleka pesa India ambako kaka yangu alikuwa amefanyiwa upasuaji. nikaambiwa yuko likizo, kumbe alikuwa mgonjwa. Kaka yangu aliyekuwa india alifariki tukamrudisha tukaenda kumzika nyumbani. Narudi Dar JULAI napata hbr za msiba wa huyu Bw.huyu na kwamba naye alipelekwa India. Huko India nako!!!!! AHH wote ndio njia tujiandae.MAUTI NI MLANGO KILA MTU ATAPITA, inna lillah wainna illaih rajiun.
ama kwa hakika kila nafsi itaonja umauti; Mwenyezi Mungu amlaze Toure mahala pema peponi Amin. Mkewe, wanawe na wanafamilia wote Mwenyezi Mungu awatie nguvu na Imani muendeleze yale aliyoyaacha, Amin.
ReplyDelete