Habari za Leo Ankal,
Naomba msaada wako wa kumpata mwenye Cheti hiki,maana alikisahau katika Stationary yangu pindi alipokuja kutoa Photocopy,ni muda mrefu sasa hajatokea na nahisi hakumbuki alikisahau wapi.
Naomba usaidia kupatikana kwake ili aje akichukue cheti chake.
awasiliane nami kwa namba hii
0654 969 715.
Asante kiongozi;Atapatikana tu...hapa ndipo kwenyewe haswaaa....
ReplyDeleteDavid V
ubarikiwe
ReplyDeleteNakupongeza kwa uaminifu wako na Mungu atakupa malipo unayostahiki kwa kitendo chako hicho.
ReplyDeleteNamfahamu huyu dada tulisoma nae Jitegemee nitajaribu kutafuta contacts zake.
ReplyDeleteHaya jamani hao wa UK mpooo ???? siku moja mashamba mmoja kutoka kwenu alisema humu humu kwenye blogi yetu kwamba , maana kuna mtu kutoka Italia alipoteza vitambulisho vyake. Huyo mshamba wa UK alisema hiviii !! bora angepotezea UK angevipata lakini bongo asahau !! Yaani we acha tu , nilikasirika mpaka tumbo likawa linaniuma. Zebedayo.
ReplyDeletehapa ni moyo wa mtu tu, na uaminifu, mambo ya kusema wa uk, hayapo, mtu anamuibia baba yake mzazi au mama yake na hao ndio wamemlea utasemaje ikikutokea kwako, ukapoteza kitu kupitia ndugu yako wa karibu?
ReplyDeleteMungu akubariki kwa uaminifu wako. Na ukishindwa kumpata huyu mtu kiarifu chuo chake IFM, watakuwa na contacts zake ili wampatie. Asante tena sana kwa uaminifu wako, jamani tunahitaji watu wengi kama hawa, na inatia moyo kwamba hata kwetu wapo!
ReplyDeleteJamaa keshanunua cheti kingine, hiki hana kazi nacho tena. Nenda kakifungie chipsi dume tuu.
ReplyDeletewe umesema kweli hapo ni moyo wa mtu na uaminifu tu! utamaduni wa wazungu, wakiona kitu cha mtu wanakiweka vizuri na mwenyewe anaweza kukipata akifuatilia! hapo nyumbani siku hizi imani kwa wengi imepotea, labda ndio mana huyo wa uk alisema hivyo, ila hata uk mtu anaweza kupoteza na asikipate, inategemea amepoteza kwa kuangusha, au kusahau, ukisahau kitu sehemu ujue utakipata kwa asilimia 90, isiwe pesa tu. ila vitu vingine unaweza kuvipata, naomba wengi hapo nyumbani tuwe na moyo huu kama wa huyu mwenzetu.
ReplyDeleteHaya ndiyo mambo mazuri yakuigwa na kuenziwa na watanzania. Mungu akubariki ndugu kwa ukarimu na wema uliotenda kwa mja wake.
ReplyDeleteJamani huyu aliyekiokota anamiliki stationary yake. Kwa hiyo anaangalia business yake zaidi ndio maana mdau anabahatika kupata cheti chake. Ingekuwa kwingine angesahau hiyo ni dili
ReplyDeletepole ulipoteza kitu kupitia ndugu wa karibu "kikulacho ....." ila kuhusu uaminifu wa dar na uk mdau mwingine ni kwamba dar kiwango cha kukosa uaminifu ni kikubwa. kumbe huyu angechukua cheti apeleke wapi? angeacha hata 500 aone kama angetafutwa! unalete utani ee!
ReplyDeleteASANTENI SANA WANDUGU WOTE , KWELI NASHUKURU SANA KWA UAMINIFU WAKO, MAANA SIKUWA NAKUMBUKA CHETI CHANGU KILIKUWA WAPI, YAANI SINA MANENO MENGI YA KUSEMA ILA ASANTE SANA , SANA.
ReplyDeleteNDIMI HONORATHA SAWERE
DAR ES SALAAM.
Ukiangalia vizuri hiki cheti utaona kwamba tarehe imechakachuliwa. namba 7 imebadilishwa kuwa namba 2. Jiulize kwanini?
ReplyDelete