Rais wa Rotary Club Arusha Profesa Justin Maeda akitoa maelezo mafupi katika tafrija fupi ya kukabidhi Taa za Solar zipatazo 50 zilizotolewa kwa ajili ya shule ya msingi emboreet iliyopo Simanjiro,Jijini Arusha.
Rais wa Rotary Club Arusha Profesa Justin Maeda akibadilishana bendera za lotary club na mtoto wa mwanachama wa Rotary club ya Tewkesbury ya uingreza.
mkurugenzi mkuu wa Helvetic Solar Contractors Patric Ngowi pamoja na mkurugenzi wa ufundi wakitoa maelezo mafupi juu ya utumiaji wa taa za solar wanazoziuza.
Baadhi ya wanafunzi kutoka Uingereza wakishuhudia makabidhiano ya taa za solar jijini Arusha.
Katika juhudi za kusaidia maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla, wadau mbalimbali jijini Arusha wamechangia taa za solar 50 katika shule ya msingi ya emboreet ya wilaya ya simanjiro, mkoani Arusha.
Akizungumza katika tafrija fupi ya kukabidhi taa hizo jijini Arusha, mwalimu Shilar toka shule ya Royal ya nchini uingereza alieleza kuwa baada ya kufanya kazi na shule ya msingi emboreet kwa muda walipata ombi la kusaidia taa za solar kwa ajili ya kusaidia wanafunzi kusoma nyakati za usiku kwani eneo hilo halina umeme.
Katika juhudi za kutafuta pesa, shule yake ya royal ya Uingereza pamoja na Rotary club Tewkesbury ya uingereza zilifanikisha kupatikana pesa.
Aidha mkurugenzi mkuu wa Helvetic Solar Contractors bw. Patric Ngowi alieleza kwamba mwaka jana walipata ombi la kuuza taa za solar toka kwa Shilar.
Kwakuwa malengo ya ununuzi wa taa hizo ni kusaidia shule katika nchi, uongozi wa kampuni uliamua kuwa taa zitauzwa kwa asilinia 70 ya bei yake halisi na asilimia 30 iliyobaki itakuwa ni mchango wa kampuni katika shule hiyo.
Pia alieleza kuwa taa hizo ni rahisi kutumika, vilevile ni taa zinazoweza kuwaka kwa masaa 14. Taa hizo zinaweza kutumika kuchaji simu, hivyo kuongeza mawasiliano katika sehemu hiyo.
Rais wa Rotary club ya Arusha aliwashukuru mwalimu Shilar, lotary club ya Tewkesbury ya uingereza na Helvetic Solar Contractors kwa kuwezesha kupatikana kwa taa hizo.
Alisisitiza kuwa taa ni kitu kimojawapo kikuu cha kumsaidia mwanafuzi katika kujiendeleza kimasomo. Akasema hii itakuwa ni chachu kwa wazazi na wanafunzi kujifunza zaidi ili kujisaidia wenyewe na taifa kwa ujumla.
Anawaasa wadau wengine kujitokeza na kusaidia maeneo mbalimbali ili kusaidia kuondokana na ujinga na pia umaskini.
Profesa maeda aliongeza kuwa club ya Arusha itaendelea kushirikiana na Rotary mbalimbali duniani katika kusaidia maendeleo. Pia lilifanyika tendo la kubadilishana bendera kati ya Rotary club ya Arusha na Rotary club Tewkesbury ya uingereza .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...