Kwa msomaji yeyote naomba atambue kwamba mimi ni mpenzi mkubwa wa club yangu ya Simba sports.

Nimekuwa nikufuatilia sana tena kwa karibu kabisa hii sarakasi ya Simba,Yondani, Yanga na TFF. lakini kikubwa kabisa ni haya maamuzi ya juzijuzi kuhusu mstakabali ya mkataba wa Kelvin na matamshi yake kupitia vyomba mbali mbali vya habari. siyo siri mimi kama Mtanzania wa kawaida kabisa nimeshangaa aina ya mkataba walio saini viongozi wangu wa Simba. 

Simba club kubwa tena kubwa kabisa inawezaje kusaini mkataba wenye mapungufu kiasi hiki lakini kibaya zaidi ni pale mtu mmoja anaposhidwa kwenda kuusajiri mkataba huko TFF. Simba siku hizi ina Katibu mtendaji, Mhasibu na watu wengine kedekede ambao wanafanya kazi za utendaji au haya hayapo tena ni mwenyekiti na makamu wake wanaendelea kuchapa kazi kama kawa----ni aibu kubwa tena sana kusikia madudu yanayofanyika Simba. 

tuwe wakweli kusema viongozi wetu hawajali kabisa kabisa club yetu. Amri Kiemba anacheza sasa kwa nguvu ya kocha na yuko sawasawa kweli, very discipline player lakini tunaambiwa kuna Kiongozi alikuwa hamtaki na Yondani nae yalikuwa hayohayo akaondoka Simba Yanga wakamsajiri huko mtaani----huyu Kiongozi ni nani? na haya mambo ya kiongozi kutomtaka mchezaji yataaisha lini Tanzania hasa Simba na Yanga?

Imeniuma sana lakini Yondani ni halali kucheza yanga, tuwe wakweli kwamba viongozi wa Simba ndiyo waliompeleka huyu kijana Yanga. hizo kelele zao za kwenda FIFA na mkataba mbovu huu zitatuabisha zaidi Watanzania.

Simba tujitazame kwanza utendaji na umakini kwenye mambo yenye maslahi na club yetu ikiwemo mikataba ya wachezaji. tuna watendaji kwenye club yetu tuwatumie basi.

Naitwa Denis Aristoto Mkereketwa wa Simba
Gaborone-Botswana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2012

    Kwa kumsaidia mdau ni kwamba Yanga wamemsajili Kelvin sio wamemsajiri
    ni Kusajili sio Kusajiri. Mmmmhhh tutafika na lugha yetu ya Kiswahili.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2012

    Kuhusu suala la Yondani, ni wazi kwamba viongozi wa Simba ndio waliamua aende Yanga na wanayoongea na kufanya sasa ni kujisafisha tu kwa wanachama. Kuna suala jingine linakuja kuhusu Okwi, huyu anangojea tu mkataba wake uishe Simba ili aende Yanga, viongozi wa Simba wanalijua hili na wameafiki lakini muda ukifika utawasikia wakileta USANII mwingine. Kama Simba hapatakuwa na viongozi makini, klabu hii haiwezi kupiga hatua.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2012

    kama ni club yako, si una maamuzi katika kilicho chako?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...