TASWIRA MBALI MBALI ZA MATOKEO YA MGOMO WA MABASI YA USAFIRISHAJI KATI YA ARUSHA NA MOSHI KAMA WANAVYOONEKANA ABIRIA WAKIWA KWENYE STAND KUU YA MABASI JIJINI ARUSHA WAKITAFUTA USAFIRI KAMA WALIVYOKUTWA NA KAMERA YETU. MGOMO HUO BADO UNAENDELEA KWA SIKU YA TATU SASA HALI INAYOLETA USUMBUFU KWA ABIRIA HAO AMBAO HATA INAWABIDI KUINGILIA MADIRISHANI KWENYE MABASI MACHACHE YANAYOFANYA KAZI, NA WENGINE KUIBIWA. INASEMEKANA MGOMO HUO UMETOKANA NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI KUPANDISHA USHURU KUTOKA 1000 -2000 BILA YA KUFIKIA MUAFAKA NA WAMILIKI HAO WA VYOMBO VYA USAFISHAJI MJINI HUMO. Picha na Mahmoud Ahmad, Arusha |
Home
Unlabelled
mgomo wa mabasi ya moshi-arusha wazua tafrani vituoni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mateso yote haya yanatokana na kukosekana kwa watawala ambao aidha hawana dhamira ya kuifanyia kazi dhana ya utawala bora au hawana uelewa wa dhana yenyewe. Utawala bora unakita katika misingi ya ushirikishaji (participatory and involvement) wadau mbali mbali katika maamuzi yanayowagusa. Inashangaza kuona ubabe ikitawala hadi sasa na matokeo yake ni usumbufu usiokuwa na sababu kwa wananchi.
ReplyDeleteKwani huo mgomo umetokea kwenye basi la Mtei pekee?
ReplyDeleteNi kweli Juu ya hoja hapo juu. Usumbufu mkubwa umetokea kwa mgomo huu kudumu kwa sikuhizo bila ufumbuzi wa haraka_Wanaokwenda kazini, mashuleni, hospitali, kazini, mashambani na kwengineko imekuwa adha kubwa! Wao wana magari yao wakipeta juu kwa juu bila shida ! Aidha uchumi umeyumba - mauzo mengi yamedoda kwani wadau wanshindwa kufikia masoko na huduma- mfano wauza mafuta wamekiona - kutoa gari takribani 200 si mchezo! Je nani atatulipa adha hii tuloipata! Mheshmiwa mstahiki Meya na Mkurugenzi manispaa mtujibu.
ReplyDelete