MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Nimroadi Mkono amekamilisha ahadi yake ya kupeleka Madawati mapya katika shule ya sekondari Butuguri baada ya kubainika kuwa madawati yaliyotengenezwa na mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika shule hiyo hayana ubora.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea awamu ya kwanza ya Madawati zaidi ya 50,diwani wa kata ya Butuguri Mwita Charles alimpongeza Mbunge huyo kwa kukamilisha ahadi hiyo huku akitoa wito kwa viongozi wengine kuiga mfano huo.

Diwani huyo alisema kuwa Madawati yaliyotengenezwa na TASAF hayana ubora na hivyo anaunga mkono kauli ya Mh Mbunge kuyarudisha Madawati hayo katika Halmashauri ya Musoma.

Kuhusu wale wote waliohusika katika ubadhilifu huo diwani huyo alisema kuwa wanatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa viongozi wengine ambao wapo kwa masilahi yao.

Naye Mwalimu mkuu Wa Shule hiyo Godfrey Robert alisemshukuru Mbunge huyo na kusema kuwa amesaidia kupunguza mzigo kwa wazazi katika kukabiliana na upungufu wa madawati uliokuwepo shuleni hapo.

Amesema Madawati yaliyokuwepo hayatoshi ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi waliopo katika shule hiyo,na hivyo mwaka huu walikuwa na mpango wa kutengeneza madawati hayo.

Aidha madawati yote yaliyotengenezwa na mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF tayari yamerudishwa katika halmashauri ya Musoma Vijijini kutokana na kutokuwa na kiwango kinachokubalika

Hivi karibuni akifanya ziara shuleni hapo mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Nimrodi Mkono aliyakataa madawati zaidi ya 1000 yaliyotengenezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kutokana na kutokuwa na kiwango chenye ubora

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2012

    YAANI YEYE NA UZANAKINI TU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Ahadi ni DENI na baadhi ya IMANI zetu tunaamini ni zenye kuja kuulizwa siku ya siku, the way zilivyotimizwa. Hongera sana Mh. Mkono kwa kuitimiza ahadi yako, mana kumi kwa mmoja hasa katika viongozi wetu, hutoa ahadi na matokeo yake ni kuhadaa. Ingependeza kama wataweza kuiga mfano wako au waache kabisa tabia yao ya kutoa ahadi hewa, hasa katika sekta mbali mbali za maendeleo ya Taifa letu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...