Uncle Issa Nahitaji Msaada kutoka kwa wadau..

nilipokua nikisafiri wakati niko kwenye transit hotel Cairo.. niipata nafasi ya kuogelea sasa maji yakaingia masikioni nikajaribu kurukaruka hayakutoka nikapanda ndege kuendelea na safari yangu mpaka nikafika leo ninasiku ya tano nahangaika sana kutoa yale maji lakini bado hayataki kutoka masikioni yananifanya nishindwe kusikia vizuri alafu sina balance ya kichwa naomba kama kuna doctor anaeweza ku recommend nifanyaje please anisaidie niko nchini kwa watu hata english hawajui nimejaribu kwenda clinic nikakuta hatuelewani....

Rogers Akatoeli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2012

    Ndugu wewe kwani umekulia wapi ? maana hilo siyo tatizo hata kidogo kwa sisi watu wa ziwa victoria. cha kufanya weka maji mengine ndani ya hilo sikio ,halafu inamisha kichwa chako mara moja upande upande sehemu ya sikio lenye maji,BASI !!! hayo maji mapya utakayoweka ,yata kilieti vaqumu na yatayavuta yale mengine ndani ya sikio na yatatoka-watoto tulikuwa tunafanya hivyo. Nijulishe kama nimekusaidia, mimi siyo daktari wala nini,machinga tu. Zebedayo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2012

    jaribu kulalia upande wa hilo sikio lililoingia maji usiku huu, make sure unalalia upande huo huo usiku mzima bila kugeuka...utashangaa tu maji ya moto yametiririka ghafla kutoka sikioni, huwa nafanya hivyo maji yakiingia sikioni kwangu na mara zote huwa inasaidia kuyatoa nikifanya hivyo. yasipotoka huna jinsi ndungu yangu, itabidi utafute mkalimani ikiwezekana, ila nenda hospitali.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2012

    Elekeza sikio lenye maji chini kisha gonga gonga kichwa opposite na ule wenye sikio lenye maji utaona matone yanatoka pole pole

    ReplyDelete
  4. Pole sana ndugu yangu kwa hali iliyokukuta.cha msingi fanya hivii..weka maji kwenye kiganja chako kisha yamimine kwenye lile sikio lililoingia maji hakikisha maji yameingia kwenye tundu ya sikio vizuri kisha kwa haraka inamisha sikio lako ili maji yatoke,hapo utaona na yale maji yaliyokuingia sikioni yanatoka pamoja na yale uliyoyaingiza.Ikishindikana kwa mara ya kwanza fanya tena.kama hukuelewa jinsi ya kufanya tafadhali wasiliana na mimi ili nikujulishe kwa njia ya simu.namba yangu ni +32 49 222 33 25 hata kama huna pesa kwenye simu yako fanya kunibeep then mimi nitakupigia.pole sana ndugu yangu kwa hali hiyo,najua jinsi unavyoangaika ila ni kitendo cha dakika tu kuyaondoa hayo maji.Hiyo njia ni rahisi na salama kabisa.natumaini kwamba utanielewa kama hukunielewa fanya mawasiliano nami.Maganga One.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2012

    Pole kwa tatizo hilo .Jaribu kulala upande wa sikio lenye maji na yatatoka .Jaribu kulalia huo upande kama dk. 10-15 hivi.Ikishindikana jaribu kumuona Dr. wa Masikio ,Koo na pua,huwa kuna mtaalamu wa kitengo hicho na ni tatizo dogo sana endapo utawahi.Kila la heri ,mdau na mtaalamu ktk medicine .Big Joe

    ReplyDelete
  6. Mama K, Mtoni, Dar es Salaam.July 21, 2012

    Haihitaji doctor kaka yangu...kwa sisi wa pwani tulozoena kuogelea baharini tunalitambua hili. Hayo majo yaliyomo ndani ya msikio yameweka kama ngome na ndio maana hayatoki...sasa cha kufanya achukue maji kidogo kama matone mawili matatu aweke kwenye sikio hilo lenye maji na haya maji utakayoyaweka yatavunja hiyo kitu kama ngome na yote yatatoka....na kama haitasaidia muone doc...

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 21, 2012

    Huko uliko,

    Sisitiza huko uonane na Wataalam wa (Head, Nose and Throat) 'HNT' ndio utapata msaada sahihi.

    Kama ungekuwa hapa Dar ningekushauri uende Magomeni mwembe chai kwa Dr.Ole ,Dakitari mmoja Mmasai Bingwa wa masuala hayo ana hiyo Hospitali anaendesha.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 21, 2012

    wewe mdau wacha uzushi wako na ulimbukeni wa safari eti natafuta doctor wa kunisaidia kwani hii ni site ya madokta?

    eti nimeenda kliniki hawajui english hahahaha kuna sehemu ikakosa hata mtu wa kukusaidia kuongea hicho kilugha cha hapo?

    wacha kutujazia ukurasa wa ankali kwa vitu vya kijinga wewe mchimba chumvi rudi kwenu ukapigwe na vumbi

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 21, 2012

    Unapenda starehe Unaogelea hadi ukiwa safarini. Huko unakoishi hakuna madaktari. Au unataka madaktari wa mtandaoni tu?
    Ushauri wangu ukome kufanya starehe za kuogelea ukiwa safarini.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 21, 2012

    Wacha fiksi ww labda umeenda viclinic cya vichochoroni. Misri imetawaliwa na waingereza na majority wanao gea kiingereza. Itakuwaje ukose wa kukuelewa?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 21, 2012

    Ndugu yetu,

    Wewe hujui kuogelea halafu unazama bila utaratibu.

    Kuogelea kuna basics zake za kufuata isipokuwa kwa chura na samaki wao kimaumbile wameumbwa tayari kwa maisha ya maji na hawahitaji maelekezo kama sisi viuombe wengine ambao maji sio makazi yetu!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 21, 2012

    wewe usiwe mjinga kiasi hicho chukua maji kwenye kiganja chako fanya laza sikio kiubapa kamavile unataka kuyaingiza sikioni tena kabla hayajaingia vizuri inamisha sikio chini yatatoka yote na yaliyokuwa ndani,jaribu nipe jibu au nipigie kwenye +255713450966 nikuelekeze vizuri

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 21, 2012

    unatakiwa uzibe pua yako alafu usukume pumzi nje na hayo masikio yatafunguka

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 21, 2012

    Ndugu Rogers,

    Naomba uwe mkweli omba usaidiwe lakini sidhani kama katika mahospitali ya Cairo hakutakua na daktari anaelewa kizungu au ni wewe umeshindwa kujieleza kizungu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJuly 21, 2012

      hivi mwenzetu darasani ulikuwaga unakuwa wangapi? umesoma vizuri lakini alichoandika au jazba tu na kusikia mbongo kaogelea nje ya bongo haaa haaaa

      Delete
  15. Ziba pua na mdomo halafu fanya kama unameza mate mara kadhaa then nipe majibu

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 21, 2012

    Rogers Akatoeli tafadhali nitafute kwa namba 0654037007 nikusaidie

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 21, 2012

    kwa umbile la sikio jinsi lilivyo hayo maji hayaendi kokote zaidi, nadhani kinachokusumbua ni hali ya kutojisikia vizuri na kutosikia ktk kipindi hiki kuanzia sasa jaribu kulalia upande huo huo wa sikio lililokua na maji kutokana na mgandamizo mkubwa wa joto maji yatatafuta njia na yatatoka yakiwa ya ujoto, ni vizuri ukawa mtulivu yaache yaishe taratibu hakuna kubwa zaidi la kutisha zaidi ya kutojisikia vizuri tu.

    ReplyDelete
  18. Duuh wengine wanapaka na wengine wanatoa ushauri haya kazi kwenu..

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 21, 2012

    fuata ushauri wa juu wa kutia maji kwenye kiganja kwa sababu ni bubbles zimefanya kwenye ear canal mara tu ukitia maji zile bubble zitapasuka na maji yatatoka yote.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 21, 2012

    duh...pole sana...zeee zeee doktaaaz wamegomaaaaz

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 21, 2012

    Mtu kaomba msaada kidogo kelele nyingi msaada hakuna, kweli utu umekwisha. Na wewe ndugu yangu hata mkalimani hakuna?

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 21, 2012

    Kwani ulivyokua unaondoka uliaga vizuri kwa Mzee nanii?

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 21, 2012

    Rogers, umefurahisha sana jamvi leo hata mimi nimepatamo na mambo mapya, hizi ndizo mada nzuri za kuchekesha na kupeana maarifa,angalia mimi ,nilikuwa naijua njia moja tu ,kumbe ziko nyingi !!! Hongera sana Michuzi kwa kutoibania hii mada ya jamaa Roger, sipendi zile mada za kubishania dini, au Muungano-hizo mada zinaleta chuki na wala hazichekeshi,halafu watu wa UK wanakuwa wakali ukiwakosoa. Zebedayo

    ReplyDelete
  24. Pole sana ndugu yangu
    fugua bomba la kuogea la maji ya mvua (shower) inamisha kiwa upande wa sikio lenye maji fungua bomba maji yatoke kwa nguvu kidogo yawe yana ingia kwenye sikio lenye maji kama dakika 2 hivi nafikiri maji yote yatatoka unaweza kurudia mara 2-3 hivi mpaka maji ya ndani yatoke yote kama hujaelewa nibip nikupigie nikuelekeze zaidi 8190 4422 8555

    ReplyDelete
  25. Rogers AkatoelJuly 22, 2012

    Jamani Asante hiyo njia ya kuongeza maji imenisaidia maji yametoka..... God Bless you all.. Alafu sorry to say this mtu unapokua na shida lazima uwe desprate sana, ni mara yangu ya kwanza kufika kwenye hii nchi ya Souther Mongolia hakuna watu wanajua english zaidi ya hotelini ambako wameita tax tax ikanipeleka clinic kufika hapo ndo hatuelewani kabisaa.. hivyo sio uzushi

    ReplyDelete
  26. Jamani mtu ameomba msaada wa tatizo lake, kwa nini kumsimanga?eti hakuna mkalimani, alikuwa wangapi darasani, aliaga kwao.... yote haya ya nini?? Angewaomba hela je?

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 22, 2012

    Rogers,
    Mshukuru Zebedayo na Mama K,sio tu wamekuelewa ila wamekupa ushauri mzuri. Umeona lakini wale waliodhani bado uko Misri? Umeona wale waliokupa ushauri wa dkt bila kukwambia useme kwa kiingereza kwa hao madkt? Maana hoja ilikuwa hiyo. zebedayo alianza vizuri baadae akapagawa na Sangara!
    Zebedayo, umeona daraja la mbagala leo? Mti tu na mfereji umejaa taka halafu useme Bongo kumekucha!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 22, 2012

    Pole ndugu, pamoja na kashfa kibao lakini angalau umefanikiwa. Ila hapo juu kuna jamaa nae kachakachua! Eti kasema ukawaone madaktari mabingwa wa HNT (Head, Nose and Throat) ...... Aise? Ndugu yangu ni ENT (Ear, Nose and Throat).... Darasa la bure hilo mdau. Shukran Ankal, kweli blogu yako ni Shule ya aina yake. Twajifunza mengi humu ati......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...