KWA mara nyingine, Watanzania tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kuzama kwa meli ya MV. Skagit iliyotokea jirani na kisiwa cha Chumbe, Unguja. Ndugu zetu wapatao 60 tayari wameripotiwa kupoteza uhai. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa letu.

Mjengwablog, kama chombo cha jamii cha habari na mawasiliano kinatoa salamu za rambirambi kwa wahanga wote wa msiba huu mkubwa. Na tunachukua fursa hii kumpa mkono wa pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, vivyo hivyo, mkono wetu wa pole umfikie Mheshimiwa Dr. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar.

Mjengwablog inaungana na Watanzania wote katika siku hizi tatu za maombelezo kwa kutorusha habari na picha za matukio yenye kuashiria sherehe na burudani.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2012

    Oleaginous? me thinks!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2012

    Napita tuu!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2012

    michuzi mkuu wewe mbaguzi sana tena sana tumeandika comment zetu umetuwekia kapuni huyu jamaa wa juu kakuandikia maneno hata hatuyajui umeiweka comment yake, kwani blog yako sisi hatuna haki ya ku post comment zetu.

    acha ubaguzi wewe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...