KWA mara nyingine, Watanzania tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kuzama kwa meli ya MV. Skagit iliyotokea jirani na kisiwa cha Chumbe, Unguja. Ndugu zetu wapatao 60 tayari wameripotiwa kupoteza uhai. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa letu.
Mjengwablog, kama chombo cha jamii cha habari na mawasiliano kinatoa salamu za rambirambi kwa wahanga wote wa msiba huu mkubwa. Na tunachukua fursa hii kumpa mkono wa pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, vivyo hivyo, mkono wetu wa pole umfikie Mheshimiwa Dr. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar.
Mjengwablog inaungana na Watanzania wote katika siku hizi tatu za maombelezo kwa kutorusha habari na picha za matukio yenye kuashiria sherehe na burudani.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.
Oleaginous? me thinks!
ReplyDeleteNapita tuu!!
ReplyDeletemichuzi mkuu wewe mbaguzi sana tena sana tumeandika comment zetu umetuwekia kapuni huyu jamaa wa juu kakuandikia maneno hata hatuyajui umeiweka comment yake, kwani blog yako sisi hatuna haki ya ku post comment zetu.
ReplyDeleteacha ubaguzi wewe