London Interbank Offered Rate (LIBOR) ni makadirio ya kiwango cha riba kinachotumika wakati benki zinapokopeshana pesa. Kiwango hicho cha riba kinatumiwa na mabenki yanapokopeshana kwa kulipa mikopo ya muda mfupi na muda mrefu (siku moja, mwezi hadi mwaka) Kiwango hicho kinawekwa na British Bankers’ Association (BBA) kila siku saa tano asubuhi kwa time za Uingereza.

Taasisi za pesa wanapotoa mikopo, credit card au (Mortgage) kumkopesha mteja nyumba, wanawatoza wateja kiwango cha riba kulingana na kile kiwango cha riba kilicho pangwa na BBA (LIBOR) au wanaongeza zaidi. 

LIBOR kwa kawaida inatumika kama kigezo (benchmark) cha kiwango cha riba kwa pound ya kiingereza na sarafu za nchi nyingine nyingi. Kinachofanyika ni kwamba kila siku, benki 16 zinatakiwa zitaje kwa wawakilishi wa mabenk (BBA) kiwango cha riba (borrowing cost) kinachotozana pindi mabenki hayo yanapo kopeshana.

LIBOR imezusha mjadala mkubwa kuhusu uhalali wake na vigezo inavyovitumia ktk kufanya kazi kwake, kwa mfano gavana wa bank ya England Mervyn King ameripotiwa akisema ‘wakati umefika kwa LIBOR kubadilsha utendaji wake wa kazi kutoka kwenye makadirio na kwenda kwenye kuangalia jinsi soko la biashara lilivyo ili kujua vipi riba inaweza kukadiriwa.

Moja ktk vitu ambavyo vimekua na mshituko mkubwa kuhusiana na utumiaji wa Libor ni pamoja na ile ya kutozwa faini ya pound 290 million Barclays bank kwa kile kilichodaiwa kwamba kwa makusudi wameweka kiwango maalum cha LIBOR (kufix) kwa maslahi ya bank hiyo. 

Kwa mujibu wa taarifa rasmi mbalimbali ambazo zilizoandaliwa Marekani na uingereza zimeeleza kwamba, kulikua na mazungumzo kati ya viongozi wa juu wa Barclays na viongozi wa mabank mengine ambapo ilidawa kua bank nyingine zilionyesha wasiwasi wao kutokana na kiwango cha riba cha Barclays kua juu ukilinganishe na kile cha bank nyingine.

Kufuatia maelezo hayo tumeona ipo haja ya kulizungumzia swala zima la LIBOR kwa ujumla na uhusiano wa LIBOR na bank za kiislam kwa ufupi. Tukirudi kwa upande wa bank za kiIslam, wasomi wengi wameonyesha waiwasi wa kutumia LIBOR kwa sababu kuna mazingira ya riba ambayo hayakubaliki kisheria. 

Pamoja na mambo mengine, mwaka 2011 Islamic bank ilifanikiwa kupata the Islamic Interbank Benchmark Rate (IIBR). Kwa ufupi, IIBR ni kiwango cha faida ambacho kinakubalika na Mabank kwamba kimekamilisha masharti yanayokubalika na sheria ya kiIslam, Mabank yanafanya hivyo kwa kukubali kutoa na kupokea kiwango hicho kulingana na hali halisi ya soko la biashara. 

Makadirio ya kiwango hicho yanafanyika kabla kidogo ya saa tano asubuhi kwa taimu za Makkah ambayo ni sawa na taimu za (GMT + 3).

Kinachotokea ni kwamba kinanyakuliwa kiwango cha Mabank 16 na Thomson Reuter saa 10. 45 AM kila siku kuanzia Jumapili mpaka Al khamis. Bank zinaombwa zitaje kiwango chao kati ya saa 9.00 AM- 10.44 AM kwa taimu za Makkah ,na zinatakiwa zijibu maswali yafuatayo. 

Ni kiasi gani cha faida yatapenda kushiriki kwa ajili ya inter-bank ambayo inafuata sheria ya kiislam na je yatakubali kuuza na kununua kwa kiwango hicho kwa muda wa siku moja au wiki moja na kuendelea. 

Baada ya hatua hiyo, Thomson Reuters inajiridhisha kwamba utaratibu umefuatwa kwa kufanya audit na kwa kuhakikisha kwamba kiwango kilichotajwa ni sahihi na wanachukua wastan utakaopatikana ktk Mabank hayo 16 na kiwango hicho kinatumiwa kupatikana IIBR. 

Tofauti nyingine ni ile ya sheria ya kiislam kuzuia kamari (speculation) na hadaa (gharar), na kuzuia biashara ambazo sio halali kisheria. Faida ya mtaji ktk uchumi wa kiIslam inategemea jinsi gani mjasirimali atakua tayari kukubali hasara inayotokana na biashara na sio kutegemea riba. 

Upande mwingine ni ule unaohusiana na kuuza deni pamoja na kutaka uhakika (guarantee) ya faida, hilo haliruhusiwi ktk sheria ya kiIslam na badala yake mifumo mingine ya kibiashara inaweza kutumika kama vile Mudarabah na musharakah.

Kufuatia scandal ya LIBOR bado inaendelea na kuna uwezekano mkubwa wa kuchukua muelekeo mwengine kabisa ktk wakati wa baadae lakin hadi sasa, mwenyekiti wa Barclays Marcus amejiunzulu Jumatatu ya tarehehe 2/07/2012 na mkurugenzi (Chief executive) wa Barclays Bob diamond nae amejiunzulu kufuatia shinikizo la wanasiasa. Kwa maelezo zaidi na ushahidi wa hayo soma www.ijuebankyakiislam.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2012

    unatoa taharifa jina lako hujaandika hapo chini au wewe ndio walewale wajuaji nini?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2012

    hapa ndio utaona kuwa dini ya uislam ilipokemea suala zima la RIBA kuwa ni haramu huu ndio ukweli

    dini hii ya kiislam ilishajuwa madhara ya riba sasa mpaka mataifa ya magharibi yanaanza kugunduwa leo hii na adhari zake bado zinakuja zaidi

    jiepushe na hii haramu kwani iko wazi kwakweli wewe maskini unakwenda kuomba msaada baada ya wao kukusaidia wanazidi kukuongezea matatizo vipi hii isiwe haramu na ndio dini yetu ya kiislamu ikapiga vita saba hii RIBA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 09, 2012

    Kwa kawaida uchumi wowote ili uweze kukidhi mahitaji, ni lazima kuwe nauwiano kati ya mahitaji ya binadamu na faida iliyopo ktk uchumi huo. hakuna faida ya uchumi ambao baadhi ya tabaka ktk jamii inafaidika sana na baadhi nyingine inateseka kwa sababu ya mpangilio mbaya wa kiuchumi au kwa sababu ya kutojali mahitaji ya binadamu na malengo hasa ya kuumbwa kwake.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 09, 2012

    Uchumi wa Msingi wa Riba:

    Hebu tujiulize bei ya vitu sokoni haina mtu anayeratibu na kuipanga hutegemeana na DEMAND and SUPPLY yaani,,,(Mahitaji na Upatikanaji).

    Kinachofanya RIBA (interest)ya Kibenki isikubalike ni kuwa haiheshimu kanuni hii ya Masoko wakati fedha ni bidhaa kama zilivyo bidhaa zingine kwa kuwa ina thamani (utility of value).

    Hivyo RIBA tunayoielewa ktk sehemu zote hadi kwenye Mabenki inapangwa kwa Misingi ya Tamaa na Ubinafsi!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 09, 2012

    Ina maana kama Uongozi wa Barclays uliwatoza Wateja kiwango cha juu, wao walikula cha katikati!

    Tuseme Riba ni R
    Kama LIBOR ilipendekeza R% huku Barclays wakiwachaji Wateja N%ambapo R<N:

    Ina maana Wizi na Ufisadi waliochuma Barclays ulikuwa ni:-

    R=N%-R%

    Kwa taraimu kama LIBOR wanaweka 10% halafu Barclays wanachaji kiwango cha juu mfano 15% ina maana (15%-10%=5%) ile ya juu 5% ndio waliyokuwa wanawaibia Wateja Dunia nzima!

    Je, itakuwa ni POUNDS Biloni ngapi hizo kwa miaka yote hiyo ya wizi?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 09, 2012

    Ukitaka kusoma ubaya wa Riba soma Riwaya ya Merchants of Venice!

    Jinsi Shylock Mfanya Biashara wa Kukopesha Fedha wa Kiyahudi,

    1.Alivyokuwa akimwapiza Mkopaji amkate sehemu ya mwili wake kufidia hasara endapo angeshindwa kurejesha Mkopo kwa kiwango alichopangiwa (cha Riba) ktk mudaliokubaliana!

    2.Alivyokuwa na uchu wa faida kwa kufikia kuwa anakadiria kiwango cha Riba kwa uzito wa unywele wake ktk Mzani wa Kupimia!

    Hapa ndio utaona ya kuwa Uchumi wa mfumo Riba ni Unyama!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 09, 2012

    tujiulize kwa nini mfumo-riba wakibenki ndiyo unaotamba duniani kuliko mifumo mingine isiyotaka riba.

    wataalamu wa ngambo zote yaani mfumo-riba wa kibenki na wale wanaosema mfumo-usio-riba wa kibenki, tujuzeni kwa nondo za uhakika ili tujikwamue kwa kutafuta riziki.

    mdau
    maisha- magumu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...