Soko la Ngarenaro Mjini Magugu wakionekana  wachuzi na wanunuzi  wakiendelea na biashara na wengine wakinunua bidhaa kwa mahitaji ya nyumbani. Wananchi wameitaka Halmashauri kuliendeleza soko hilo liwe la kisasa badala ya  kama ilivyokutwa la kamera yetu Magugu, Wilayani Babati Vijijini.
 Power Tiller  likiwekwa wese kwenye sheli moja mjini Magugu, Babati, mkoani Arusha. Serikali imetakiwa kuangalia kabla madhara hayajatokea kwani inahatarisha usalama wa wananchi walio pembeni na sheli hiyo. 
Picha na Mahmoud Ahmad wa  Globu ya Jamii,  Babati Vijijini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2012

    NAOMBA KUWAKUMBUSHA KUWA BABATI IKO MANYARA SIO ARUSHA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 12, 2012

    WANAJITAHIDI HIVYO WAPONGEZWE, KWA KUWA BABATI NI MJI MKUU WA MANYARA NA MANYARA NI MKOA NAOMBA SHUGHULI ZIFANYWE KISASA/KIMAENDELEO SIO KAMA KIJIJINI. PIA SEHEMU YA KUUZIA MAFUTA YA MAGARI/MASHINE NI KITUO CHA MAFUTA SIO SHELI, SHELI NI JINA LA KAMPUNI MOJA YA MAFUTA AMBAYO KWA SASA HAIPO TENA HAPA TZ. WATANZANIA TUSIPENDE KUSEMA AU KUTAJA/KUITA VITU MAJINA BILA KUJUA USAHIHI WAKE, HAYA MAZOEA YA KUJISEMEA CHOCHOTE YANATUTIA AIBU, WALA SI MPAKA USOME SANA, K.M. PENYE MZUNGUKO ZINAPOKUTANA BARABARA UTASIKIA PALE "KEEP LEFT" SIO SAWA NI "ROUND ABOUT", KEEP LEFT MAANA YAKE NI KUWA UPANDE WA KUSHOTO WA BARABARA, SASA HII NI KOTE SI MPAKA ZINAPOKUTANA BARABARA. TUJITAHIDI MBONA ASIYEENDA SHULE KABISA SI BUBU ANAONGEA NA KUELEWEKA NA ANAFANYA KILA WAJIBU WAKE KATIKA MAISHA YAKE?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...