PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA SHAMRASHAMRA ZA MWENGE WA UHURU ULIPOKUWA KATIKA MBIO ZAKE KATIKA MKOA WA MOROGORO AMBAPO KATIKA WILAYA MPYA YA GAIRO, ULIPOKELEWA KWA HESHIMA ZOTE KUTOKA KWA WALINZI WA JADI KWA KUONESHA NAMNA WALIVYOIVA KATIKA KUPAMBANA NA UHALIFU KATIKA MAENEO YA VIJIJI VYAO KWA KUUNDA VIKUNDI VYA ULINZI SHIRIKISHI.
Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii
 Walinzi wa Jadi ' Sungusungu' kutoka Vijiji mbalimbali vya Wilaya mpya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro wakionesha namna ya kutambaa chini wakati wa kusaka wahalifu.
 Walinzi wa jadi ' Sungusungu' Kata ya Idibo, Wilaya mpya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro wakisubiri amri
 Jeshi la walinzi wa Jadi ' Sungusungu' si mwanamke wala mwanaume kazi ni moja tu ulinzi imara wa wananchi
 Maofisa wakike wa JWTZ wenye vyeo vya Kapteni wakifurahia mapokezi ya Mwenge wa uhuru eneo la Pangawe, Wilaya ya Morogoro
Wanajeshi wa JWTZ , Pangawe wakishiriki zoezi la kushika Mwenge wa Uhuru ulipokuwa ukipita eneo la Kambi hiyo hivi karibuni ukitokea Morogoro Vijijini kwenda Manispaa ya Morogoro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2012

    Sungusungu na ndala? ha ha haaaaa...........Usanii huo!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2012

    Swali la kizushi hivi ni kwanini asilimia kubwa ya wanajeshi wana sura mbaya?

    au sura zao mbaya ndio vigezo vya kuamua kufanya kazi ya jeshi ili wafanane na kazi zao?

    nauliza tu ankali kwa roho safi usinichukie.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2012

    labda wanaotoka kwenu, wanaotoka kwetu mahandsome ile mbaya

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2012

    Mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya zote za moro..tunataka kuona mashule mazuri yanajengwa na mahospitali mazuri..tunaomba mkae pamoja na wabunge wote ili mwangalie wapi mlipokwama ili muweze kutatua hayo matatizo..na hatutaki tena kusikia jina la manispaa tunataka moro liwe jiji la mfano na mtoke mwende sehemu kama vile south africa mkaone wezenu kwa jinsi majiji yao yalivyo.. kila la heri...ni mm wenu masikini wa kipato lakini tajiri wa mawazo endelevu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2012

    aah wangekuwa wamevaa kininja wala usingejua kama ni wabaya au la. lakini beuty is in the eyes of the beholder. mimi nampenda huyo wa kwanza kulia aliyeweka mikono mfukoni. Ankal naomba unipatie contacts zake.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2012

    Hongera! Hongera! Sungusungu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...