WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII INAWATANGAZIA MADAKTARI WOTE WANAOFANYA MAFUNZO KWA VITENDO (INTERNS), WALIOPEWA BARUA ZA KURUDISHWA KWA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII, WANATAKIWA KURIPOTI MAKAO MAKUU YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII IFIKAPO SIKU YA IJUMAA TAREHE 6 JULAI, 2012.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
3/07/2012
Kwa kawaida serikali huwa haiyumbishwi, hao vijana wakishindwa kuripoti hadi kufikia siku hiyo iachane nao ili wakaajiriwe huko wanakokupenda na 'liwalo na liwe', na ninaamini kuwa hawatakuwa na mafanikio kwa vile watakuwa wamekosa radhi za mzazi wao ambae ni serikali. Kuzidi kuwabembeleza ni kuitia aibu serikali na wataendelea kufanya hivyo kila siku kufuata maagizo ya huyo 'Bwana' yao!!
ReplyDeletetumesoma kwa mgomo kuanzia siku ya kwanza tunapojiunga chuo na nikawaida tunagoma na kisha wanatuita kwa barua kujieleza na baada ya mwaka tena tunagoma.udhoefu tuliojengewa na serikali katika suala la migomo vyuoni ndio tunautumia sasa.na unaweza mburuta punda mtoni ila huwezi mlazimisha kunywa maji.ngoja tuone mechi itakavyokuwa.
ReplyDelete