.Wateja wa mtandao wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania watanufaika na ofa ya mwisho wa wiki.

.Manufaa ni kuhusu kupiga simu,kutuma ujumbe mfupi, na huduma ya hifadhi habari kwa Shs, 250/- tu

Manufaa ni kwa mwisho wa wiki kuanzia Ijumaa saa 5 usiku hadi Jumatatu saa 1 asubuhi.

Dar es Salaam 21/07/2012 .Wateja wa Vodacom Tanzania wana sababu ya kufurahi kipindi cha mwisho wa wiki kufuatia kuanzishwa kwa huduma mpya ambayo itawaruhusu kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi kwa gharama ya Shs. 250/- tu.

Huduma hii ni kwa mwisho wa wiki kuanzia Ijumaa saa 5 usiku hadi Jumatatu saa 1 asubuhi kwenda mitandao yote.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza huduma hii imekuja kufuatia kubaini kwamba watumiaji wa mtandao huu huhitaji huduma hizi kwa masaa mengi zaidi na wakati mwingine mpaka usiku mwingi.

"Tumekuja na huduma hii ili tuweze kuhakikisha kuwa tunawaridhisha wateja wetu na papo hapo wafurahi na wale wawapendao," alisema Meza.

Mkurugenzi mtendaji huyo aliongeza kuwa Mtandao wa Vodacom Tanzania unaona faraja kwa wateja na hivyo kuwa na hali ya kuwapa upendeleo mahsusi wateja wake ili kuongeza idadi ya watumiaji.

Huduma hii inakuja wiki moja baada ya kampuni hii kuzindua huduma nyingine inayowalenga vijana wa Kitanzania ambayo inatilia mkazo wa matumizi ya mitandao ya kijamii.


"Wateja wetu tayari wananufaika na matumizi ya bure ya mtandao wa kijamii wa facebook, twitter na wikepedia kupitia huduma ya "phoneson kwa wajanja". Pia tumeingia ubia na kampuni ya Nokia ili kuwawezesha vijana kupata huduma rahisi ya mtandao yaani Internet sambamba na mauzo ya bei ya chini ya simu aina ya ZTE ambazo zinauzwa hadi Shilingi 13,000/- yote hii ikiwa ni kutaka kuwapa raha wateja wetu," alimalizia Bwana Meza  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...