Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Injinia William Mhando akionyesha moja ya nguzo za umeme zinazotumika kwa uwizi alioubaini katika maeneo mbali mbali ya Jijini Dar.
Fundi wa Tanesco akikata Umeme katika nyumba iliyokuwa ikiiba Umeme.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Injinia William Mhando (pili kulia) akisikiliwa maelezo ya Mmoja wa wakazi wa nyumba Iliyokuwa ikiiba umeme.
WIZI wa umeme kwa njia ya mtandao umemfanya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Injinia William Mhando, kuingia mitaani kushiriki zoezi la ukaguzi wa mita za wateja.
Akiwa kwenye zoezi hilo ambalo kwa wananchi lilionekana si la kawaida kutokana na kufuatana na baadhi ya mameneja na wataalamu Mhando alisema wamepokea taarifa ambazo si nzuri za wizi wa umeme kwa njia ya mtandao hali iliyomlazimu kufuatilia kwa makini tangu ngazi ya chini kabisa.
Mhando alisema tangu kuanza kuzifanyia kazi taarifa hizo wamekamata watu 2 Dodoma na 3 Dar es Salaam ambao kesi zao zimefikishwa mahakamani wakituhumiwa kutumia umeme ambao haujulikani umenunuliwa wapi.
“Utakuta mteja amenunua umeme wa Sh10’000/ kwetu lakini unapokwenda kukagua utakuta anaumeme wa zaidi ya pesa hizo, nah ii inamaanisha kuna sehemu zingine wananunua tofauti na Tanesco ambapo kwenye mfumo haupo,” Alifafanua Mhando.
Alipoulizwa kuhusu sababu za kuwepo kwa tatizo hilo Mhando alisema tuna wasiwasi kuwa mtaalamu aliyekuja kuingiza mfumo huo aliacha program mtaani na kufanya watu wenye nia mbaya kutumia nafasi hiyo.
Hata hivyo Mhando alisema tatizo hilo limegundulika haraka kutokana na mita maalum (Automatic Meter Reader) zilizofungwa ambazo husomwa moja kwa moja kwenye Tanesco bila ya kwenda kwa mteja na ndio maana tatizo hilo limegundulika haraka.
Aidha alisema wameanza kufunga mfumo mwengine wakudhibiti wizi aina hiyo kwa kufunga kifaa maalum (Supply Group hold) ambacho hadi sasa kimefungwa kwa wateja wakubwa 3000 jijini Dar es Salaam na kudhibiti wizi wa aina hiyo na zoezi hilo litaendelea kwa wateja wakawaida.
Mbali na wizi wa mtandao Mkurugenzi huyo alishuhudia wateja waliojiunganishia umeme kabla haujafika kwenye mita na kuamuru watendaji wake kukata umeme huo huku akiamrisha jeshi la polisi kuwachukua na kuwafungulia mashitaka ya wizi, ambapo mama mwenyenyumba mmoja na Meneja wa Baa ya King Paris walichukuliwa na polisi.
Katika eneo la Keko mbali na nyumba za kawaida umeme ulikatwa kwenye nyumba za wageni pamoja na Baa mbalimbali zikiwemo baa ya Miami Shambwe na Baa ya King Paris zilizopo kwenye eneo hilo.
Nae Meneja wa kanda hiyo ya Temeke Richard Mallamia alisema hasara inayotokana na wizi wa umeme ni zaidi ya Sh80Millioni ambapo tangu kuanza kwa zoezi hilo wamefanikiwa kukusanya Tsh40Millioni kutokana na faini pamoja na ukusanyaji wa madeni.
Zoezi hilo ambalo ni endelevu linatarajia kukamata watu zaidi ili kuweza kufidia hasara ambayo shirika linapata kutokana na wizi.
Tanesco hukusanya mapato mengi zaidi ya 80% kutoka kwa watumiaji wakubwa waumeme ambao ni 20% ya wateja wote na ndio sehemu waliyoanza kufanya udhibiti wa ufungaji wa vifaa maalum vya kuzuia wizi.
jamani tanesco nisaidieni ,miminina mpangaji kwenye nyumba yangu dar es salaam boko amekaa mwaka sasa,kinachoshangaza ni kuwa amedisconnect luku umeme unawaka kama kawaida,amedisconect maji anaiba maji,nimeripot tanesca tangu mwaka jana cha kushangaza walikuja mwaka huu kuukata umeme,lakini bado yule mzee tena ni age ya babangu anao umeme sijui anautoa wapi luku inasoma zero imefikia kumwambia ahame potelea mbali nibaki na madeni yangu nitakuja kulipa,hataki hata kuhama,sasa sijui pa kuanzia wadau naombeni ushauri mi nimehamishiwa kikazi niko mkoani.nikitaka kumfungulia mashtaka nianzie wapi maana hadi naumwa kichwa kwa ajili ya huyo mzee rweyemamu.michuzi nisaidie.0783 30 80 37
ReplyDeletekwa maisha yalivo magumu lazima watu watafute njia ya kupunguza makali mbona tunasikia na serikali huwa hawalipi madeni ya tanesco? kama kiongozi halipi mwananchi wa kawaida afanyeje?
ReplyDeleteOnge na Mkurugenzi Tanesco William Muhando atakusaidia hilo tatizo ni mtu msikivu hasa kwa watu wanaohujumu Tanesco.Usikate tamaa.
ReplyDeleteNdugu yangu wee, hii blogi yetu tukufu ni ya kukutana kuchangia mada mbali mbali za kimaendeleo ya nchi yetu na dunia kwa ujumla, na pia kama umepata nondozz au unatafuta mchumba au unauza nyumba na gari au kiti chochote >yaani kwa kifupi ni globu ya jamii sehemu ya kustarehe na mazungumzo ya watoa mada.Sasa wewe unataka kumgeuza Ankal kuwa shu shu shu. haya mambo uliyoyataka ni kazi za FBI siyo michuzi blogi, ndugu yangu ,kweli una nia nzuri lakini mada hii siyo ya hapa kwenye blogi , wewe nenda huko makao makuu kawaone wahusika wa ngazi za juu au nenda polis, mbona siku hizi shughuli za kutapeli zinazidi kukabwa koo ??? nazinapigwa vita kweli kweli kila kona-bingeni ndiyo usiseme. Tukimlimbikiza Ankal kazi za kufuatilia waharifu, itabidi aanze kutembea na bodigadi. Zebedayo msema kweli.
ReplyDeleteNikupe pole sana. Unajua tatizo kubwa ni wafanyakazi kutokuwa wazalendo na taasisi wanayoifanyia kazi. Huyu mzee ninahisi anafungamana na wafanyakazi wa TANESCO wasiokuwa na uzalendo na shirika lao na bila shake ndio wanaomsaidia.
ReplyDeleteTuanze somo la uzalendo kutoka shule za awali tukilenga familia, jamii, taifa na pale tunapofanya kazi.
Sasa Mhando ataiweza hiyo kazi kama wahusika ni wafanyakazi walio chini yake?
Tanesco inabidi muelewe asili ya tatizo hili au mtakuwa mnatwanga maji kwenye kinu na zoezi kama hili litakuwa ni sawa na moto wa makaratasi tu unawaka na kuzimika chap chap. Kwanza ni bei ya umeme. Kwa kipato cha wananchi wengi nchini ni vigumu kumudu gharama hizo kwa sasa. Hivyo wizi huu utatulia kidogo tu ila hautakoma . Pili, ni huduma zenu mbovu na mtandao wenu kusumbua kila mara . Mtu una hela zako unaenda kununua umeme saa tatu usiku unaambiwa network haipo! Ebo !!!! Sasa ulale kiza na hela zako mfukoni ? Hebu jipangeni vizuri huko ndani mwenu kabla ya kukurupuka kwa staili hii
ReplyDeletehe mdau, unateseka nini? peleka mahamani huyo babu.
ReplyDeleteHuyo fundi wa tanesco mwenyewe mbona hajakaa kikazi, amepanda huko juu kama sio fundi vile.
ReplyDeleteHapo ndio mjue kwamba ufisadi upo katika kila ngazi ya jamii. Kuanzia kwa wananchi wa kawaida, wanafunzi mashuleni na vyuoni, wafanyabiashara, viongozi na wasio viongozi maofisini, wanasiasa wa kawaida hadi viongozi wa serikali. Kwa mtaji huo tusiwalaumu viongozi wetu kwa ufisadi. Tuanza kujisafisha sisi wenyewe kwanza.
ReplyDeleteKwa ugumu huu wa maisha lazima tuwaibie tu. Maisha magumu sa tufanyeje na umeme tunautaka. Hakuna mtu mwenye kipato atatumia njia ya udanganyifu kupata umeme. Tutabanana hapo hapo.
ReplyDeleteMimi nilikuwa naweka madirisha ya grill katika madirisha ya nyumba yangu, sasa nikamuomba jirani nitumie umeme. Basi nikanunua luku nikampa fundi aweke, baadae akanipigia simu kwamba kumetokea katika luku ya jirani basi akatafuta fundi ili atengeneze, kumbe yule ni mfanyakazi wa tanesco ambae aligundua kuwa ni umeme wa kuiba unachukuliwe nyumba kwa uwani wakati sisi wote umeme wetu unachukuliwa kutoka nguzo za barabarani. Basi fundi akasema kwamba ile seal imefunguliwa na inabidi akatafute seal mpya ili airudisha, hivyo zikanitoka T.shs. 25,000/= ili akapate hiyo seal mpya. Hapa nilijua tu nilikuwa natapeliwa hivyo nilikubali kila nilichokuwa naambiwa mradi kazi yangu isisimame. Umeme kuimbiwa ni jambo la kawaida hapa mjini. Wafanyakazi wa TANESCO wengi ni weizi.
ReplyDeleteUmeme bei juu mno wakati unazalishwa kwa maporomoko ya maji ya Mungu,je mhando na watu wake wangetakiwa kuzungusha turbines!
ReplyDelete