Timu ya Tanzania ya Olimpiki, imewasili kwenye kijiji cha michezo ya Olimpiki kilichopo Stratford, London, ikitokea kwenye mji wa Bradford.  Timu hiyo ya Tanzania, iliweka kambi ya mazoezi katika Chuo Kikuu cha Bradford tangu walipowasili nchini Uingereza wiki mbili zilizopita, ikiwa tayari kuiwakilisha Taifa katika michezo hiyo ya Olimpiki 2012.  Timu hiyo ilipokelewa na Balozi wa Tanzania, nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe na maofisa wengine wa Ubalozi na kusindikizwa moja kwa moja kwenye kijiji cha michezo hiyo kilichopo Stratford, ikiwa tayari kwa maandalizi na ufunguzi rasmi wa michezo hiyo utakaofanyika siku ya Ijumaa 27/07/2012 hapa London.


Balozi wa Tanzania, Mheshimiwa Peter Kallaghe akiwa pamoja na Wanamichezo hao watakaoiwakilisha Taifa mwaka huu katika Michezo hiyo ya Olimpiki nchini Uingereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2012

    sawa hawa ni wanariadha wetu Hivi serikali haina nguo za ziada kuwapatia hawa wana riadha nilikua nikiwaona ona wakipita na matreki suit ya buluu kila kona ya Bradford tena maeneo ya Chuoni kabisa

    nikajiuliza hawa jamaa vipi sasa kumbe ni wana riadha wetu.

    Sijui wataruditena Bradford angalau warudi na suit

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2012

    Mbona picha hazifungukia ankali?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...