SERIKALI ya UINGEREZA imeahidi kuendelea kushirikiana na TANZANIA katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii ili kufikia malengo yake ya kukuza uchumi na kuwaletea maendeleo wananchi wake

Ahadi hiyo imetolewa jana Jioni JIJINI LONDON na waziri mdogo wa UINGEREZA anayeshughulikia maendeleo ya Kimataifa, STEPHEN O’BRIEN wakati akimkaribisha rasmi RAIS JAKAYA KIKWETE na ujumbe wake nchini humo kwaajili ya kushiriki mkutano wa kimataifa wa Uzazi wa Mpango unaoanza leo

Mazungumzo kati ya Waziri huyo mdogo wa Uingereza anayeshughulikia maendeleo ya Kimataifa STEPHEN O’BREIN na Rais wa Jamhuru ya Muungano wa TANZANIA STEPHEN O’BREIN umefanyika katika hotel ya CHUCHIL HAYATT REGENCY Jijini LONDON.

Katika mazungumzo yake na mgeni wake, Waziri huyo amesema serikali ya Uingereza itaendelea kuongeza misaada kwa Tanzania hususan katika mpango wake wa utafutaji wa gesi unaoendelea ili Tanzania iweze kunufaika na sekta hiyo

OBREIN ambaye amewahi kuishi nchini Tanzania, mkoani MTWARA, amesema kuwa serikali yake imeridhika na namna rais Kikwete anavyoshughulikia matatizo mbalimbali yanayoikabili nchi yake ikiwemo kupiga vita umasikini

Aidha Kiongozi huyo aliyekwenda kumkaribisha Rais Kikwete kwaniaba ya Waziri Mkuu wa nchi hii DAVID CAMEROON, ameisifu Tanzania kwa jitihada zake za kutekeleza kampeni ya uzazi wa mpango wenye lengo la kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto

Kwa upande wake Rais Kikwete ametumia fursa hiyo kuipongeza serikali ya Uingereza kwa kushirikiana na Tanzania katika Nyanja mbalimbali na kuishukuru nchi hiyo kwa ahadi yake ya kuendelea kuisadia nchi yake ili iweze kuboresha uchumi na hatimaye kuinua maisha ya wananchi wake

Katika hatua Nyingine Rais Kwete leo mchana atashiriki katika mjadala wa kutafuta njia bora na kukusanya fedha kwaajili ya kusaidia shughuli za uzazi wa mpango wakati wa mkutano wa kimataifa utakaojadili suala hilo unaofanyika leo katika ukumbi wa QUEEN ELIZABETH hapa jijini LONDON

Katika mpango huo unaolenga kukusanya zaidi ya dola za kimarekani BILIONI 14 kwaajili ya kuwafikia wanawake milioni 120 ifikapo mwaka 2020, Tanzania inahitaji kiasi cha shilingi Bilioni 140 sawa na dola emilioni 88 ili iweze kufanikisha mpango wake wa miaka mitano wa uzazi wa mpango kwa kuwafikia zaidi ya wanawake Milioni sita na laki sita nchini kote ifikapo mwaka 2015.

Rais Kikwete ni miongoni mwa wakuu wa nchi tatu kutoka Afrika walioalikwa kushiriki katika mkutano huo wa siku moja ulioitishwa na kudhaminiwa na Serikali ya Uingereza, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) na Taasisi ya Bill na Belinda Gates.

Mbali na Rais kikwete, viongozi wengine wa Afrika walioalikwa kwenye mkutano huo ambao pia utahudhuriwa na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroun ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Paul Kagame wa Rwanda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2012

    hivi uingereza inaisaidia Tanzania au zinasaidiana, au zinashirikiana. Manaake kuisaidia inamaanisha kutoa tu bila kupata faida.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2012

    Mhe. Raisi wetu JK msimamo wetu juu ya Msahariti ya Misaada upo pale pale, tunayo imani ndiyo hivyo hadi sasa.

    Hao jamaa Uingereza waje kwa Mipango ya tija na heshima kwa manufaa ya Tanzania na watu wake kama hiyo nia yao ya kushirikiana na sisi ktk Miradi ya Nishati ya GESI na MIPANGO YA KUPIGA VITA UMASIKINI tutakuwa pamoja na Uingereza na si vinginevyo!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 11, 2012

    Heko Mhe. JK !

    Ongea nao hao jamaa watushukie sisi Tanzania kibishara zaidi na kiuchumi!

    Uchumi tunao!, Tunayo nishati ya gesi kama Mwingereza anavyoshuhudia na wala asituchukulie sisi kama masikini.

    Je kwa mtaji huo wa mali yetu gesi tuliyonayo pana sababu ya kupewa Misaada kwa mashariti ya ajabu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...